Wednesday, January 31, 2018

KIVURUGE WA TANDALE- 4



ILIPOISHIA:
Mara nikasikia mlango unafunguliwa, nikashtuka na kuinuka haraka kutaka kutazama ni nani aliyekuwa akiingia, nikashtuka kumuona Salma, mtoto wa kike akiwa ameingia kwenye vyoo vya wanaume, nilipomtazama vizuri alikuwa akilia, machozi yakawa yameulowanisha uso wake.
SASA ENDELEA...
Harakaharaka niliacha kila nilichokuwa nakifanya, nikalishika shati na kutaka kulivaa lakini nilikuwa nimechelewa, Salma alifunga mlango wa maliwatoni kwa ndani kisha akanisogelea mpaka mwilini, huku machozi yakiendelea kumtoka.
“Umepatwa na nini Salma?”
“Kwa nini unanitesa? Ina maana hujui kama nakupenda? Kwa nini unanitesa Ashrafu,” alisema Salma huku akipitisha mkono wake na kunishika kiunoni, akanisogelea na kujilaza kwenye kifua changu.

Ulikuwa ni zaidi ya mshtuko kwangu, nimefanya kazi na Salma kwa zaidi ya mwaka mzima na kamwe sikuwahi kuhisi hata mara moja kwamba alikuwa na hisia za mapenzi na mimi.
Mara kwa mara ugomvi wa mimi na yeye ulikuwa ni kwenye kupishana kauli, tabia yake ya kuwa na kisirani muda wote ilifanya watu wengi wawe wanaogopa kumuuliza chochote lakini mimi sikuw anamuogopa na mara kwa mara alipokuwa akinijibu kwa mkato nilikuwa nikimjia juu, kiasi kwamba kulumbana lilikuwa jambo la kawaida kwetu.
Nakumbuka siku chache zilizopita niliamua kuiweka namba yake kwenye ‘black list’ kwa sababu alikuwa na kawaida ya kunipigia simu muda ambao siyo wa kazi na kuanza kunilaumu mambo chungu nzima yanayohusiana na kazi, mara kwa nini nimeondoka bila kuaga, mara bosi ananitafuta, mara kwa nini nimeondoka bila kupanga vifaa vyangu vya kazi vizuri, basi ilikuwa ni purukushani nguo kuchanina.
“Sasa kinachokuliza ni nini Salma jamani?” nilisema kwa upole huku nikijifuta maji kwa kutumia kitambaa, mkono mmoja na mimi nikiwa nimemshika Salma kwa upole.
“Wewe unaona ulivyonijibu pale mlangoni kwa bosi ni vizuri? Kwa nini mimi najipendekeza kwako kila siku lakini huoni umuhimu wangu?”
“Lakini Salma, wewe ndiyo kila siku umekuwa mstari wa mbele kunituhumu mimi kwamba sijatulia, nina wanawake wengi na nahisi hata bosi umeshamwambia kwamba mimi naitwa Kivuruge, unawezaje leo kusema kwamba unanipenda?”
Nilimuuliza kwa upole huku nikimtazama usoni, mkono wangu nikiwa nimeuhamisha na kukishika kidevu chake kilaini, akawa ananitazama ka macho yaliyoonesha dhahiri kwamba alichokuwa akikisema kinatoka ndani ya moyo wake.
“Yote hayo ni kwa sababu nakupenda! Ningekuwa sikupendi ningekufuatilia wa nini? Ningekuwa sikupendi ningekuwa nakupigiapigia simu?”
“Lakini mbona hata kwenye simu kila ukinipigia unanilaumu na kunifokea?”
“Sasa wewe unatakaje Ashrafu? Unataka nikupigie nikuchekee ili unione najitongozesha kwako?” alisema Salma huku akikunja uso wake kama kawaida yake, nikahisi maswali yangu kwake yalishamchosha, nikashusha pumzi ndefu na kumsogeza kwangu, nikambusu kimahaba mdomoni.
Kitendo hicho kilionesha kumchanganya sana, na yeye akanibusu na katika hali ambayo sikuitegemea, nilimuona akianza kufungua vifungo vya blauzi aliyokuwa ameivaa, huku akinitazama kwa macho yake yaliyokuwa yamebeba hisia nzito za mapenzi.
Ni muda huohuo nilikuwa nimetoka kumsulubu Madam Bella na tayari Salma naye alikuwa na uhitaji uliovuka mipaka, nitafanya nini? Nilijiuliza ndani ya kichwa changu, nikaona siwezi kuiacha bahati ile ya mtende inipite kwa sababu ukiachilia mbali kasoro yake ya kuwa na hasira muda wote, Salma alikuwa ‘kifaa’ cha nguvu.
Alipofungua vifungo vya blauzi yake, macho yangu yalitua juu ya maembe bolibo mawili yaliyokuwa yamejaa vizuri kifuani kwake, nikajikuta nikimeza mate kama fisi aliyeona mfupa, kwa ufundi wa hali ya juu nilipitisha mkono mmoja mpaka mgongoni kwake, nikaigusa ‘loki’ ya sidiria yake kwa ufundi, ikafyatuka na kusababisha iachie, nikayavamia maembe bolibo huku nikianza kuyafakamia, kuanzia kwenye ‘kikonyo’ kuja juu.
Salma alianza kupiga ukelele uliosababisha mashetani yangu yaamke, nikasahau kabisa kwamba muda huohuo nilikuwa nimetoka kwenye kazi nzito, nikaendelea kucheza na maembe bolibo hayo kwa ufundi wa hali ya juu.
Mashetani yalipopanda mpaka kichwani, sikuwa na simile tena, nilimnyanyua Salma na kumuweka juu ya sinki la kunawia mikono mle maliwatoni, nikalisogeza ‘kufuli’ pembeni, Salma akashtuka maana ni kama hakutegemea tukio hilo.
Sikuwa na muda wa kupoteza, nikaanza kulisakata kabumbu kwa mtindo wa pasi ndefundefu, umahiri wangu ukaonesha kumkosha sana roho Salma kwa sababu ilifika mahali akasahau kama tupo maliwatoni, tena sehemu ya wanaume, akawa anaachia miguno kwa sauti ya juu.
Nililazimika kufanya kitu ili kunusuru hali halisi, mkono wangu mmoja nikaupeleka kwenye mdomo wake na kuuziba, nikaendelea kuonesha umahiri wangu, kwa kupiga chenga za mwili, danadana, kanzu na hatimaye nikabaki mimi na mpira golini.
Nilichokifanya, nilitishia kama nataka kupiga shuti, Salma akajibinua kwa lengo la kuzuia, nikaurudisha mpira mguuni na kuukokota mpaka pembeni kidogo, nikatishia tena kama napiga, nikambabatiza Salma na kusababisha aanze kupaparika kama kuku aliyekatwa kichwa.
Hakuchukua raundi, akajifunga mwenyewe huku safari hii mkono niliouweka kwenye mdomo wake ukishindwa kufua dafu kuzuia kelele zake za kushangilia goli.
Harakaharaka nilimuinua pale juu ya karo, safari hii mwili wake ukiwa umelegea kabisa, nikafungulia bomba la maji na kumlowanisha kidogo usoni, akawa ni kama amezinduka kutoka kwenye usingizi mzito.
“Ashrafu, we mkali sana jamani, kumbe ndiyo maana wanakugombea licha ya tabia yako mbaya,” alisema kwa sauti iliyokuwa inatokea puani, nikatabasamu tu. Nilijimwagia maji harakaharaka maana mwili wote ulikuwa umelowa chapachapa, nikaona kama nikiendelea kumuendekeza Salma, huenda tukakutwa kule maliwatoni halafu uwe msala.
“Nina kazi, kama vipi baadaye,” nilisema huku nikivaa shati langu harakaharaka, nikafungua mlango na kuchungulia nje, hakukuwana mtu koridoni, nikatoka haraka na kumuacha Salma akinawa.
Nilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye meza yangu, nikajinyoosha kwenye kiti cha kuzunguka huku nikitazama kazi kibao zilizokuwa zinanikabili, ambazo nilitakiwa kuzifanya mara tu baada ya kurejea kutoka ‘lunch’.
“Aah! Nitazifanya kesho, siwezi kufanya chochote kwa sasa,” nilisema huku nikiweka vitu vyangu vizuri. Nilijua lazima Salma akitoka kule maliwatoni, atanifuata pale kwangu, na bosi naye akizinduka kutoka usingizini, lazima pia atanifuata.
Ili kuepusha mkanganyiko, kwanza nilizima simu yangu halafu haraka nikaanza kushuka kwenye ngazi kuelekea chini, huku miguu yangu ikiwa haina nguvu kabisa, nikawa nachekacheka mwenyewe kwa jinsi nilivyofanikiwa kuwapiga ndege wawili kwa jiwe moja, tena kwenye mazingira yenye ukakasi.
“Kaka vipi? Kama vipi kesho bwana mi nasepa zangu.”
“Wapi sasa hiyo!”
“Tandale mzee, si unajua mida ya kurudisha majeshi kihomu,” nilikuwa nikizungumza na mlinzi wetu ‘sharobaro’ pale ofisini,  Shija ambaye tumezoeana naye sana kutokana na haiba yake ya ucheshi.
“Sasa sikia, kuna duu alikuja kukutafuta hapa, nimepanda mpaka ofisini kwako sijakukuta, kasema kama vipi ukipata muda umpigie simu, namba yake hii hapa,” alisema Shija, nikashtuka kwa sababu sikuwa na miadi na mtu yeyote kwa muda huo.
“Ooh, tena imekuwa bahati nzuri, kumbe hakuwa ameenda mbali, yule pale anakupungia mkono,” alisema Shija huku akinionesha kwa kidole upande wa pili wa barabara, mahali palipokuwa na kigrosari cha vinywaji baridi, nikatazama huku nikiwa na shauku ya kutaka kujua ni mwanamke gani aliyekuwa akinisaka kwa udi na uvumba kiasi hicho.
Nilijikuta nikishtuka, mapigo ya moyo yakaanza kuienda mbio kwa sababu ni jambo ambalo sikulitegemea kabisa. Sikukumbuka hata kumalizana na Shija, harakaharaka nikavuka barabara kuelekea upande ule aliokuwa amekaa yule mrembo, huku nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia anataka kuniambia nini.
“Mambo kivuruge?” alinisalimia huku akitabasamu, nikashtuka amelijulia wapi jina hilo? Uso wangu ukajawa na aibu.
Je, nini kitafuatia? Usikose Jumamosi kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...