ILIPOISHIA:
Niliendelea
kumkumbatia msichana huyo huku marafiki na jamaa zangu wengine wakiwa pembeni
wakitutazama, tukiwa kwenye hali hiyo, nilisikia mlango wa wodi ukifunguliwa na
mtu akaingia mbiombio mpaka pale kitandani kwangu, nikashtuka na kumuachia
Raya, Raya naye akainua uso wake, watu wote tukawa tunamtazama kwa mshangao mtu
yule aliyeingia, tukiwa ni kama hatuamini.
SASA
ENDELEA...
Hakuwa
mwingine, bali Shenaiza ambaye alikuwa amevaamavazi ya hospitalini hapo
kuonesha kwamba alikuwa amelazwa, mkononi akiwa na sindano iliyofungwa na
plasta, nafikiri kwa ajili ya kumuingizia dawa au kumtundikia dripu, nikawa
namtazama usoni, naye akawa ananitazama.
“Jama!
Kumbe ni kweli hujafa?” alisema Shenaiza kwa sauti ya kukwamakwama, wote
tukatazamana tena kisha nikageuka na kumtazama Shenaiza, alionesha kabisa
kwamba hakuwa sawa, nikawa najiuliza maswali mengi kichwani ambayo sikuwa na
majibu yake.
Nilikumbuka
kwamba kuna muda mimi na Shenaiza tulikuwa tumnekaa siti moja kwenye treni la
ajabu, tukielekea kusikojulikana, giza likiwa limetanda kila sehemu. Kama mimi
nilikuwa kitandani, wodini, na Shenaiza naye alikuwa hospitalini hapo akiwa
amelazwa, ina maana kwamba mimi na yeye tulikutana wapi?
Nilikumbuka
pia kwamba yeye mwenyewe aliniambia kwamba ameamua kuyakatisha maisha yake kwa
kujiovadozi dawa ya usingizi, na kwamba aliamua kufanya hivyo kama njia ya
kupumzika na mateso aliyokuwa anayapata, sasa Shenaiza aliyejiua ni nani na
huyo aliyekuwa amesimama mbele yangu ni nani?
Nilihisi
kama kichwa kinapata moto kwa sababu ya utata wa kilichokuwa kinaendelea, hata
hivyo nilipoemndelea kutuliza kichwa changu, nilianza kupata baadhi ya majibu.
“Kumbe
kweli hukufa?” Shenaiza aliniuliza tena swali lile ambalo lilinizindua kutoka
kwenye lindi la mawazo.
“Hebu
naomba mtupishe kidogo nizungumze na Shenaiza,” niliwaambia watu wote waliokuwa
wamenizunguka pale wodini lakini Raya alikataakatakata.
“jamal!
Are you out of your mind?” (Jamal umechanganyikiwa) alisema raya kwa sauti ya
juu. Akaendelea kuniambia kwamba Shenaiza ndiye aliyekuwa chanzo cha mimi
kutaka kupoteza maisha, iweje leo nimuone yeye ndiyo wa maana kiasi c ha
kuwataka watu wote watoke nje?
“Kama
amekuja kwa lengo la kukumalizia je? Mimi siendi popote, nitakaa hapahapa kukulinda,”
alisema Raya huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara, nikashindwa
cha kufanya.
Wale
watu wengine wote walitoka lakini kama Raya alivyosema, hakutaka kuinuka pale
pembeni ya kitanda changu alipokuwa amekaa na mimi sikuona sababu yoyote ya
kumlazimisha.
Bado
tulikuwa tukiendelea kutazamana na Shenaiza, kadiri nilivyokuwa nazidi
kumtazama ndivyo nilivyokuwa naendelea kukumbuka mambo mengi yaliyotokea kwenye
ulimwengu usio wa kawaida na kwenye ulimwengu wa kawaida.
“Haya
sema shida yako iliyokuleta,” Raya alivunja ukimya, Shenaiza akashusha pumzi
ndefu na kusogea kwenye kitanda nilichokuwa nimelazwa.
‘Samahani
dada wala mimi sijaja hapa kwa nia mbaya, kwanza nimejikaza tu kwani bado
naumwa sana, nimetoroka tu wodini baada ya kusikia Jamal yupo hapa,” alisema
Shenaiza kwa sauti ya chini, nikamuona Raya naye akishusha pumzi kwani
alishajiandaa kwa shari lakini msichana huyo akaonesha kwamba hakuwa amekuja
kisharishari.
“Nilisikia
kwamba umekufa na mimi nilithibitisha hilo,” alisema Shenaiza kwa upole,
nikamuliza amesikia wapi na amethibitishaje hilo?
“Niliambiwa
na daktari mmoja kati ya wale waliokuwa wanakutibu, akaniambiakwamba ulishakata
roho lakini walikuwa wamekuunganisha kwenye mashineya kusaidia moyo wako
uendelee kudunda, akanihakikishia kwamba saa chache baadaye watakutoa kwenye
mashine hiyo.
“Mh!
Sikuelewi! Raya wewe unamuelewa anachokisema huyu?”
“Mimi
namuelewa, ni kweli hata mimi daktari aliniambia kwamba huwezi kupona,” alisema
Raya na kunifanya nikose cha kujibu, nikawa nawatazama mmoja baada ya mwingine
usoni kwa zamu. Unajua miongoni mwa mambo ambayo sikuwa nataka kuyasikia, ni
kwamba eti watu wote walikuwa wanajua kwamba nimekufa.
“Halafu
kuna mambo yananichanganya sana kichwa changu, sijui ni ndoto, maruweruwe au
uchawi hata sielewi. Mbona nakumbuka kama mimina wewe kuna sehemu tulikutana
halafu tukaongea mambo mengi tu? Na kubwa zaidi mbona nakumbuka kama na mimi
nilikufa?”
Swali
hilo la Shenaiza liliunga kabisa na kile nilichokuwa nakifiria kichwani mwangu
muda wote. Ni kweli hata mimi nilikuwa najua kwamba kuna sehemu mimina Shenaiza
kuna sehemu tulikuwa pamoja na tukazungumza mambo mengi tu pamoja, tena tukiwa
tumekaa kwenye siti moja kwenye treni la ajabu.
“Utakuwa
ulikuwa unaota, ulikutana wapi na Jamal wakati tangu siku ile ulipomsababishia
atake kufa hajainuka kitandani na leo ndiyo amefumbua macho?” Raya aliingilia
mazungumzo yale, sote tukawa tunamtazama kwa sababu hakuwa akijua chochote.
“Mh!
Inawezekana kweli nilikuwa naota, kwa sababu katika maisha yangu sijawahi
kupanda treni hata siku moja lakini nakumbuka eti tulikuwa tumekaa kwenye siti
mojaya treni,” alisema Shenaiza na kuzidi kunihakikishia kwamba kumbe kile
kilichotokea kilikuwa ni jambo halisi, Raya akazidi kubisha.
“Sasa
mtu yupo kitandani anaumwa hoi hajitambui atapandaje treni? Dada ulikuwa unaota
na sidhani kama Jamal anahitaji kusikia ndoto zako, kama hicho ndicho
kilichokuleta naomba uondoke, mgonjwa anahitaji kupumzika,” alisema Raya kwa
msisitizo.
“Basi
tuachane na hayo, Jamal nimekuja kukuomba msamaha!”
“Msamaha
wa nini Shenaiza?”
“Kwa
yote niliyokufanyia. Haikuwa kusudioa langu kukuingiza kwenye matatizo, najua
wewe na watu wako wote wa karibu mnanichukia sana.”
“Msamaha
wako una maana gani leo? Kama angekuwa amekufa ungemuomba nani msamaha? Dada
hebu nakuomba uondoke,” Raya alijibu kwa ukali, nikamuona Shenaiza akijiinamia
na kuanza kuangua kilio.
“Wewe!
Kwa nini unatusumbua kukutafuta? Kwa nini unatoka wodini bila taarifa wakati
unajua hali yako siyo nzuri? Unatusababishia matatizo kwa ndugu zako,” manesi
wawili waliingia mbiombio mle wodini, akawamshika Shenaiza huku an kule na
kumtoa msobemsobe huku mwenyewe akiendelea kuangua kilio. Mimi na Raya
tukatazamana!
“Inaonesha
mnafahamiana kuliko hata mimi ninavyojua, huyu si mmekutana juzijuzi tu hapo,
mbona inaonesha kama kuna kinachoendelea nyuma ya pazia?” Raya aliniuliza,
akionesha dhahiri kuwa na wivu mkali ndani ya moyo wake, nikashindwa cha
kumjibu.
“Jamal,
nakupenda sana mpenzi wangu, nakuomba uamini ninachokisema. Sijawahi kumpenda
mtu yeyote katika maisha yangu na wewe mweyewe ni shahidi kwamba umenikuta
nikiwa simjui mwanaume yeyote.
“Niliamua
kukupa zawadi ya kuwa mtu wa kwanza kunijua na nataka uwe wa mwisho kwangu,
nataka unioe tuishi pamoja milele Jamal,” alisema Raya huku machozi yakimlengalenga.
Kiukweli
na mimi nilikuwa nimetokea kumpenda Raya baada ya kuwa nimeutezsa moyo wake kwa
kipindi kirefu na kweli nilishaanza kuweka mnalengo ya maisha yangu ya baadaye
nikiwa naye lakini niliona kama huo siyo muda muafaka wa kuzungumzia mapenzi.
Ndiyo
kwanza nilikuwa nimerejea kwenye ulimwengu wa kawaida, bado kuna maswali mengi
ambayo sikuwa nimeyapatia majibu, kuhusu mimi mwenyewe na pia kumhusu Shenaiza
na familia yake.
Hata
hivyo, sikutaka Raya ajisikie vibaya kwa namna yoyote, mwenyewe nilishajiwekea
nadhiri moyoni kwamba nitakuwa sehemu ya furaha ya raya, hasa baada ya kugundua
ni kwa kiasi gani alikuwa akinipenda.
Nikamkumbatia
na kubusu kwenye paji lake la uso, nikamwambia hakuna chochote kinachoendelea
kati yangu na Shenaiza isipokuwa ilikuwa ni lazima niendelee kuwa naye karibu
kwa sababu kuna mambo muhimu ilikuwa ni lazima niyajue, hasa kuhusu baba yake
Shenaiza.
“Kuna
kazi nimepewa ya kuhakikisha namzuia baba yake Shenaiza hicho anachokifanya, na
ni lazima nitimize.”
“Kazi?
Nani aliyekupa hiyo kazi? Halafu umzuie kwani anafanya nini na wewe umejuaje?”
Raya alinibana kwa maswali, nikawa nashindwa hata namna ya kumjibu.
Je,
nini kitafuatia? Usikose Ijumaa kwenye Gazeti la Championi Ijumaa.
No comments:
Post a Comment