ILIPOISHIA:
“Tupeleke
Coco Beach, kule wanakouza mihogo,” alisema Rahma, safari ikaanza lakini mita
chache mbele, nilishtuka baada ya kusikia mtu akiliita jina langu kwa nguvu,
tena sauti yenyewe ilikuwa ya kike, ilibidi Rahma amwambie dereva asimame,
tukageuka nyuma kutazama ni nani aliyekuwa ananiita kwa sababu mimi nilikuwa
mgeni na hakuna mtu yeyote aliyekuwa akilifahamu jina langu zaidi ya wale
tuliokuwa tukiishi pamoja.
SASA
ENDELEA...
Mimi
ndiyo nilikuwa wa kwanza kushuka kwenye Bajaj, Rahma naye akafuatia, nikawa na
shauku kubwa ya kumjua aliyeniita kwa bashasha kiasi kile.
“Togo,
ni wewe! Ooh siamini macho yangu, sikujua kama nitakupata!” alikuwa ni yule
msichana ambaye tulikaa naye siti moja kwenye basi wakati tukisafiri kutoka
Mbeya kuja Dar es Salaam. Alikuwa amevaa sketi fupi na nyepesi ambayo ilimfanya
maungo yake yajichore vizuri.
Juu
alikuwa amevaa blauzi ndogo ambayo iliacha sehemu kubwa ya kifua chake wazi,
akawa anatembea kwa maringo akinifuata huku tabasamu pana likiwa limechanua
kwenye uso wake. Kiukweli na mimi nilishindwa kujizuia kutabasamu, hasa
nilipokumbuka wakati mzuri tuliokuwa nao kwenye basi mpaka tulipoachana Ubungo.
“Jamani
mbona ile simu niliyokupa hupatikani hewani? Nimehangaika sana kwa kweli,”
alisema akiwa tayari ameshanifikia, kufumba na kufumbua nikashtukia
amenikumbatia kimahaba na kunibusu mdomoni.
“Dada
mambo!” alimsalimia Rahma ambaye alikuwa amesimama pembeni yake, akiwa ni kama
haamini kile alichokuwa anakiona. Ilibidi nianze kuvungavunga pale maana kila
kitu kilikuwa kikitokea kwa kasi kubwa mno.
“Umepajuaje
hapa?”
“Ilibidi
nimtafute dereva teksi aliyewabeba wakati mnatoka pale Ubungo, kwa bahati nzuri
akawa anakumbuka sehemu alipowaleta, ndiyo amenileta, yule pale kwenye gari,”
alisema huku akigeuka nyuma na kuonesha upande teksi alityokuja nayo ilipokuwa
imepaki.
“Mnaenda
wapi kwani?”
“Tunaenda
bichi,” nilimjibu harakaharaka huku nikigeuka na kumtazama Rahma usoni ambaye
bado alionesha kutoelewa kinachoendelea.
“Kwa
nini tusipande kwenye ile teksi, mi nimeshalipa.”
“Hapana,
ahsante,” Rahma alidakia na kunishika mkono, naona uzalendo ulishafika kikomo,
akatangulia kuingia kwenye Bajaj na kunivuta mkono na mimi niingie.
‘Kwani
mnaenda bichi gani?” aliuliza huku akionesha bado kuwa na shauku kubwa ya
kuzungumza na mimi.
Sikuwa
nakujua Coco lakini kwa sababu nilimsikia Rahma akimueleza dereva wa Bajaj kuwa
atupeleke wanakouza mihogo, na mimi nilijikuta nikijibu hivyohivyo.
“Coco
wanakouza mihogo,” baada ya kumjibu hivyo, nilimuona haraka akigeuka na kurudi
kwenye teksi aliyokuja nayo. Watu kadhaa waliokuwa eneo lile, waliacha kila
walichokuwa wanakifanya na kugbaki wakishangaa muvi iliyokuwa inaendelea.
“Togo,
yule ni nani?”
“Mh!
Jina lake simjui lakini tulikaa naye siti moja kwenye basi wakati tunakuja.”
“Muongo!
Yaani mtu uliyekaa naye siti moja tu ndiyo akuzoee kiasi hiki? Angalia
amekupaka lipstiki yake mdomoni,” alisema Rahma huku akionesha kuanza
kulengwalengwa na machozi.
“Kweli
tena, hata ukimuuliza atakwambia hivyohivyo, hata hatujuani vizuri,” nilisema
huku nikijifuta mdomoni, kweli kulikuwa na mabaki ya lipstiki aliyoniachia
aliponibusu mdomoni.
“Yeye
amenizoea tu lakini hakuna chochote kati yetu.”
‘Mbona
nimemsikia akisema alikupa simu? Yaani inawezekanaje mtu akupe simu tu? Halafu
umeona alivyovaa, kwa nje tu anaonekana changudoa, ka hiyo kumbe wewe unatembea
na machangudoa? Si nakuuliza?” Rahma alizidi kunibana kwa maswali mengi.
Sikuwahi kumsikia Rahma anavyozungumza akikasirika lakini siku hiyo alikasirika
kwelikweli, akawa anaendelea kufoka na muda mfupi baadaye alianza kulia.
Ilibidi
nianze kazi ya kumbembeleza, nikamkumbatia kifuani kwangu na kumbusu sehemu
mbalimbali za mwili wake, kidogo nikamuona akianza kutulia, na yeye
akanikumbatia kwa nguvu kifuani huku Bajaj ikizidi kukata mitaa.
“Halafu
umemuelekeza mpaka sehemu tunapoenda, hujui anaweza kukufuata? Dereva
nimebadilisha mawazo, hebu tupeleke Msasani Beach na siyo Coco tena,
nitakuongeza hela,” alisema Rahma, dereva akatingisha kichwa kuonesha kwamba
amemueleza.
“Unajua
mimi nakupenda, kwa nini unanifanyia makusudi lakini?”
“Nisamehe
Rahma, hayakuwa makusudio yangu, nimejikuta tu mambo ya ajabu yametokea,
nisamehe,” niliendelea kumbembeleza na kumbusu, cha ajabu alitulia kabisa na
hakusema neno lingine lolote mpaka tulipofika Msasani Beach. Sikuwa naijua
mitaa lakini kiukweli nilifurahia sana mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.
Alimlipa
dereva kisha tukashuka, tukawa tunatembea kuelekea baharini huku nikiwa na
shauku kubwa ya kuiona bahari maana nilikua nikisikia tu. Nilitaka pia nikaonje
maji yake nihakikishe kama kweli yana chumvi kama ambavyo watu huwa wanasema.
Tulipita
sehemu ambapo kuna viti vya kupumzikia, tukawaona watu mbalimbali wakiwa
wanapunga upepo, wengine wakila na kunywa. Tulipitiliza mpaka baharini kama
nilivyomuomba Rahma na kitu cha kwanza nilichokifanya, ilikuwa ni kunawa usoni
na kichwani kwa kutumia maji ya baharini.
Niliwahi
kusikia pia kwamba maji ya baharini huondoa mikosi, nikanawa kwa maji mengi na
hapo ndipo nilipogundua kuwa ni kweli maji hayo yalikuwa na chumvi, tena nyingi
kiasi kwamba huwezi hata kuyanywa. Kiukweli nilifurahi sana kuiona bahari na
kuyagusa maji ya bahari, nikawa najisikia kama nimetua kwenye ulimwengu
mwingine tofauti.
Rahma
muda wote alikuwa akicheka kwa furaha, hasa kwa jinsi nilivyokuwa ‘najitoa
ufahamu’ na bahari. Nilifurahi kumuona akicheka mpaka kukaukia, akiwa amekaa
kwenye mchanga, jirani na pale nilipokuwa.
Baada
ya kucheza sana kwenye maji, nilirudi pale alipokuwa amekaa Rahma, nikakaa
pembeni yake na kumuegamia, akanibusu kwenye paji la uso na kuniambia kuwa
nimemfurahisha sana. Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale lakini mra kwa
mara Rahma alikuwa akipenda zaidi tuzungumze mambo ya kikubwa.
Alikuwa
anataka kusikia nina mal;engo gani naye siku za usoni, alitaka kujua napenda
kuwa na familia ya watoto wangapi au nitakuwa baba wa aina gani kwa wanangu.
Aliniuliza pia kama nina mpango wa kujiendelea kwenye fani yoyote ili mwisho na
mimi nije kuwa na uwezo wa kutunza familia.
Kwangu
mazungumzo hayo si tu kwamba yalikuwa mageni kwangu, lakini pia mambo mengi
sikuwahi kuyawaza. Nadhani hili ndiyo tatizo linalowakumba watu wengi
wanaopishana umri wa wenzi wao, hasa kama mwanamke akiwa mkubwa. Kwangu Rahma
alikuwa mkubwa, kama nilivyowahi kusema siku za nyuma, alikuwa akilingana na
dada yetu mkubwa, Sabina.
Hata
mazungumzo yake, alikuwa ni mdada anayejiheshimu, mwenye busara na anayewaza
mbali, alionesha kweli kwamba ameanza kukomaa kiakili. Hali ilikuwa tofauti
kwangu kwa sababu hata mwanamke mwenyewe, yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza
kwangu, kwa maana sikuwahi kuwa na mpenzi wala kushiriki sanaa za kikubwa kabla
ya kukutana naye.
Sikuwa
nikiwaza chochote kuhusu familia, au mke au maisha ya ndoa, nadhani ni kwa
sababu ya umri. Hata hivyo, kwa sababu Mungu alinipa uwezo wa kumsoma mtu
haraka, sikutaka kumkasirisha mawazo Rahma, kwa hiyo ikabidi na mimi nianze
kuzungumza kama mtu mzima flani hivi, tukawa tunaenda sawa.
“Mh,
hebu naomba simu yangu mara moja, sijaigusa tangu tumefika,” alisema rahma,
nikamsogezea pochi yake ndogo ambapo alifungua na kutoa simu.
“Mh!
Baba amepiga sana, sijui alikuwa anasemaje,” alisema Rahma huku akiendelea
kubonyezabonyeza simu yake, mara akanigeukia na kunitazama usoni.
“Kulikuwa
na ujumbe wako hapa lakini tumechelewa sana, hata sijui itakuwaje,” alisema,
hali iliyonifanya na mimi nishtuke kwa sababu ya jinsi yeye mwenyewe
alivyoonekana kushtuka.
“Kuna
nini kwani?” nilimuuliza, akaniambia baba alikuwa amempigia simu kwa lengo la
kutaka kuzungumza na mimi na kubwa alilokuwa anataka kuniambia ni kwamba
wamesahau kuniambia kwamba nikienda ufukweni nisiguse kabisa maji ya bahari.
Nilishangazwa sana na maelezo hayo, nikajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.
Tayari
nilishayagusa na siyo kuyagusa tu bali niliyachezea vya kutosha na kama Rahma
asingenizuia au kama siyo woga wa bahari, nilitaka hata niogelee. Tukiwa bado
tunashauriana cha kufanya, mara simu ya Rahma ilianza tena kuita, harakaharaka
akaipokea.
“Samahani
simu ilikuwa kwenye mkoba baba,” nilimsikia Rahma akijitetea, bila shaka
aliulizwa kwa nini hakupokea simu.
“Eeeh
niko naye,” alijibu tena, nikajua lazima ameulizwa kama yupo na mimi, nikamuona
akinipa simu, akaniambia baba anataka kuzungumza na mimi.
“Haloo
Togo.”
“Haloo
baba.”
“Hebu
ongea na mzee,” alisema baba yake Rahma akimaanisha nizungumze na baba, akampa
simu. Alimpa simu baba na swali lake la kwanza lilikuwa ni kama nimeshayagusa
maji ya bahari. Ilibidi nimjibu kwamba nimeshayagusa kwani sikuwa najua
chochote.
“Mungu
wangu, kuna mtu anaenda kufa,” alisema baba kisha akakata simu, nikashtushwa
mno na kauli yake hiyo. Sikuelewa nini kimetokea au kosa langu lilikuwa ni
nini.
“Mbona
watu wanachezea maji, wengine wanaogelea bila tatizo, mimi kosa langu nini,”
nilijikuta nikijisemea, Rahma akanishika na kunituliza pale chini kwani
nilishaanza kuchanganyikiwa kutokana na kile alichokisema baba.
“Amesemaje
kwani?” aliniuliza Rahma, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni, sikutaka
kumwambia ukweli wa nilichoambiwa na baba, nikamdanganya kwamba baba amenifokea
sana kwa sababu nimegusa maji hayo. Aliupokea uongo wangu, akanikumbatia na
kunipa pole, nikatulia kifuani kwake.
Ghafla
tulishtushwa na kishindo kikubwa ambacho hata sikuelewa kimetokea wapi.
Je,
nini kimetokea? Ni kishindo cha nini? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment