ILIPOISHIA:
Hakuwa
na nguo yoyote mwilini zaidi ya kipande cha sanda alichokuwa amefunikwa kuanzia
juu kidogo ya mapaja mpaka kifuani ambacho nacho kilikuwa na damudamu. Baba
akanitazama usoni, na mimi nikamtazama nikiwa na shauku kubwa ya kusikia kile
atakachoniambia. Nilikuwa tayari kwa chochote ilimradi Rahma apone.
SASA
ENDELEA...
“Mlichokifanya
mkidhani ni siri yenu ndicho unachotakiwa kukifanya hapa,” alisema baba huku
akigeuka na kuanza kutoka. Ilibidi nimshike mkono na kumvuta, sikuwahi
kumfanyia baba hivyo hata siku moja lakini siku hiyo nilijikuta tu nikifanya
hivyo.
“Baba!”
“Ambacho
huelewi ni nini? Kama unataka apone fanya nilichokwambia na wakati wa tendo
hakikisha hiyo sanda huivui,” alisema baba kisha akatingisha kichwa kuonesha
kwamba niendelee, akanifinjia kijicho na kuachia tabasamu hafifu. Nilijikuta
nikiogopa pengine kuliko kipindi chochote maishani mwangu.
Yaani
mtu anaumwa kiasi kile, yupo kwenye hatua za mwisho za kukata roho, halafu eti
naambiwa nifanye naye mapenzi, tena mwili wake ukiwa umelowa damu na mimi
nikiwa nimevalishwa sanda! Moyo wangu ulipigwa na ganzi.
“Nakupenda
Rahma na sinba cha kufanya zaidi ya kukusaidia, namuomba Mungu anisamehe na
akusamehe pia na wewe,” nilisema huku machozi yakinilengalenga. Hali aliyokuwa
nayo Rahma pale kitandani ilikuwa ya kuhuzunisha mno, nikaamua kupiga moyo
konde na kuivaa roho ya kinyama.
Ilikuwa
ni lazima niivae roho ya kinyama kwa sababu vinginevyo ningemuonea huruma Rahma
kutokana na hali aliyokuwa nayo na pengine huruma yangu ndiyo ingekuwa tiketi
yake ya kuendelea kuzimu.
Niliifunua
ile sanda kwa mbele na kuacha uwazi, nikafumba macho na kuanza kuvuta hisia za
jinsi mimi na Rahma tulivyokuwa tukiogelea kwenye dimbwi la mahaba, kwa mbali
hisia zikaanza kunijia. Sikutaka kufumbua macho kabisa, niliendelea kufumba
macho, nikapapasa na kupanda juu ya kile kitanda, mapigo ya moyo yakinienda
mbio kuliko kawaida.
Nilipiga
magoti na kumuweka rahma katikati yangu, nikakisogeza kile kitambaa cha sanda
pembeni, nikaendelea kuvuta hisia huku machozi mengi yakinitoka na muda mfupi
baadaye, tayari nilikuwa nikiogelea kwenye dimbwi la damu. Niliendelea kujikaza
kisabuni, nikawa napiga mbizi hivyohivyo huku nikiendelea kulia.
Katika
hali ambayo sikuitegemea, nilishtuka baada ya Rahma kuzinduka na kunikamata
mikono yangu kwa nguvu, ikabidi nifumbue macho, nikamuona amefumbua macho yake
huku akijiuma midomo kama aliyekuwa akitaka kuzungumza kitu.
‘Ongeza
spidi, dawa inakaribia kufanya kazi,” nilisikia sauti ya baba, sijjui hata
ilitokea wapi kwani chumba kilikuwa kimefungwa na hata pazia lilikuwa
limefunikwa. Nilijisikia aibu sana lakini sikuwa na cha kufanya, nilizidisha
kasi ya kile nilichokuwa nakifanya, nikashangaa Rahma akiniachia mikono na kunikumbatia
kifuani huku akianza kuangua kilio.
Sikujali
damu zilizokuwa zimeulowanisha karibu mwili wake wote na pale kitandani,
niliendelea kufanya kile nilichoagizwa na ghafla, nilimuona Rahma akianza
kukakamaa mwili wake, nikazidi kuongeza kasi.
“Kuna
kitu kitamtoka mdomoni, hakikisha unakikamata,” alisema baba, nikashtuka maana
kauli yake ilimaanisha hicho kitakachomtoka kitakuwa na uhai, sasa tangu lini
mtu akatoa kiumbe chenye uhai kutoka mdomoni?
Ghafla
rahma alifumbua mdomo huku mwili wake wote ukiwa umekakamaa, nikashtukia kiumbe
cha ajabu kama panya mweusi lakini asiye na manyoya mwilini akichungulia kutoka
mdomoni, nilishtuka mno kiasi cha kunifanya nishindwe kuendelea kufanya kile
nilichokuwa.
Ghafla
kile kiumbe kiliruka kutoka mdomoni na kuangukia juu ya kitanda, nikasikia
sauti ya baba akinisisitiza kwamba lazima nihakikishe nakikamata. Ilikuwa panya
siyo panya, chura siyo chura yaani hata sijui nikielezeeje maana kichwa na
kiwiliwili kilikuwa kama panya lakini hakuwa na manyoya wala mkia na hata
kutembea kwake hakikuwa akikimbia kama panya bali kilikuwa kikiruka kama chura.
Nilijikuta
nikipiga moyo konde, moyo wa kijasiri ukanivaa, nikaruka kutoka pale kitandani
mpaka chini, nikakirukia kile kiumbe na kufanikiwa kukidaka kwenye mikono yangu
lakini cha ajabu, kilipasukia mikononi mwangu, nikashtukia nimeshika mabonge ya
damu.
“Safi
sana!” baba alisema huku akiingia akiwa ameongozana na baba yake Rahma ambaye
naye alianza kunipongeza, wakawa wananipigia makofi. Bado nilijihisi kama nipo
ndotoni, sikuelewa kile kiumbe kimepotelea wapi tena na kuniacha na mabonge ya
damu mikononi, nikawa natetemeka kuliko kawaida.
“Harakaharaka
baba alitoa kitambaa cheupe, akanifuta yale mabonge ya damu na kukiweka kile
kitambaa kwenye mfuko mweusi, akatoa wembe, akanichanja kwenye paji la uso,
eneo nywele zinapoanzia na kutoa dawa kwenye kichupa, akanipaka na kuisugua kwa
nguvu. Dawa ilikuwa ikiuma mno, akarudia kunipongeza kisha akaniambia kazi
imekwisha, nimsaidie rahma kumsafisha na kusaficha chumba chote, wakatoka tena
huku wote wakionesha kuwa na furaha kubwa mioyoni mwao.
“Togo!”
“Naam
Rahma!”
“Nini
kimetokea?” alisema Rahma huku akiinuka kitandani, akawa anashangaa kila kitu.
“Ni
stori ndefu, naomba twende kwanza ukaoge,” nilimwambia, harakaharaka nikamuona
akiinuka na kukimbilia khanga yake, akajifunga huku akionekana kunionea aibu.
Hakuwa Rahma yule ambaye muda mfupi uliopita alikuwa akikaribia kukata roho,
alishabadilika na kuchangamka utafikiri hakuna kilichotokea.
Baada
ya kujifunga khanga, alisogea kwenye dressing table na kujitazama, nikamuona
jinsi alivyoshtuka.
“Mungu
wangu, mbona nimelowa damu hivi? Halafu mbona na wewe umelowa damu? Kwani nini
kimetokea?” alihoji Rahma, ikabidi nivae tabasamu la uongo ili kumuondolea hofu
moyoni. Nakumbuka baba amewahi kunifundisha kwamba njia nzuri ya kuishi na
wanawake, ni pale wanapoonekana kulichukulia tatizo kwa ukubwa, wewe
lirahisishe.
Hatua
hiyo kweli ilifanikiwa sana, kwani licha ya mshtuko aliokuwa nao, aliponiona
mimi nikitabasamu, Rahma aliamini kwamba kilichotokea hakikuwa tatizo kubwa,
nikamshika mkono na kutaka kutoka naye tuelekee bafuni.
“Hiki
nini ulichovaa?” aliniuliza, nikamtazama usoni na kumuomba anipe khanga
nyingine na mimi nijifunge.
“Hujanijibu
lakini.”
“Mbona
una haraka ya kujua mambo yote mara moja? Nimekwambia nitakueleza kila kitu,
kuwa mpole.”
“Halafu
mimi si nilitaka kujiua?” alisema akiwa ni kama ameanza kurudiwa na fahamu
zake, nikachukua khanga mwenyewe na kumshika mkono kumpeleka bafuni maana
niliona akili yake bado ina mawenge.
“Utumie
ile sabuni niliyokuwa kuogea wewe na yeye,” baba alisema, wote tukageuka na
kuwatazama, kumbe walikuwa wakituangalia, wakiwa ni kama hawaamini kama Rahma
yule aliyekuwa akikaribia kunusa umauti, ndiyo yule aliyekuwa akitembea
mwenyewe.
“Nilifungua
mlango wa bafuni, nikamtanguliza Rahma, nikamuona akitaka kujifungia mlango
lakini nilisukuma na kuingia.
“Wanatuona,
unafikiri baba na mama watatuelewaje?”
“Wao
ndiyo wamenipa kazi ya kukusaidia kwa hiyo usiwe na wasiwasi,” nilisema huku
nikifunga mlango kwa ndani, rahma akawa ananitazama kwa macho yenye maswali
mengi bila majibu.
“Unatakiwa
kuoga kwa kutumia hii sabuni,” nilisema huku nikimpa kile kijiwe cha ajabu
nilichopewa an baba, ambacho nilikiacha humohumo bafuni, Rahma akawa bado
anashangaashangaa, ilibidi nimdogeze kwenye bomba, nikafungulia maji, yakaanza
kumwagikia ambapo alionekana kama kuanza kuzinduka.
“Kile
nilichokiona mle bafuni na kuhisi kama naoga damu, ndicho kilichokuwa kinatokea
muda huo kwani maji yaliyokuwa yakichuruzika kutoka kwenye mwili wa Rahma,
yalikuwa damu tupu, nikavuta kumbukumbu na kuhisi labda kile kilichonitokea
kilikuwa na uhusiano na tukio hilo.
Nilijifungua
ile sanda, na mimi nikabaki kama Rahma, nikasogea pale kwenye bomba, maji
yakawa yanatumwagikia, chini damu zikawa zinaendelea kutiririka kuelekea kwenye
bomba la kutolea maji machafu. Nilimshika mikono Rahma, nikamvutia kwenye kifua
changu, tukawa tunatazamana huku maji yakiendelea kutumwagikia, nikajikuta
nikitamani kumbusu mdomoni.
Je,
nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment