ILIPOISHIA:
Sikupata hata muda wa kujibu chochote, Raya
akanikumbatia kwa nguvu mwilini na kuanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili
wangu, japokuwa sikuwa tayari kwa alichokuwa anakitaka, nilijikuta kwenye
wakati mgumu mno, kwani ukichanganya joto la mwili wake na uzuri aliokuwa nao,
ukizingatia kwamba tulikuwa wawili tu, nilijikuta nikishindwa cha kuamua,
‘Jamal’ wangu naye akaanza usumbufu.
SASA ENDELEA…
Nilishindwa kujizuia, na mimi nikamkumbatia
Raya, kitendo ambacho kilimfurahisha mno, akausogeza mdomo wake kwangu, nami
nikafanya hovyohivyo, ndimi zetu zikagusana, nikamsikia akitoa migumo ambayo
ilizidi kuipagawisha akili yangu.
Japokuwa sikuwa mtaalamu sana kwenye mambo ya
kikubwa, nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu kumuonesha Raya kwamba na mimi
sikuwa mshamba, ‘amsha-amsha’ ziliendelea na hatimaye kipyenga kikalia
kuashiria kuanza kwa mpambano wa kukata na shoka, usio na refa wala jezi, huku
nikishindwa kuzidhibiti papara zangu.
Wakati nikijiandaa kusakata kabumbu, ghafla
mawazo juu ya Shenaiza na kilichokuwa kinaendelea kule nyumbani kwangu yalipita
kwa kasi kubwa ndani ya kichwa changu, nikashangaa ‘Jamal’ wangu ambaye muda
mfupi uliopita alikuwa ngangari ile kinoma, akianza kunywea na kupoteza kabisa
ukakamavu wake.
Raya ambaye tayari alishajiweka tayari kupokea
‘mashuti’ ya nguvu kutoka kwangu, alishtushwa na kilichotokea, akaacha kila
alichokuwa anakifanya.
“Vipi tena jaman mpenzi wangu, na..ta…ka…,”
alisema Raya kwa sauti iliyokuwa ikikatakata, ikitokea kwenye matundu ya pua
zake.
“Subiri kidogo,” nilisema kwa aibu kubwa,
sikuwahi kutokewa na hali kama hiyo hata mara moja, nikashangaa imekuwaje?
Sikupata jibu. Ili kuzuga, ilibidi niamke na kujifanya nataka kwenda
maliwatoni, nikamuacha Raya amelala palepale huku akiwa kimya kabisa, akionesha
kuugulia maumivu ya ndani kwa ndani.
Harakaharaka nilitoka na kuelekea choo cha
ndani, nikajifungia mlango na kuanza kutafakari kuhusu kilichotokea.
Nilijisikia aibu sana kwani sikujua Raya atanichukuliaje kama amenitafunia kila
kitu na kuniwekea kabisa mdomoni lakini nimeshindwa kumeza. Japokuwa ulikuwa ni
usiku sana na kulikuwa na baridi, nilifungulia maji ya bomba la mvua na kuanza
kujimwagia. Nilisimama huku maji yakiendelea kunimwagikia kwa zaidi ya dakika
tatu mpaka nikaanza kutetemeka kwa baridi.
Nikafunga bomba na kurudi chumbani ambako
nilimkuta Raya amelala vilevile kama nilivyomuacha. Nikawa najisemeshasemesha
ili ‘kuua soo’, nikajifuta maji na kupanda kitandani, nikamvutia Raya kifuani
kwangu ambapo alikuja mzimamzima, ni hapo ndipo nilipogundua kwamba kumbe
alikuwa akilia.
Lawama zake kubwa kwangu ni kwamba sikuwa
nikimpenda na ndiyo maana nilimfanyia hivyo lakini kiukweli, wala sikuwa
nimepanga hayo yatokee bali nilijikuta tu nikiishiwa ukakamavu.
Nikawa nambembeleza kwa maneno matamu na kwa
mara ya kwanza nikamtamkia kwamba nampenda sana japokuwa nilisema vile ili
kumtuliza. Alifurahi sana aliposikia maneno hayo kutoka kwangu, nikamuona
akitabasamu na kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, na mimi nikawa naonesha
ushirikiano.
Niliamini safari hii nitaweza kukata kiu yake
kwani ‘Jamal’ wangu naye alishaanza kuonesha ushirikiano, akawa anafura kwa
hasira na kunipa matumaini makubwa kwamba nitaifuta aibu kubwa iliyokuwa
inataka kunikabili.
Tuliendelea kufanya ‘warm-up’ kwa dakika
kadhaa lakini safari hii Raya alionesha kutotaka kuchelewesha tena mambo, kabla
hata kipyenga cha kuashiria kuanza kwa mpambano hakijalia, yeye alitaka
kujianzishia mpira mwenyewe.
Katika hali ambayo sikuitegemea, mawazo juu ya
Shenaiza yalijirudia tena akili mwangu, nikawa sijui nini kilichoendelea baada
ya mimi kuondoka, kama ilivyokuwa mwanzo, ‘Jamal’ wangu akanywea, jambo
lililomkasirisha sana Raya, safari hii akawa analia kwa sauti kama mtu
aliyepokea taarifa za msiba.
