ILIPOISHIA:
“Please nakuomba tuonane usiku huuhuu, baba na
mama wamesafiri tangu juzi, niko mwenyewe tu, nahisi haupo sawa na nahitaji
kukusaidia, niambie nikukute wapi, nakuja na bodaboda sasa hivi,” alisema Raya,
nikashusha pumzi ndefu.
SASA ENDELEA…
Nilishindwa nimjibu nini Raya, ni kweli
nilikuwa kwenye matatizo makubwa na nilihitaji mtu wa kunisaidia lakini
nilipomfikiria Raya, nilijikuta nikikosa majibu. Nilikumbuka jinsi msichana
huyo alivyokuwa anajitoa kwa ajili yangu, akihitaji ukaribu wangu tu.
Watu wengi walikuwa wakihisi kwamba huenda
tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini haikuwa hivyo, nilimchukulia kama
rafiki wa kawaida tu ingawa hata yeye alikuwa akiwaambia marafiki zake kwamba
mimi ndiyo mumewe mtarajiwa.
Mara kwa mara alikuwa akinilazimisha sana aje
nyumbani kwangu lakini nikawa nampiga chenga sana na hata akija, nahakikisha
sipo peke yangu, namuita rafiki yangu Justice au Prosper kisha tunajumuika
wote. Japokuwa alikuwa akionesha waziwazi anavyonipenda, nilikuwa namchukulia
kama rafiki tu na sikutaka kabisa uhusiano wetu uvuke zaidi ya hapo.
Hata hivyo, hakuwahi kuchoka, naye akawa
ananialika mara kwa mara niende nyumbani kwao lakini sikuwa tayari kwa hilo.
Nilijiwekea mipaka kati yetu na kamwe sikutaka tuivuke zaidi ya kuwa marafiki
wa kawaida. Japokuwa nilikuwa najua kwamba namkera sana Raya kwa misimamo yangu
lakini sikujali.
“Mbona hunijibu Jamal? Au hutaki nije?” swali
hilo la Raya ndilo lililonizindua kutoka kwenye lindi zito la mawazo.
Nilishasahau kwamba nazungumza na simu, nilizama kwenye mawazo ya kumfikiria
Raya na kushindwa kuamua nini cha kufanya kwa wakati huo.
“Ok… ok… njoo hapa jirani na kituo cha polisi
Mabatini, nakusubiri,” niliamua kukubali kwani sikuwa na ujanja mwingine,
akakata simu. Mitaa yote ilikuwa kimya kabisa usiku ule, kelele pekee
zilizokuwa zinasikika ni za vyura waliokuwa wakikoroma, wenyeji wa Kijitonyama
watakuwa wananielewa vizuri kwani maeneo hayo hasa nyakati za mvua, huwa
kunakuwa na vyura wengi wanaopiga sana kelele nyakati za usiku.
Nilisogea pembeni ya barabara na kusimama,
nikawa namsubiri Raya ambaye hata dakika kumi hazikupita, akawasili akiwa
kwenye bodaboda. Alishtuka sana kwa hali aliyonikuta nayo, mkononi nikiwa bado
nimeshikilia mfuko wa chipsi nilizokuwa nimeenda kununua kwa ajili ya kula na
Shenaiza.
“Jamal! What’s wrong with you?” (Jamal!
Umepatwa na nini) alisema Raya huku akinisogelea, akionesha dhahiri alivyokuwa
na shauku ya kutaka kujua kilichonitokea. Nilimjibu kwa kifupi kwamba ni stori
ndefu na nipo kwenye matatizo makubwa.
“Twende tukaongelee nyumbani, it’s not safe
out here in this dark hours (siyo salama hapa nje muda huu wa giza) alisema
Raya huku akinipokea ule mfuko wa chipsi, akanitaka tupande ‘mshikaki’ kwenye
bodaboda iliyomleta. Huo ulikuwa mtihani mwingine kwangu lakini sikujali sana.
Alitangulia yeye, akakaa kwa mtindo wa
kujibinua, nilijua anafanya vile kwa lengo gani. Na Mimi nikapanda na kukaa
nyuma yake, tukawa tumesogeleana sana kiasi cha miili yetu kugusana.
Hata hivyo, sikupatwa na hisia zozote kwani
akili zangu hazikuwa hapo muda huo, nilikuwa nikiendelea kuwaza kuhusu hatima
ya Shenaiza kule nyumbani kwangu. Dakika chache baadaye, tuliwasili nyumbani
kwa akina Raya.
Kama alivyonieleza kwenye simu, kweli wazazi
wake hawakuwepo, akanikaribisha mpaka sebuleni kwao, akafunga milango na mageti
yote kisha akataka nimueleze kilichotokea. Tayari saa ya ukutani ilikuwa
ikionesha kwamba ni saa saba za usiku.
Ilibidi nimueleze Raya ukweli wa kila kitu.
Kwanza alinishangaa sana na kuniuliza nilipata wapi ujasiri wa kwenda
kumtorosha hospitalini mtu ambaye ndiyo kwanza nimejuana naye siku hiyohiyo.
Akazidi kunishangaa kwamba kwa nini sikumlazimisha msichana huyo anieleze
ukweli wa kilichosababisha akajeruhiwa kiasi hicho na zaidi akaendelea
kunilaumu kwa nini nimempeleka nyumbani kwangu, tena usiku ule.
“Mimi kila siku nikikwambia nije kukutembelea
kwako unakuwa na visingizio lukuki, hata nikija hutaki tukae wawili tu lakini
huyo umeweza kumuingiza kwako, tena usiku, kwa nini Jamal?” Raya alianza kulia
kwa wivu.
“Naomba tuachane na hayo kwanza Raya, hebu
tulimalize hili lililopo mbele yetu,” nilisema kwa upole kwani japokuwa alikuwa
akisumbuliwa na wivu, kuna mambo ya msingi kabisa aliyoyaongea ambayo hata mimi
nilipofikiria vizuri, niligundua kwamba nilikosa umakini katika kulishughulikia
suala hilo.
Tukaanza kujadiliana nini cha kufanya ambapo
aliniambia kwa sababu muda umeshaenda sana na nimeshatoa taarifa polisi, kwa
usalama nilale hapohapo nyumbani kwao mpaka asubuhi ndiyo tutajua nini cha
kufanya.
Sikuwa na cha kufanya, pamoja na ujanja wangu
wote nikawa nimenasa kwenye tundu bovu, Raya akainuka na kuniandalia chakula
kilichokuwa kimesalia, akaniambia zile chipsi nilizoenda kununua nizitupe kwani
zinaweza hata kuwa zimewekwa sumu, nikakubaliana naye.
Ilibidi nijilazimishe tu kula kwani bado
nilikuwa nikisumbuliwa sana na mawazo, nikala huku Raya akijitahidi
kunichangamsha na kuniambia nichukulie kila kitu kilichotokea kuwa ni mipango
ya Mungu.
“Huenda Mungu amesikia kilio changu cha siku
nyingi cha kutaka uje kwetu,” alisema na kucheka mwenyewe, nikatabasamu kiaina
kwani bado moyo wangu ulikuwa na hofu kubwa mno. Baada ya kumaliza kula,
alinipeleka kuoga kisha kinarudi pale sebuleni.
“Si tunalala wote kitanda kimoja?” alisema
Raya, kauli iliyonishtua sana kwa sababu niliona haiwezi kuwa tabia njema kwa
mimi kulala naye kitanda kimoja wakati hakuwa mpenzi wangu, na pia tukiwa
nyumbani kwao. Nikamkatalia katakata!
“Basi usijali, wewe utalala chumbani kwangu
halafu mimi nitaenda kulala chumba cha wageni,” alisema akionesha kupoteza
furaha. Nilimwambia yeye akalale chumbani kwake kama kawaida halafu mimi
nikalale huko kwenye chumba cha wageni, akawa hataki, tukabishana kidogo lakini
baadaye alikubali.
Akanipeleka mpaka kwenye chumba cha wageni
huku mara kwa mara akinishika mwilini, niliamua kujikausha kwani nilijua endapo
nitamchekea tu, usiku huo hautaisha salama, lazima tutaangukia dhambini.
Kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka kwa
pilikapilika za siku nzima, nilipoingia tu chumbani na Raya kutoka, nilivua
nguo na kubaki na bukta tu, nikajilaza kitandani ambapo muda mfupi baadaye,
nilipitiwa na usingizi mzito.
Nilipokuja kuzinduka, nilishtuka mno baada ya
kugundua kuwa sikuwa nimelala peke yangu bali kuna mtu mwingine, tena wa jinsia
ya kike, na kibaya zaidi, hata ile bukta yangu niliyolala nayo, ilishavuliwa.
Nilikurupuka kwa kasi lakini yule mtu aliyelala pembeni yangu akanituliza na
kuniambia nisiogope.
“Mungu wangu,” nilisema baada ya kugundua kuwa
kumbe alikuwa ni Raya, tena naye akiwa mtupu kabisa, akaniambia kwamba alikuwa
anaogopa kulala peke yake na ndiyo maana amekuja kulala na mimi.
Sikupata hata muda wa kujibu chochote, Raya
akanikumbatia kwa nguvu mwilini na kuanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili
wangu, japokuwa sikuwa tayari kwa alichokuwa anakitaka, nilijikuta kwenye
wakati mgumu mno, kwani ukichanganya joto la mwili wake na uzuri aliokuwa nao,
ukizingatia kwamba tulikuwa wawili tu, nilijikuta nikishindwa cha kuamua,
‘Jamal’ wangu naye akaanza usumbufu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment