ILIPOISHIA:
“Habari za saizi nesi,” Raya alimsalimia
Shamila kwa unyenyekevu, jambo ambalo hakuwahi kulifanya kabla. Shamila naye
akajibu kwa uchangamfu, nikabaki njia panda. Sikujua walizungumza nini muda ule
mpaka wakamaliza tofauti zao. Raya akaja mpaka pale kitandani na kunibusu
mdomoni, Shamila akageuka na kulishuhudia tukio hilo.
SASA ENDELEA...
Alipogundua kwamba namtazama,
harakaharaka Shamila alijifanya kama hakuwa ameona chochote.
“Leo nimekupikia chakula kizuuri,
naamini utakipenda,” alisema Raya huku akianza kuniandalia chakula. Nikawa
nimetulia pale kitandani huku akilini mwangu mawazo mengi yakipita. Nilikuwa
nimeingia kwenye mtego hatari sana ambao sasa ilikuwa ni lazime nifanye kila
kinachowezekana kujikomboa.
Njia pekee ambayo ingenisaidia, ilikuwa
ni kuhakikisha baba yake Shenaiza na kundi lake lote wanafikishwa mbele ya
sheria na mamia ya watu ambao maisha yao yalikuwa hatarini, wanaokolewa kutoka
kwenye shimo la mauti.
Ni jambo hilo pekee ndiyo lingenifanya
niwe na amani kwa sababu bila kumdhibiti baba yake Shenaiza, maana yake ni kwamba
angeendelea kunisaka kwa lengo la kuniua, akiamini tayari kuna siri zake nyingi
nazijua, lakini pia maana yake ni kwamba baada ya kunimaliza mimi, angefuatia
Shenaiza na baada ya hapo, angeendelea na kazi yake haramu ya kuteketeza maisha
ya watu bila huruma.
“Mbona unaonekana kama una mawazo mengi,
nini kinakusumbua?” swali la Raya ndilo lililonizindua kutoka kwenye dimbwi la
mawazo. Akaacha kuandaa chakula na kunisogelea, akaniinamia pale kitandani na kunibusu
kwenye paji la uso, akawa ananiuliza kwa upole kinachonisumbua.
Mpaka muda huo, Raya hakuwa akielewa
chochote kilichokuwa kinaendelea, zaidi ya kufahamu tu kwamba nilikuwa
hospitalini nimelazwa baada ya kuvamiwa na majambazi ambao almanusra wayakatishe
maisha yangu. Hakuwa anajua ‘connection’ iliyokuwepo kati ya matukio yaliyokuwa
yananitokea hata kidogo.
“Kuna jambo linanisumbua sana kichwa
changu.”
“Jambo gani mpenzi wangu, si unajua
sipendi kukuona ukikosa raha?”
“Najua mpenzi wangu, mambo yamenifika
shingoni,” nilimwambia Raya, akazidi kunidadisi ambapo nilimwambia aniandalie
kwanza chakula mengine tutaongea baadaye.
Kwa jinsi hali ilivyokuwa, sikuona
sababu ya kuendelea kumficha Raya, nilitaka nimueleze ili naye akae akiwa
anaelewa kuhusu kipindi kigumu nilichokuwa napitia ili kama kuna msaada wowote
anaweza kunisaidia afanye hivyo.
Baada ya kumaliza kuandaa chakula,
alinisogezea na kuanza kunibembeleza nile. Kwa jinsi alivyokuwa amepika chakula
vizuri, nilikula chote mpaka nikamaliza, jambo ambalo lilimfurahisha sana.
“Enhee, haya niambie sasa,” alisema
baada ya kumaliza kutoa vyombo, kama nilivyokuwa nimedhamiria kutoka ndani ya
moyo wangu, nilianza kumueleza ukweli wa kila kitu. Jambo pekee ambalo
sikumueleza, kama ilivyokuwa kwa Shamila, ni kile kilichonitokea baada ya
kupoteza fahamu. Nilihisi naweza kumjaza woga moyoni akaanza kunitazama kwa
macho yasiyo ya kawaida.
Nilimficha pia suala la mimi na Shamila
kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, nikamwambia kwamba alitokea kuguswa na kilichonipata
na kuamua kunisaidia kwa sababu hata yeye kuna ndugu yake amewahi kusafirishwa
na shirika hilo na mpaka muda huo hawakuwa na mawasiliano naye. Niliamua
kutumia uongo huo ili asishtuke mapema kwamba mimi na Shamila tulikuwa na
uhusiano wa kimapenzi
Kiukweli Raya alishtuka sana
nilipomueleza kilichokuwa kinaendelea, akawa hataki kuamini, akawa anahisi
labda nimeamua kumtungia stori za kumtisha. Nilimhakikishia kwamba kila kitu
nilichomwambia ni kweli na kama anataka kuthibitisha, ipo siku atajionea
mwenyewe.
Nilimuona Raya akishusha pumzi ndefu,
akainua shingo yake akiwa anatazama huku na kule kisha akanigeukia: “Kwa hiyo
wewe ulikuwa umeamuaje?”
“Ni lazima nipambane nao.”
“Jamal, umechanganyikiwa nini? Unawezaje
kupambana na watu hatari kama hao?”
“Ni lazima nifanye hivyo Raya, sipo
tayari kufa kama kifaranga cha kuku mbele ya mwewe, ni lazima nipambane.”
‘Sidhani kama hilo ni jambo sahihi kwa
sasa, isitoshe bado hata afya yako haijawa poa, kwa nini tusitafute sehemu nje
ya Dar tukaenda kujificha huko na kuanzisha maisha yetu bila mtu yeyote kujua?
Mimi nipo tayari hata sasa hivi na naamini nikiwaambia wazazi wangu watakuwa
tayari kutusaidia,” alisema Raya, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama.
“Ni lazima nipambane Raya, siwezi
kuwakimbia. Najua ni kazi ngumu lakini mwisho wa siku ni bora nife nikiwa
napambana,” niliendelea kushikilia msimamo, raya akawa hana cha kuniambia tena.
Bado alikuwa na maswali mengi yaliyokosa
majibu ndani ya kichwa chake, akawa ananiuliza kila alipokuwa anakumbuka.
Aliniuliza kama watu hao ndiyo walioenda kuvunja nyumba yangu siku ile usiku,
nikamjibu kwamba kwa ushahidi huo, inaonesha moja kwa moja kwamba ni wao.
Maswaliyalikuwa mengi mpaka ikabidi
nimkatishe, nikamwambia anatakiwa kupeleka vyombo nyumbani ili na yeye apate
muda wa kupumzika, nikamuona akisimama kwa shingo upande na kukusanya vitu
vyake.
“Nimeongea na daktari, anasema naweza
kuruhusiwa ndani ya siku hizi mbili kwa sababu naendelea vizuri.”
“Ooh! Itakuwa vizuri sana, sasa umepanga
ukitoka ukaishi wapi?”
“Itakuwa ni siri yangu lakini kwa sasa
sitakiwi kukaa pale kwangu kwa sababu najua watakuwa wananiwinda usiku na
mchana.”
“Natamani sana tukaishi nyumbani kwetu,
wazazi wangu wanakaribia kurudi lakini usijali ile nyumba ni kubwa, wanaweza
kukupa hata vyumba vya uani, ukakaa hapo chini ya uangalizi wangu mpaka mambo
yatakapotulia.”
“Ahsante sana mpenzi wangu, hivi kazini
unaenda kweli wewe?”
“Kazini siendi, nimeomba ruhusa kwamba
nakuuguza wewe, kwanza ukiwa kama mfanyakazi mwenzangu na pia ukiwa mume wangu
mtarajiwa, kwa hiyo usijali,” alisema Raya huku tabasamu pana likiwa limechanua
kwenye uso wake, akakusanya vitu vyake, akaja kunibusu kisha akaniaga.
Akatoka na kufunga mlango, mara Shamila
naye akaingia, ni kama alikuwa amekaa sehemu anasubiri aondoke tu ili na yeye
aingie. Akaja uso akiwa ameukunja, nilishaelewa ni kwa sababu gani yupo kwenye
hali hiyo.
“Vipi?”
“Mbona unapenda kunitesa Jamal, kwani
huyo mwanamke wako huwezi kumkataza kukubusu mbele yangu?”
“Siyo hivyo mpenzi wangu, naomba kaa
kwanza tuzungumze.”
“Sitaki, na kwa sababu yeye ameanza basi
mimi namaliza,” alisema Shamila na kwenda kufunga mlango kwa funguo, akashusha
na mapazia yote, nikawa sielewi alichokuwa anataka kukifanya.
“Nikiwa bado nimepigwa na butwaa,
nilishtuka kumuona akianza kufungua vifungo vya gauni lake la kazini, mara
akalivua na kubaki na sidiria na nguo ya ndani tu, ukichanganya na jinsi
alivyokuwa amegawanyika na kujaa sehemu za katikati, nilijikuta nikikosa cha
kufanya.
“Una..ta..ka kufa...nya ni...ni,”
sikumalizia kauli yangu, akawa tayari ameshafikapale kitandani, tukagusanisha
ndimi zetu huku Shamila akionesha kweli kudhamiria kile alichokitaka. Hakuogopa
kabisa kwamba pale ni wodini.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeletebuy best
ReplyDelete