“Kwa nini unanitesa hivi Jamal? Kwani mimi
nina kasoro gani mpaka unifanyie hivi?” alisema huku akilia, nikaanza upya kazi
ya kumbembeleza huku nikijisikia aibu kubwa ndani ya moyo wangu. Haikuwa kazi
nyepesi kumtuliza Raya mpaka atulie, nikawa najaribu kujikakamua na kumfosi
‘Jamal’ wangu arudi tena mchezoni lakini ilikuwa sawa na kazi bure.
Mpaka kunapambazuka, hakuna kilichofanyika
zaidi ya kubembelezana, saa kumi na moja alfajiri, wote tulipitiwa na usingizi
mzito na tulipokuja kuzinduka, tayari ilikuwa ni saa moja za asubuhi. Mimi
ndiye niliyekuwa wa kwanza kuzinduka, nikajaribu kujikakamua tena kuona kama
angalau naweza kufanya chochote lakini ilikuwa sawa na kazi bure, Jamal wangu
alikuwa amelala doro, jambo lililonifadhaisha sana.
Muda mfupi baadaye Raya naye aliamka, macho
yake yakiwa yamevimba na kuwa mekundu kutokana na kulia sana, akaenda chumbani
kwake na kuniacha nikijiandaa. Baada ya kumaliza kujiandaa, nilitoka hadi
sebuleni ambako nilimkuta Raya akiandaa kifungua kinywa.
Ule uchangamfu aliokuwa nao kwangu uliyeyuka
kama theluji iyeyukavyo juani. Nilitamani sana ajue kwamba sikuwa nimemfanyia
makusudi bali lilikuwa ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wangu lakini
haikuwezekana, alichoamini Raya ni kwamba sikuwa nampenda na nilifanya vile
kumkomoa.
Tulipata kifungua kinywa kimyakimya, kwa kuwa
sikuwa najua kilichotokea nyumbani kwangu usiku ule, sikuwa na muda wa
kuendelea kukaa pale, nilimuaga Raya na kumwambia tutakutana kazini baadaye
lakini cha ajabu, alikataa katakata kuniacha niondoke peke yangu, akaniambia
atanisindikiza na kama ni kuomba ruhusa kazini, niombe ya watu wawili, mimi na
yeye.
Ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwangu kwa
sababu kwa kilichotokea kati yangu na yeye, nilihitaji kupata muda wa kukaa
peke yangu na kutafakari kwa kina kilichosababisha hali ile iliyonitokea usiku.
Lakini kubwa zaidi, sikutaka kumuingiza kwenye
matatizo yangu na Shenaiza, kwa kuwa nilikuwa nimeyaanza mwenyewe, nilitaka
nikayamalize mwenyewe. Hata hivyo, sikutaka pia kuendelea kumuudhi, ikabidi
nimkubalie ambapo tulitoka na safari ya kuelekea nyumbani kwangu ikaanza.
Tukiwa njiani nilimpigia simu bosi kazini na
kumueleza kwamba nilikuwa nimepatwa na matatizo makubwa na kwamba nitachelewa
kufika kazini. Sikutaka kumfafanulia kilichotokea, kwa bahati nzuri alinielewa.
Nilimpigia pia simu Justice na kumtaka asizungumze chochote kazini kuhusu
nilichomwambia jana yake.
“Sasa mbona umeomba ruhusa peke yako? Kwa nini
usiniombee na mimi kama tulivyokubaliana?” Raya aliniuliza kwa sauti ya chini,
iliyoonesha dhahiri kwamba hakuwa na furaha, Nilishindwa cha kumjibu zaidi ya
kumtaka apige mwenyewe simu na kuomba ruhusa kivyake ili tusije kuonekana
kwamba tumepanga kutega kazi kwa makusudi.
Kwa bahati nzuri naye alikubaliwa, tukaendelea
na safari ya kuelekea kwangu kwa kutumia Bajaj ambayo Raya ndiye aliyelipa,
kadiri tulivyokuwa tunazidi kukaribia kwangu ndivyo mapigo ya moyo wangu
yalivyokuwa yanazidi kuongezeka, sikujua nitakutana na nini.
Nilimuelekeza dereva njia ya kupita kwani
sikutaka kutokezea upande wa mbele wa mtaa niliokuwa naishi, nilitaka tutokezee
uchochoroni kwa sababu za kiusalama, kweli dereva yule alinielewa na safari
iliendelea. Hatimaye tukafika kwangu, tukashuka kwenye Bajaj na kumwambia yeye
aondoke zake, tukaanza kupita kwenye uchochoro unaotokezea kwangu.
Tulipokaribia kufika, huku mapigo ya moyo
wangu yakizidi kupiga kiasi cha kunifanya nitokwe na kijasho chembamba japokuwa
bado ilikuwa ni asubuhi na kulikuwa na kibaridi, nilishtuka zaidi baada ya
kuona umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika mbele ya nyumba niliyokuwa
naishi.
“Mungu wangu,” nilisema huku nikifikicha macho
na kutazama vizuri, kuna muda nilikuwa nahisi kwamba huenda nipo ndotoni lakini
haikuwa hivyo, sikuelewa pale kwangu kuna kilichosababisha watu wajae kiasi
kile.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
Nifollow kwenye mitandao ya kijamii kwa:
Facebook: Hash Power
Instagram: Hashpower7113
Twitter: Hash- Power.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment