ILIPOISHIA:
“MUNGU wangu,” nilijisemea, mapigo ya moyo yakiwa
yananienda mbio kuliko kawaida, nikiwa sijui nini kitatokea, hasa ukizingatia
kwamba nilikuwa ugenini na ndiyo kwanza tulikuwa tumewasili.
SASA ENDELEA…
ALINIACHIA huku naye akionyesha kushtuka,
akashuka kitandani na kuokota khanga yake, akajifunga kivivu na kunionyesha
ishara kwamba niingie kwenye kabati la nguo, nilifanya hivyo haraka, nikamsikia
akifungua mlango.
“Baba amesema usije ukafunga mlango mkubwa wa nje,
watachelewa kuingia ndani kwani kuna kazi wanaifanya.”
“Haya poa,” nilimsikia akizungumza na mdogo wake,
akashusha pumzi ndefu na kuufunga mlango, nikamsikia safari hii akifunga kwa
funguo kabisa, akaja pale kabatini na kufungua mlango, akanionyesha ishara
kwamba nitoke.
Sikulaza damu, nilitoka harakaharaka nikiwa kama
nilivyo, na yeye akauachia ule upande wa khanga, ukadondoka chini, tukawa
tunatazama kama majogoo yanayotaka kupigana. Alipiga hatua moja mbele, miili
yetu ikagusana, akazungusha mikono yake kwenye shingo yangu, na mimi nikiwa
sijiaminiamini, nikaukumbatia ‘mlima’ wake.
Nikiri kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya
kwanza kuwa kwenye hali kama hiyo na nilichokihisi kwenye mwili wangu, sikuwahi
kukihisi kabisa tangu napata akili zangu. Ni hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwa
nini watu wengi huwa wanayasifia sana mapenzi kwamba ni matamu kuliko asali.
Ni hapo pia ndipo nilipoelewa kwa nini watu
wengine hufikia hatua hata ya kutoana roho, baada ya mmoja kugundua kwamba
anatembea na mkewe au mpenzi wake. Dakika chache baadaye, nilikuwa nahema kama
nataka kukata roho, ufundi wa mikono yake kuvinjari kwenye mwili wangu,
ulinifanya mara kwa mara niwe natoa miguno ambayo sikuwahi kuitoa kabla.
Hata sikukumbuka nilifikaje kwenye uwanja wake wa
fundi seremala, nilikuja tu kushtukia yeye yuko juu yangu nikiwa nimelala chali,
huku nikiendelea kupumua kwa fujo, mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio sana na
‘Togolai’ akiwa anazidi kuongeza hasira kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Kwa ufundi wa hali ya juu, alimuelekeza njia ya
kupita, nikajikuta nikianza kuzungumza kama bubu, maneno hayatoki wala
hayaeleweki, kucheka natamani lakini muda huohuo natamani kupiga chafya,
ilikuwa ni hali ya ajabu mno. Safari iliendelea, mwanzo alikuwa akipiga hatua
fupifupi lakini baadaye nikaanza kumuona akinogewa na kuongeza huku akitoa
ukelele fulani ulioongeza raha kubwa kwenye masikio yangu.
Baadaye ilibidi tubadilishane magoli kwenye mechi
ile ya kirafiki isiyo na refa wala jezi, yeye akawa anapeleka mashambulizi Kaskazini
mwa uwanja na mimi napeleka Kusini.
Japokuwa hata danadana sikuwa najua kupiga na
siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza, nilijitahidi kuonyesha kiwango kwa sababu
nimewahi kusikia kwamba ukicheza chini ya kiwango, huwa unadharaulika mbele ya
viumbe hawa.
Akaongeza mno kasi ya mashambulizi kisha
akanikaba kwa nguvu shingoni kama wanavyofanya wale watu wanaopora simu au
fedha, akanishikilia kwa nguvu na kunibana, na mimi nikaongeza kasi,
nikajisikia hali fulani hivi nzuri sana, akazidi kunibana kisha akaniachia na
kudondokea upande wa pili, jasho likiwa limemlowanisha chapachapa na mimi
nikiwa hoi bin taaban, nilijikuta nikicheka mwenyewe kwa furaha.
Hakuzungumza jambo lolote kwa dakika kadhaa,
baadaye aliinuka na kukaa kitandani, akawa ananitazama kama ambaye haamini kitu
fulani.
“Una miaka mingapi?”
“Kwa nini unaniuliza hivyo?”
“Kwa nje unaonekana mdogo lakini wewe ni zaidi ya
mwanaume,” alisema na kunikumbatia tena, akaanza kunibusu sehemu mbalimbali za
mwili wangu huku akiniambia kwamba ananipenda na anaomba nisimuache ila
uhusiano wetu uwe wa siri.
Bado sikuwa naelewa alichokimaanisha, akaendelea
na uchokozi wake na hata sijui nini kilitokea lakini muda mfupi baadaye, nilishtukia
tukiwa tena dimbani, safari hii kidogo nikawa sina ugeni na uwanja pamoja na
mchezo wenyewe.
Mpambano mkali uliendelea mpaka baadaye ambapo
ile hali iliyotutokea mwanzo ilitokea tena, tena kwa kila mtu. Safari hii,
alipoangukia upande wa pili, haukupita muda mrefu akaanza kukoroma.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana, harakaharaka
niliinuka na kuvaa nguo zangu nikaenda kufungua mlango na kutoka huku nikinyata,
nikaenda mpaka kwenye mlango wa kile chumba ambacho nitalala na ndugu yangu
mmoja.
Kwa bahati nzuri, mlango haukuwa umefungwa,
nikaingia mpaka ndani, tayari ndugu yangu naye alikuwa akikoroma, nikajilaza
kitandani huku nikisikia uchovu wa kiwango cha juu, karibu kila sehemu kwenye
mwili wangu ilikuwa inauma.
