ILIPOISHIA:
Nilijifungua
ile sanda, na mimi nikabaki kama Rahma, nikasogea pale kwenye bomba, maji
yakawa yanatumwagikia, chini damu zikawa zinaendelea kutiririka kuelekea kwenye
bomba la kutolea maji machafu. Nilimshika mikono Rahma, nikamvutia kwenye kifua
changu, tukawa tunatazamana huku maji yakiendelea kutumwagikia, nikajikuta
nikitamani kumbusu mdomoni.
SASA
ENDELEA...
“Mbona
najisikia hivi?”
“Unajisikiaje?”
“Hata
sijui nisemeje lakini najisikia raha ya ajabu ndani ya moyo wangu,” alisema
Rahma na kabla hata sijafanya kile nilichokuwa nakitamani, yeye alinianza
akanibusu kwa midomo yake milaini huku akinikumbatia kwa nguvu, na mimi
nikamuonesha ushirikiano.
“Kwa
nini ulitaka kujiua?” nilimuuliza, akafumbua macho yake ambayo kwa muda wote
alikuwa ameyafumba, akanitazama usoni bila kusema chochote, akajiinamia.
Niligundua kwamba hakulipenda swali hilo, nikaamua kubadilisha mada lakini bado
hakuzungumza chochote.
Nilimsaidia
kumsafisha mwili wake wote mpaka damu zote zikaisha kwenye miili yetu,
nikafunga maji na kumpa khanga yake lakini aliikataa kwa sababu nayo ilikuwa na
damu.
“Vaa
tu kwanza tutaoga tena kwa mara nyingine, inabidi tukafanye usafi chumbani kwako,”
nilimwambia, akakubali. Tulichukua ndoo za maji na vifaa vya kufanyia usafi,
tukaelekea chumbani kwake ambako kila sehemu ilikuwa imechafuka kwa damu.
Tukaanza
kufanya usafi lakini bado Rahma hakuzungumza chochote, muda wote alikuwa kimya
kabisa na pale alipohitaji kunielekeza jambo, alikuwa akitumia zaidi ishara.
“Mbona
umebadilika ghafla? Nisamehe kama kuna kitu nimekukwaza,” nilimwambia,
akanitazama tena.
“Kwani
nini kilitokea?”
“Wewe
unakumbuka nini?”
“Nakumbuka
niliamua kunywa sumu ili nife.”
“Kwa
nini?”
“Kwa
sababu nakupenda.”
“Kwa
sababu walituambia kwamba sisi ni ndugu,” alisema Rahma huku akiacha kila
alichokuwa anakifanya, machozi yakaanza kumtoka.
“Kumbe
walisema vile kututishia kwamba tusije tukaanza kufanya mapenzi lakini siyo
kweli, hatuna undugu ila baba yangu na baba yako ni marafiki tangu wakiwa
vijana wadogo kwa hiyo ni kama ndugu tu,” nilimwambia.
Hata
mimi maneno hayo niliwasikia mama na mama yake Rahma wakiongea kule
hospitalini, wakilaumiana kwa maneno waliyotuambia ambayo ndiyo yaliyosababisha
Rahma achukue uamuzi wa kuyakatiza maisha yake.
Nilipomueleza
maneno hayo, alinitolea macho akiwa ni kama haamini, akanisogelea na kunishika
mkono, akawa ananitingisha kwa nguvu akitaka nimhakikishie kwamba ni kweli.
Nikarudia tena kumueleza vilevile, jambo lililosababisha anikumbatie na kuanza
upya kulia.
“Nisamehe!
Niliona bora nife tu kuliko kuishi bila wewe, nimejikuta nikikupenda mno
mwenzako, utafikiri tulijuana miaka mingi nyuma,” alisema huku akiendelea
kulia.
“Na
hizi damu imekuwaje?” aliniuliza, kama nilivyokuwa nikimjibu mwanzo,
nikamwambia asiwe na haraka atajua kila kitu kilichotokea. Alinibusu tena,
tukaendelea kufanya usafi. Ilibidi nguo zote zilizokuwa zimechafuka kwa damu,
tuzikusanye kwa ajili ya kwenda kuzifua, tulitoa kuanzia mashuka mpaka foronya.
Tukasaidiana
kupiga deki kwa kutumia sabuni maalum, chumba chote kikawa kisafi kabisa. Baada
ya kumaliza, tulibeba furushi la nguo chafu kwa ajili ya kwenda kuzifua kule
bafuni lakini wakati tukitoka, baba alikuja kutuambia kwamba nguo hizo
hazikutakiwa kwenda kufuliwa bali inabidi zikachomwe moto.
Itabidi
mvue hata hizo mlizovaa, zote hizi ni za kuchoma moto, tena inabidi nyie
wenyewe kwa mikono yenu. Tulifanya kama baba alivyotuelekeza na muda mfupi
baadaye, tulikuwa tumemaliza kila kitu, ikabidi tukaoge tena na safari hii,
kila mtu alienda kuoga peke yake. Rahma alinipa fulana yake moja niivae kwani
sikuwa na nguo zozote za maana nilizobeba kutoka kule kijijini.
“Baba
yako amenipa hii pesa anasema muende sehemu yoyote nzuri mkatembee na Togo,
hata kama ni ‘beach’ ila msichelewe kurudi,” alisema mama yake Rahma huku
akitoa noti mbili nyekundu na kumpa Rahma.
“Lakini
mama, naomba unisamehe!”
“Usijali,
tumeshakusamehe Rahma, tunamshukuru Mungu kwa kukuokoa kutoka kwenye bonde la mauti.
Jioni mtapenda kula nini?” alisema mama yake Rahma kwa upole wa ajabu.
Hata
mimi nilishangaa sana, nilitegemea kwamba baada ya kila kitu kutulia, lazima
mimi na Rahma tulikuwa na kesi ya kujibu lakini mambo yakawa tofauti kabisa.
“Nataka
tule pilau, si ndiyo Togo,” alijibu Rahma, na mimi nikatingisha tu kichwa. Kule
kijijini kwetu, pilau lilikuwa likipikwa sikukuu tu, tena Krismasi, nikajikuta
nikijilamba midomo yangu kwa uchu. Baada ya hapo, mama yake Rahma alitoka na
kututakia matembezi mema.
“Twende
wapi kutembea,” alisema Rahma huku akinikumbatia na kunibusu, nikamwambia mimi
sijui sehemu yoyote kwa hiyo yeye ndiyo aniongoze, akacheka sana na kunipiga
mgongoni. Yaani kama kuna mtu alimuona Rahma saa chache zilizopitahali
aliyokuwa nayo, asingeamini kwamba ndiye yeye.
Harakaharaka
alianza kujiandaa, akaenda tena kuoga na kurudi chumbani kwake, mimi nikawa
nimekaa kwenye kiti cha pembeni. Niweke wazi kwamba safari hii sikuwa naogopa
chochote ikwa sababu baba na baba yake Rahma ndiyo walioniruhusu kuwa karibu na
Rahma wakihofia kwamba kama wataendelea ukali juu yetu, anaweza kujidhuru tena.
Na
waliniambia natakiwa nisimuache peke yake kule chumbani kwake kwa hiyo
nilikuwepo pale kihalali kabisa ingawa waliniambia kwamba sitakiwi kufanya
chochote naye kwa sababu kulikuwa na mambo yasiyo ya kawaida wameyabaini na
chanzo cha yote ilikuwa ni mimi kufanya naye mapenzi.
“Hebu
niambie Togo, unanipenda kweli kama mimi ninavyokupenda?”
“Nakupenda
tena sana,” nilimwambia, nikamuona akiachia tabasamu pana, akanisogelea pale
nilipokuwa nimekaa, akanishika mkono na kunivuta ili nisimame, nikatii,
alinivutia kifuani kwake na kunibusu kimahaba, na mimi nikafanya kama yeye.
“Kama
kweli unanipenda nataka unioe,” alisema Rahma kwa sauti ya kunong’ona,
akanibusu tena.
“Usijali
kabisa, kwako nipo tayari kwa chochote,” nilimwambia. Kiukweli nilimjibu tu kwa
lengo la kumfurahisha maana niliambiwa sitakiwi kumuudhi kwa chochote. Baada ya
hapo, aliniachia na kwenda kufungua kabati, akaniambia nimsaidie kuchagua nguo
ya kuvaa.
Kwangu
ulikuwa mtihani mkubwa sana kwani wakati mwingine alikuwa akiiachia ile khanga
aliyotoka nayo bafuni na kuufanya mwili wake wenye mvuto wa kipekee ubaki wazi,
nikawa na kazi ya ziada. Baadaye aliipata nguo aliyoitaka mwenyewe, akavaa
gauni zuri lililompendeza na kujitanda ushungi.
Kwenye
suala la mavazi, Rahma alikuwa akijitahidi sana, alikuwa akivaa mavazi ya
heshima tofauti na wasichana wengi wa mjini. Mimi sikuwa na cha kubadilisha,
vilevile nilivyokuwa nimevaa, tulitoka, nikataka kuvaa mabuti yangu lakini
akaniambia kuna raba nzuri huwa anafanyia mazoezi, akaingia tena ndani na
kutoka nazo.
Zilinipendeza
vizuri, nikawa nachekacheka tu, tulienda sebuleni na kuaga, ndugu zangu
waliokuwa wamenogewa na tivii, walinitazama kwa macho ya wivu, tukatoka mpaka
nje ambapo Rahma alipunga mkono upande kulipokuwa kumepaki Bajaj, ikaja moja,
tukaingia na kukaa.
“Tupeleke
Coco Beach, kule wanakouza mihogo,” alisema Rahma, safari ikaanza lakini mita
chache mbele, nilishtuka baada ya kusikia mtu akiliita jina langu kwa nguvu,
tena sauti yenyewe ilikuwa ya kike, ilibidi Rahma amwambie dereva asimame,
tukageuka nyuma kutazama ni nani aliyekuwa ananiita kwa sababu mimi nilikuwa
mgeni na hakuna mtu yeyote aliyekuwa akilifahamu jina langu zaidi ya wale
tuliokuwa tukiishi pamoja.
Je,
nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment