ILIPOISHIA:
Nikiwa bado naendelea kuugulia,
nilisikia ndugu yangu mmoja akiniita kutokea dirishani, nikafunua pazia na
kuchungulia nje. Sikuyaamini macho yangu baada ya kumuona akiwa na yule
msichana tuliyesafiri naye, harakaharaka nikafungua dirisha huku tabasamu pana
likiwa limechanua kwenye uso wangu.
SASA
ENDELEA...
“Mambo Togo?”
“Safi, karibu,” nilisema huku nikitazama
huku nakule. Yule ndugu yangu alikuwa amesimama pembeni akikutazama kwa
zamuzamu.
“Samahani nina maongezi kidogo na wewe,”
alisema. Kwa hali niliyokuwa nayo, nilikuwa nikifikiria jambo moja tu
kutokakwake, mapenzi.
“Nisubiri kwa kule mbele,” nilimuelekeza
huku harakaharaka nikitoka na kuelekea bafuni. Nilijimwagia maji ya baridi kwa
wingi ili angalau nitulie kisha nikarudi chumbani na kuvaa nguo.
Nilijitazama tena kwenye kioo, bado
nilikuwa na alama za kuvilia damu usoni lakini sikujali, akili yangu ilikuwa
ikihitaji kitu kimoja tu kwa wakati huo. Nilitoka kimyakimya bila kumuaga mtu
yeyote mpaka nje.
Nikamfuata yule ndugu yangu na kumwambia
kwamba iwe siri yetu nitampa zawadi, nikamsisitiza kwamba asimwambie mtu
yeyote. Alikubali, nikamshukuru nakumfuata yule msichana ambaye alionesha kuwa
na shauku kubwa ya kuonana na mimi.
Tulitoka mpaka nje kabisa, sehemu ambayo
mtu yeyote aliyekuwa ndani asingeweza kutuona, akanikumbatia kwa nguvu na
kunibusu shingoni. Nilijikuta nikisisimka mno, nikawa nachekacheka tu mwenyewe.
Aliniambia kuna mahali anataka rtwende
pamoja kwa sababu alikuwa na jambo muhimu lililokuwa likimsumbua ndani ya moyo
wake. Nilimuuliza amepata wapi ujasiri wa kuingia mpaka kule ndani? Akaniambia
ilikuwa ni muhimu sana kuonana na mimi na ndiyo maana hakujali chochote.
“Huwa unakunywa pombe?” aliniuliza,
nikatingisha kichwa kumkatalia. Licha ya kujaribu mara kadhaa kunywa pombe za
kienyeji tukiwa Chunya, kiukweli kichwa changu kilikuwa kibovu sana, kiufupi
sikuwa na uwezo wa kuhimili pombe. Akacheka sana huku mara kwa mara
akinipigapiga begani.
“Chagua sehemu ambayo unadhani inaweza
kufaa kwa mazungumzo ya mimi na wewe, twende beach, Mlimani City au tutafute
‘lodge’ yoyote nzuri,” aliniuliza l;akini kati ya sehemu zote alizozitaja, ni
moja tu ndiyo niliyokuwa naelewa, beach. Sikuwa najua Mlimani City ndiyo wapi
na kupoje wala sikuwa najua huko ‘lodge’ ni wapi na kuna nini cha muhimu.
Waliosema ushamba mzigo, hawakukosea.
Ilibidi nimuulize ili anipe ufafanuzi,
akacheka sana, akaniambia Mlimani City ni kituo maalum cha kibiashara, mahali
ambapo kuna maduka makubwa, mabenki, migahawa ya kisasa ya sehemu mbalimbali za
starehe. Akaniambia pia kuwa neno lodge ni la Kiingereza lakini linamaanisha
nyumba ya kulala wageni. Nikashtuka!
“Unamaanisha gesti?”
“Ndiyo?” alinijibu huku akinitazama kwa
macho yake mazuri, ikabidi nijifanye sitaki nataka kwa sababu kule kwetu
kulikuwa na stori kwamba watu wanaoingia gesti wakati hawapo safarini ni wale
wahuni walioshindikana. Nikamwambia kwamba Mlimani City atanipeleka siku
nyingine, akanitazama tena usoni na kuachia tabasamu pana.
Japo jibu langu halikuwa la moja kwa
moja, nadhani alinielewa haraka nilikuwa namaanisha nini. Tuliingia kwenye
Bajaj, nikageuka huku na kule na
nilipohakikisha hakuna aliyeniona, nilimpa ishara kwamba tuondoke.
Kwa makusudi kabisa, aliniegamia
kimahaba huku mara kwa mara akiendelea kuniangushia mabusu ya hapa na pale.
Yaani kama angekuwa anajua kilichokuwa ndani ya kichwa changu, kamwe
asingethubutu kumwagia petroli kwenye moto.
Hatukwenda mbali sana, Bajaj ikaingia
kwenye jengo moja la kisasa, getini likiwa na maandishi yaliyosomeka Sideview
Hotel, tukashuka kwenye Bajaj, nikawa nashangaashangaa huku na kule, alinishika
mkono bila hata wasiwasi, tukaingia mpaka ndani ambapo alimfuata dada wa
mapokezi na kuanza kuzungumza naye.
Alimwambia anahitaji chumba kwa siku
nzima mpaka kesho yake. Nilishangaa kwa nini anataka tukae mpaka kesho yake
wakati anajua mimi ni mgeni na nilikuwa chini ya wazazi wangu. Hata hivyo,
sikutaka kumhoji chochote mpaka nipate nilichokuwa nakitaka.
Alitoa pochi yake na kuhesabu fedha,
akampa yule mhudumu, akatoka na funguo na kwenda kutuonesha chumba chenyewe.
Kilikuwa chumba kizuri mno, yaani pengine kuliko vyumba vya kwenye majumba ya
watu wengi sana. Picha niliyokuwa nimeijenga kichwani mwangu mwanzoni,
nilitegemea chumba kitakuwa kama vile vya gesti za kijiji, kitanda kidogo
chenye kunguni na kilicholegea, godoro chafu na jembamba sambamba na mashuka
makuukuu.
Kitanda kilikuwa kikubwa, juu yake
kikiwa kimetandikwa kwa mashuka meupe na mito mikubwa mizuri, chini kikiwa
kimepigwa marumaru safi nyeupe, huku taa zenye mwanga fulani mzuri zikizidi
kuyapendezesha mandhari ya chumba hicho, nikawa nashangaashangaa.
Sikuwa na habari kwamba mwenzangu bila
hata kuzungumza kile alichosema tunataka kuzungumza, ameshaanza kufaanya kazi
nyingine. Alikuwa tayari ameshavua blauzi yake na kubaki na bra, akawa anahaha
kufungua suruali yake iliyokuwa imembanana kulichora vilivyo umbo lake.
Nilijikuta nikitetemeka mwenyewe, hata sijui ni kwa nini, nikampa mgongo.
“Togo! Mimi mwenzio na...ku..pe...”
alishindwa kumalizia alichotaka kukisema, akagusanisha mdomo wake na wangu huku
mikono yake ikiwa imenibana kisawasawa kwenye kifua chake kilichosheheni. Kwa
kuwa rahma alikuwa amenipa ‘twisheni’ ya mambo hayo, na mimi sikutaka kubaki
nyuma, nilimpa ushirikiano, tukawa tunaelea kwenye ulimwengu tofauti kabisa.
Ile halai niliyokuwa naisikia mwanzo,
safari hii ilizidi mno, yaani nikawa naona kama nachelewa. Tofauti na Rahma,
huyu yeye hakuwa na aibu kabisa na kila alichokuwa anakifanya, alikuwa akifanya
kwa kujiamini. Akaninyonyoa manyoya yote kama kuku aliyechinjwa huku na yeye
akifanya hivyohivyo, muda mfupi baadaye, tukawa ‘saresare’ maua.
“Togoo!” aliniita kwa mshtuko huku akiwa
amepigwa na butwaa iliyochanganyikana na furaha.
“Kumbe upo hivi,” alisema huku
akinitazama kwa macho yake kama anasikia usingizi, sikuelewa kauli yake hiyo
ilikuwa ikimaanisha nini, lakini aliendelea kunimwagia sifa lukuki kwamba siku
ya kwanza aliponiona tu aligundua kwamba nina sifa za kipekee ambazo wanaume
wengine hawana.
Sikutilia sana maanani kile alichokuwa
anakisema, akili yangu ilikuwa ikiwaza jambo moja tu. Muda mfupi baadaye,
tuliianza safari huku mimi nikiwa ndiyo kiongozi wa msafara. Unajua kama una
kiu kali ya maji, hata ukipewa jagi zima unaweza kulifakamia lote mpaka liishe.
Hicho ndicho kilichotokea kwangu.
Ghafla nilishangaa akianza kugeuza macho
na kutupatupa mikono na miguu kama mtu anayetaka kukata roho, haraka nikashuka
chini na kuanza kumtingisha kwa nguvu huku nikishindwa hata namna ya kumuita
maana kiukweli sikuwa nalijua jina lake.
Kadiri nilivyokuwa namtingisha ndivyo
alivyozidi kulegea, mara akatulia huku macho yake yakiwa yamegeuka na kutazama
upande wa juu. Nilijaribu kusikiliza mapigo ya moyo wake lakini hayakuwa
yakipiga na hakuwa akipumua.
“Mungu wangu,” nilisema huku nikianza
kutafuta nguo zangu, harakaharaka nikavaa huku kijasho chembamba kikinitoka,
nikawa najiuliza nini cha kufanya maana tayari ulishakuwa msala. Hakuna ambaye
angeamini kwamba msichana huyo amekufa mwenyewe, wangejua kwamba nimemuua,
nilijikuta nikitetemeka mno.
Akili niliyoipata, ilikuwa ni kuondoka
haraka hotelini hapo bila mtu yeyote kujua. Nilichukua shuka na kumfunika kisha
nikafungua mlango. Nilitazama huku na kule, nilipoona hakuna mtu, nilitoka na
kuurudishia mlango, harakaharaka nikawa natembea kuelekea nje.
Kwa bahati nzuri, nilipofika pale
mapokezi, yule dada hakuwepo, nikatoka kimyakimya mpaka nje, nikaelekea lilipo
geti kubwa huku nikijitahidi kuvaa tabasamu la uongo ili walinzi wa hoteli hiyo
wasishtukie chochote.
“Aroo! We kijana... Aroo wewe,”
nilisikia sauti ya mlinzi wa nje ya geti la hoteli hiyo akiniita, moyo
ukalipuka paah!
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment