ILIPOISHIA:
“ETI kumetokea nini kwani?” sauti ya mama yake
Rahma ilisikika, akiwa ameongozana na binti yake ambaye sasa fahamu zilikuwa
zimemrudia, wakiwa pamoja na mama. Nilishindwa hata cha kujibu, mate
yakanikauka ghafla mdomoni.
SASA ENDELEA…
“ETI Rahma, nini kimetokea?” “Nilikuwa
nimelala, ghafla nikaanza kuhisi kama naungua hivi, sijui tena kilichotokea
mpaka nilipokuja kuzinduka kule sebuleni,” alisema na kunifanya nimtazame kwa
macho ya mshangao.
Ni yeye pekee ndiye ageweza kuthibitisha
kilichotokea lakini kwa maelezo yale, japo alizungumzia kidogo kuhusu kuhisi
anaungua, bado yasingetosha kumfanya mtu aamini nilichokuwa nakizungumza. “Na
hii nguo imefikaje huku?”
“Niliposhtuka usingizini, sikuwa nimevaa nguo
kwa hiyo katika zile purukushani za kuwahi kuja kumuokoa dada nikasahau kuivaa
na nadhani ilikuwa kwenye nguo zangu ndiyo maana ikaja kuangukia humu ndani,”
nilisema.
Sijui
nilipata wapi akili za kutunga uongo mkubwa kiasi hicho. Baba alinitazama
usoni, nikakwepesha macho yangu kwa sababu baba alikuwa na uwezo wa kumgundua
mtu anayezungumza uongo kwa kumtazama na kwa sababu sikuwa na kawaida ya
kudanganya, nilijua anaweza kunigundua kwa haraka.
Namshukuru Mungu uongo wangu ulipita, baba
akaisukumia ile nguo kwangu kwa kutumia mguu wake wa kushoto. Niliinama haraka
na kuiokota, nikaisunda mfukoni, kiukweli nilijisikia aibu sana kwa sababu mama
alikuwepo, mama yake Rahma alikuwepo na hata Rahma mwenyewe.
Licha ya kulimaliza hilo la kwanza kwa kuongea
uongo, bado mjadala mkubwa ulibaki kwenye ishu ya mimi kusema chumba cha Rahma
kilikuwa kikiwaka moto huku kukiwa hakuna dalili zozote za moto. Niliwaona baba
na baba yake Rahma wakinong’onezana jambo, kisha baba yake Rahma akamnong’oneza
mkewe, baba akanishika mkono na kunitoa nje, baba Rahman naye akafuatia, kwa
lugha nyepesi wanaume tukatoka na kuwaacha mama Rahma, mwanaye na mama.
Tulienda mpaka nje kabisa, tukakaa kibarazani
mimi nikiwa katikati, baba akanigusa begani na kunipigapiga. “Hebu sema ukweli,
nini kilichotokea mpaka ukaenda kuvunja mlango na kumtoa dada yako mzobemzobe.”
“Moto ulikuwa unawake, tena moto mkubwa kwelikweli.”
“Lakini wewe si unafahamu kwamba moto ukiwaka
lazima uache ishara yoyote na unavyosema kwamba ulikuwa ni moto mkubwa,
inawezekanaji muda huohuo sisi tuende chumbani na tusikute moto wala dalili
zozote za moto?” “Aaah… eeh hata mimi ndiyo nasha…ngaa,” nilisema kwa
kubabaika, maji yalikuwa yamenifika shingoni na hata sijui ningetumia lugha
gani ili nieleweke.” “Umeanza kuvuta bangi kama kaka zako?” baba aliniuliza
swali ambalo lilinifedhehesha sana.
Sikuwahi kutumia kilevi cha aina yoyote
tofauti na kaka zangu ambao kule kijijini walikuwa na tabia ya kutembea na
vijana wahuni wa kijiji ambao ilikuwa inaaminika kwamba wanavuta bangi ndiyo
maana walikuwa na uwezo wa kulima mashamba makubwa bila kuchoka au kufanya kazi
ngumu za migodini kwa muda mrefu. Nilitingisha kichwa kukataa, akaniambia
kwamba ananiamini sana ndiyo maana ananipa upendeleo kuliko mtu yeyote kwenye
familia yetu, akanitaka nisimuangushe na kama nina tatizo lolote nimwambie
kuliko kumficha. Baba yake Rahma naye aliongeza kwamba wananiamini na kuna kazi
kubwa mbele yetu ambayo walishakubaliana kwamba watashirikiana na mimi kwa hiyo
lazima niwe makini sana.