Tabasamu pana lilikuwa limechanua kwenye uso
wangu, hasa kumbukumbu ya nilichotoka kukifanya ilipokuwa inanijia. Sasa na
mimi nilijihisi kuwa mwanaume niliyekamilika. Bado nilikuwa siamini jinsi
nilivyoweza kuuangusha mbuyu kwa shoka moja, haukupita muda mrefu nilipitiwa na
usingizi.
“Motooo! Jamani moto… nakufaaaa,” sauti za mtu
aliyekuwa akipiga kelele kuomba msaada, ndizo zilizonishtua kutoka kwenye usingizi
mzito, nikakurupuka huku mapigo yangu ya moyo yakinienda mbio kuliko kawaida,
nikatoka mpaka koridoni.
Sikuamini macho yangu kusikia sauti ile ilikuwa
ikitoka kwenye kile chumba ambacho usiku huo mimi na yule dada tulilambishana
asali. Moto ulikuwa umekolea kiasi kwamba hata sehemu ya kupita haikuwa
ikionekana.
Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kufika eneo hilo
kwa sababu sikumkuta mtu mwingine yeyote, nikaona nikisema niende kuwaamsha
baba na mama, dada wa watu anaweza kufa bure, nikapiga moyo konde na kuukanyaga
mlango ambao ulikuwa ukiwaka moto, ukaangukia ndani.
Sikujali kuhusu moshi mzito uliokuwa umetanda
kwani tayari nilikuwa na uzoefu wa kucheza kwenye moshi kwani kule kijijini
ilikuwa kama tunataka kwenda kupakua asali kwenye mzinga, lazima tuwashe moto
kwa kutumia miti inayotoa moshi mzito. Nilibana pumzi, nikaenda mpaka pale
kitandani ambapo nilimkuta akiwa ameanza kuishiwa pumzi kutokana na kuvuta
moshi mwingi.
Kwa kuwa mwili wangu ulikuwa na nguvu, si unajua
tena maisha ya kijijini yanakufanya uwe ‘ngangari’ kutokana na kazi ngumu,
nilimbeba na kutoka naye mpaka koridoni, moto ukawa unazidi kuwaka lakini
kilichonishangaza sana ni kwamba haukuwa ukisambaa kwenye vyumba vingine.
Nikiwa koridoni, mikononi nikiwa nimembeba yule
dada ambaye alishapoteza fahamu, nilikutana na baba na mwenyeji wake pamoja na
mama na mwenyeji wake.
“Kuna nini tena? Rahma kapatwa na nini?” aliuliza
baba yake, ni hapo ndipo nilipojua kwamba kumbe jina lake anaitwa Rahma.
Sikuweza kuwajibu kwa sababu walikuwa wanamuona hali aliyokuwa nayo, baba yake
na baba wakanipokea na kumkimbiza mpaka sebuleni, feni zote zikawashwa.
“Kumetokea nini?”
“Moto.”
“Motoo?”
“Ndiyo, chumbani kwake kunawaka moto,” nilisema
huku nikishangaa kwa nini walikuwa wakiniuliza mara mbilimbili jambo ambalo
lilikuwa wazi. Harakaharaka walielekea kule chumbani wakati mama yake akihangaika
kumpa huduma ya kwanza lakini muda mfupi baadaye, walirudi mbiombio.
“Umesema chumbani kwake kunawaka moto?”
“Ndiyo, alikuwa anapiga kelele za kuomba msaada
ndiyo nikaamka na kwenda kumsaidia, nilisema, nikaona baba na mwenyeji wake
wakitazamana, sikuelewa walikuwa wanamaanisha nini. Ilibidi haraka nirudi kule
chumbani kwake ili kuangalia moto umefikia wapi.
Cha ajabu, mpaka nafika mlangoni hakukuwa na moto
wala dalili za moto isipokuwa mlango ulikuwa umevunjwa na nakumbuka vizuri mimi
ndiye niliyeukanyaga kwa nguvu ukavunjika.
Huku nikiwa nimepigwa na butwaa, niliingia ndani
ambako muda mfupi uliopita moto mkubwa ulikuwa umetanda kila sehemu lakini cha
ajabu kila kitu kilikuwa sehemu yake, nikageuka huku nikiwa siamini, nikakutana
na baba na mwenyeji wake ambao kumbe walikuwa nyuma yangu wakinitazama.
“Ulimaanisha chumba hiki au kingine?”
“Hikihiki, nashangaa sijui imekuwaje, kwani nyie
hamjasikia kelele za kuomba msaada?”
“Mimi nimesikia kelele za mlango kuvunjwa tu,
basi.”
“Mungu wangu,” nilisema kwa hofu kubwa,
nikijihisi kama nipo kwenye ndoto ya kutisha.
“Na vipi kuhusu hii?” baba aliniuliza, huku
akinionyeshea nguo yangu ya ndani iliyokuwa pale chini ya kitanda cha Rahma.
Kumbe wakati muda ule navaa nguo zangu, niliisahau si unajua tena maisha ya
kijijini kuvaa hiyo kitu hasa kwa sisi wanaume siyo kitu cha lazima sana? Aibu
ya mwaka ilikuwa imenifika.
“Eti kumetokea nini kwani?” sauti ya mama yake
Rahma ilisikika, akiwa ameongozana na binti yake ambaye sasa fahamu zilikuwa
zimemrudia, wakiwa pamoja na mama. Nilishindwa hata cha kujibu, mate
yakanikauka ghafla mdomoni.
Je, nini kitafuatia? Usikose Jumatatu kwenye
Gazeti la Championi Jumatatu.
No comments:
Post a Comment