ILIPOISHIA:
Nilitazama huku na kule, nilipoona
hakuna mtu anayetutazama, nilimsogelea, akanikumbatia kwa mahaba kisha
akanivutia ndani. Hatukukumbuka hata kufunga mlango, kwa makusudi aliuachia ule
upande wa khanga, ukadondoka chini, nikawa kama fisi aliyeona mfupa.
SASA ENDELEA...
Harakaharaka nilichojoa magwanda yangu
huku nikiwa na pupa isiyo na mfano, muda mfupi baadaye tulikuwa saresare maua,
nikamnyanyua Rahma juujuu na kumbwaga kwenye uwanja wa fundi seremala. Mwenyewe
alionesha kufurahia sana, akanibana kwenye kifua chake kilichojaa vizuri,
tukagusanisha ndimi zetu.
Hata hivyo, tofauti na mara zote
ninapokuwa kwenye mazingira kama hayo, ambapo ‘Togo’ wangu huwa mkali kama
nyoka koboko, nilishangaa akiwa kimya kabisa, kama hajui ni nini kilichokuwa
kinataka kutokea.
Kama nilivyoeleza tangu mwanzo, sikuwa
najua chochote kwenye ulimwengu wa kikubwa na Rahma ndiye aliyekuwa wa kwanza
kuniingiza kwenye ulimwengu huo, akifuatiwa na Isri, tena ndani ya siku chache
tu. Kwa hiyo, sikuwa mzoefu na hicho kilichotokea, kilikuwa kitu kigeni kabisa
kwangu.
Nimewahi kusikia kwamba, kwa mwanaume,
hakuna aibu kubwa kama kuwa na mwanamke faragha halafu ukashindwa kazi,
nikajikuta nikiwa na wasiwasi mkubwa kweli ndani ya moyo wangu. Sikujua Rahma
atanichukuliaje, sikujua atanidharau kwa kiasi gani, nikajikuta kijasho
chembamba kikinitoka huku akili ikiwa imehama kabisa.
“Togo, vipi?” aliniuliza Rahma baada ya
kubaini mabadiliko niliyokuwa nayo. Swali lake lilinifanya nizidi kujisikia
aibu, nilikosa cha kujibu na kiukweli sikuwa na majibu. Alipeleka mkono bondeni
yaliko makazi ya ‘Togo’ na kujaribu kumpa hamasa kwa kutumia mikono yake laini
lakini ilikuwa sawa na kazi bure.
“Mshukuru sana Mungu wako, ulikuwa
unaenda kumuua mtoto wa watu, mshenzi sana wewe,” nilisikia sauti ya baba
ikiniongelea sikioni kwa ukali, ikafuatiwa na msonyo mrefu, nikakurupuka kwa
hofu kubwa, nikawa namtazama Rahma nikiwa nimekodoa macho, kijasho chembamba
kikinitoka.
Nilikumbuka tukio lililonitokea na Isri,
nilipokutana naye kwa mara ya kwanza faragha, ambapo tukiwa mchezoni, ghafla
‘alikata roho’ ingawa baadaye nilikutana naye tena akiwa mzima na ndiyo
yakatokea yale yaliyotokea usiku uliopita. Alichokisema baba kilinifanya nihisi
kwamba huenda kuna kitu kibaya mwilini mwangu ambacho ndiyo chanzo cha yote na
nikifanya masihara, kweli Rahma atakufa na kusababisha msiba mzito kwa familia
yake.
Nilikumbuka pia kauli ya Isri kwamba
mimi ndiye mwanaume pekee niliyeweza kuushinda mtihani wa kifo baada ya
kukutana naye kimwili.
“Togo, una nini mpenzi wangu,” alisema
Rahma huku akisimama, naye akionesha kushangazwa na kilichotokea. Alinisogelea
na kutaka kunikumbatia lakini nilijitoa harakaharaka, nikavaa nguo zangu huku
nikiendelea kuhema kwa nguvu, nikamuona Rahma akikaa pembeni ya kitanda na
kujiinamia, machozi yakaanza kumtoka.
Niliondoka haraka na kuelekea bafuni,
nikajifungia mlango kwa ndani na kujiinamia, nikiwa hata sielewi nini cha
kufanya. Ilibidi nijimwagie tena maji, mwili wangu ukapata nguvu, nikatoka na
kwenda chumbani kwangu, nikawa nimejilaza huku nikiendelea kutafakari
kilichotokea.
Kwa mbali ile kiu kali ya kukutana
kimwili na mwanamke ilinianza upya, nikawa najiuliza, inawezekanaje muda mfupi
tu uliopita nimeshindwa kabisa kufanya chochote na Rahma na kumuacha akiwa na
huzuni kubwa kwenye moyo wake, halafu dakika chache baadaye niwe na hamu kali
isiyoelezeka.
Nilipokumbuka ile kauli ya baba, niliona
kabisa kinachoenda kutokea ni janga kubwa kwa Rahma kwa sababu muda si mrefu,
mimi ningeenda chumbani kwake au yeye angekuja kwangu, tungeanza kubembelezana
na mwisho tungeishia kuangukia dhambini, na matokeo yake dhambi ingekomaa na
kuzaa mauti kwa Rahma, jambo ambalo lingenifanya niishi na hatia ya kukatisha
maisha ya mtu asiye na hatia milele.
Nilichokifanya, harakaharaka niliamka
pale kitandani, nikavaa viatu vyangu na kutaka kutoka lakini nilikumbuka kwamba
giza halikuwa limeingia kwa hiyo kutoka nje kungemaanisha kwamba ningepata
madhara makubwa kama Isri alivyonipa masharti.
Niliamua kwenda kukaa sebuleni, ndugu
zangu pamoja na wadogo zake Rahma wakawa wananishangaa. Kwa muda mfupi tu
tuliokaa hapo nyumbani, tayari nilishaonesha tabia za ajabu sana. Kila mtu
akawa ananitazama kwa macho ya chinichini, haikuwa kawaida yangu kukaa
sebuleni.
Nilijikaza kiume, nikakazia macho kwenye
runinga, nikawa sina habari na mtu, ukimya ukatanda pale sebuleni. Baba na baba
yake Rahma walikuwa wamekaa kwenye sehemu ya kulia chakula, wakiwa wanacheza
bao huku mama na mama yake Rahma wenyewe wakiwa jikoni.
Muda mfupi baadaye, Rahma alikuja na
kuchungulia pale sebuleni, alipochungulia tu, macho yangu na yake yakagongana,
akanionesha ishara ya kuniita kwa mkono kisha nikamsikia akitembea kuelekea
chumbani kwake.
“Mungu wangu, sasa itakuwaje?” niliwaza,
nikaamua kujikausha kama sijamuona Rahma, nikawa naendelea kukazia macho kwenye
runinga imngawa kiukweli wala akili zangu hazikuwa pale na sikuwa najua hata
kunaoneshwa nini.
Muda mfupi baadaye, Rahma alikuja tena
lakini safari hii, alikuja na kukaa kwenye kochi nililokuwa nimekaa mimi, uso
akiwa ameukunja. Nilijua kwamba amekasirika lakini sikuwa na namna zaidi ya
kujiepusha naye, nilikuwa nampenda Rahma na sikuwa tayari kuona anapatwa na
jambo lolote baya.
Alikuwa amejifunga khanga nyepesi na
ndani hakuwa na kitu kabisa, nikazidi kujikuta kwenye wakati mgumu, tukawa tunatazama
runinga bila mtu yeyote kumsemesha mwenzake. Hata wale ndugu zetu nadhani nao
waligundua kwamba hatupo sawa kwa sababu si kawaida ya mimi na Rahma kukaa
sehemu moja bila kusemeshana, tena mara nyingi tulikuwa tukicheka na kufurahi.
Dakika kadhaa baadaye, Rahma alibadili
mkao aliokuwa amekaa, akanisogelea halafu akawa ni kama ameniegamia kimtindo,
haikuwa rahisi kwa watu wengine kuelewa kilichokuwa kinaendelea lakini kiukweli
nilijikuta nikipata msisimko mkubwa sana.
Mwisho niliamua kukata shauri maana na
mimi nilikuwa nateseka, nikaamua liwalo na liwe, nikamgeukia Rahma na kumtazama
usoni, naye akanigeukia, tukawa tunatazamana machoni, nikampa ishara kwamba
atangulie ndani, akaniitikia huku akinitazama kwa macho yenye hisia kali za
mapenzi.
Aliinuka na kutembea kwa madoido, nikawa
namsindikiza kwa macho, nikawaona watu wote pale sebuleni wakitazamana.
Nilishusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye kiti, nikawa navutia kasi ili na
mimi niinuke na kumfuata Rahma kule ndani, tukatii kiu zetu.
“Togoo,” nilisikia sauti ya baba
akiniita, nikaitika na kusimama, ilibidi nijiweke vizuri maana ilikuwa aibu kwa
wote waliokuwa pale sebuleni, nikaelekea kule walikokuwa wamekaa baba na baba
yake Rahma.
“Wewe sasa hivi una mambo ya kikubwa,
hutakiwi kuwa unachanganyikana na wenzako, inabidi uanze kukaa na sisi baba
zako, vuta kiti kaa hapa,” alisema baba, akawa ametibua shoo nzima, nilitaka
kutoa visingizio lakini hakutaka kusikia chochote kutoka kwangu, ikabidi nikae
na kujiinamia, wote wakawa wananitazama.
Je, nini kitafuatia? Usikose Jumatatu
kwenye Championi Jumatatu.
No comments:
Post a Comment