“Haya nenda kalale,” alisema baba, nikainuka
kinyonge na kuanza kutembea kuelekea ndani, huku nikijisikia vibaya sana kwa
sababu niliamini nilichokifanya ilikuwa ni kwa nia njema kabisa lakini kibao
kilinigeukia, nikaonekana eti mimi ni mvuta bangi! Nilijisikia vibaya sana
kiukweli.
Nilipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani,
nikaingia na kujitupa kitandani na kuanza kutafakari kwa kina juu ya
kilichotokea. Mambo yalikuwa yametokea kwa kasi mno, yaani siku moja ilikuwa na
matukio chungu nzima, yaani kama ingekuwa ni filamu, basi nina hakika
ingependwa sana.
Kutokana na uchovu wa safari na matukio yote
yaliyotokea kutwa nzima, kuanzia alfajiri tulipoianza safari ya kutoka
Makongorosi mpaka muda huo, tukiwa tayari ndani ya Jiji la Dar es Salaam,
nilipitiwa tena usingizi mzito. Safari hii sikushtuka mpaka asubuhi na kilichoniamsha
zilikuwa ni kelele za mafundi waliokuwa wakitengeneza mlango wa chumba cha
Rahma.
Nikaamka na kukaa kitandani, kumbukumbu za
matukio yaliyotokea jana yake zikaanza kurudi kichwani mwangu, ndugu yangu
niliyelala naye alishaamka muda mrefu tu na hakuwepo chumbani kwa hiyo nilikuwa
peke yangu.
“Kaka Togo! Kaka Togo,” sauti ya kike
ilisikika nje ya mlango wa chumba kile, kabla sijajua cha kufanya mlango
ulifunguliwa, nikakutana na sura nzuri ya Rahma, tabasamu pana likiwa
limechanua usoni mwake. Aligeuka nyuma kama anayetazama kama kuna mtu
anayemuangalia kisha nikamuona akiingia na kufunga mlango kwa ndani.
“Nimekuja kukuita tukanywe chai lakini pia
nimekuletea zawadi,” alisema huku akinipa ‘apple’ la rangi ya kijani. Niliachia
tabasamu na kulipokea, nikaanza kulila kuchangamsha mdomo kwani tangu nimeamka
hata mswaki sikuwa nimepiga. Alikuja na kukaa pembeni yangu pale juu ya
kitanda, akawa ananitazama kwa macho yake mazuri wakati nikilila lile tunda
alilonipa.
“Samahani, eti kwani jana usiku kulitokea
nini? Naomba nisamehe kama nimekusababishia matatizo.”
“Aah, kawaida tu wala usijali.” nilimjibu kwa
mkato, sikutaka kujadiliana naye sana kuhusu kilichotokea, akaendelea kuniuliza
maswali lakini nikawa namkatisha, nikamwambia tutazungumza vizuri kuhusu suala
hilo muda muafaka ukifika.
“Samahani kama nimekuudhi,” alisema huku
akiinuka na kunibusu kwenye shavu langu kisha akanikumbatia na kunibusu tena.
“Usijali kabisa, wala hujaniudhi,” nilisema huku mapigo ya moyo wangu yakianza
kwenda mrama.
Nikiri wazi kwamba Rahma alikuwa mzuri sana,
kitendo cha kunikumbatia, kumbukumbu za tulichokifanya jana yake zilianza
kujirudia ndani ya kichwa changu. Na mimi nilimkumbatia na kushika kiuno chake,
nikamuona akijinyonganyonga huku akinitazama kwa macho kama vile bado alikuwa
na usingizi. Hamasa niliyokuwa naipata, ilinifanya nisiogope chochote, nikaamua
kuyavulia tena maji nguo, tayari kwa kuyaoga.
Muda mfupi baadaye, tulikuwa msambweni na
Rahma lakini safari hii tulikuwa tukijizuia kutoa aina yoyote ya kelele kwani
tulikuwa tunajua kwamba watu wote wameshaamka. Yaani ndani ya muda mfupi tu,
Rahma alishaingia ndani ya moyo wangu na kunifanya nimpende sana na kuwa tayari
kwa chochote.
Tuliendelea kupigiana pasi fupifupi, wakati
mwingine Rahma akawa anashindwa kujizuia na kutoa miguno ya hapa na pale,
tukiwa tunaendelea, tulishtuka baada ya kusikia minong’ono dirishani kwa upande
wa nje. Kwa ilivyoonyesha, kuna watu walikuwa wakifuatilia kila kilichokuwa
kinaendelea.
“Togo,” nilisikia sauti nzito ya baba ikiniita,
harakaharaka nikamtoa Rahma, kila mmoja akawa anahaha kujiweza vizuri.
“Togooo,” alirudia kuniita, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio mno huku
mdomo ukiwa mzito kufunguka. Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment