ILIPOISHIA:
Harakaharaka
nikafungua mlango nikiwa ni kama siamini nilichokisikia, nikamkuta Shenaiza
akihangaika kujigeuza, jambo ambalo hakuwa amelifanya kwa kipndi kirefu tangu
akiwa kule hospitalini.
“Shenaiza!
Shenaiza,” nilisema huku nikipiga magoti pembeni ya kitanda chake. Bado hakuwa
amefumbua macho yake.
SASA
ENDELEA...
Hata hivyo, japokuwa hakuwa amefumbua
macho, niliona akiyapepesa kama anayetaka kuyafumbua, nikainua mikono juu kama
ishara ya kumshukuru Mungu. Kumbukumbu za yote yaliyotokea kuanzia siku ya
kwanza msichana huyo aliponipigia simu mpaka muda huo zilipita kwa kasi ndani
ya kichwa changu.
Kila kitu kilikuwa kikitokea kwa kasi
kubwa ambayo ungeweza kudhani ni ndoto ya kusisimua na muda si mrefu
nitazinduka. Kwa kuwa Junaitha aliniambia nikamsubiri chumbani kwake, sikukaa
muda mrefu ndani ya chumba hicho cha Shenaiza kwa sababu nilijua hawezi
kufurahi akinikuta nikifanya tofauti na maagizo aliyonipa, nikambusu Shenaiza
kwenye paji la uso kisha nikatoka na kuelekea chumbani kwa Junaitha.
Maisha aliyokuwa akiishi mwanamke huyu
yalikuwa na tofauti kubwa kati ya nje na ndani. Wakati kwa nje ungeweza kudhani
Junaitha ni mwanamke ‘mayai’ anayependa sterehe na anasa, ndani ya nafsi yake
alikuwa mtu mwingine kabisa. Nikaingia ndani ya chumba chake kilichojaa vitu
vingi vya kisasa, tena vyote vya thamani kubwa na kwenda kukaa kwenye sofa dogo
lililokuwa pembeni ya kitanda.
Japokuwa kimwili nilikuwa hapo lakini
kiakili nilikuwa mbali sana. Nilianza kujiuliza kwamba yale yote yaliyokuwa
yananitokea, yalikuwa na maana gani hasa? Nilifikia hatua hiyo baada ya kuona
ni kama naishi kwenye ‘script’ fulani ambayo tayari maisha yangu yameshapangwa
kwamba ni lazima nipitie hatua moja hadi nyingine kuelekea nisikokujua.
Hata mtu mwingine yeyote angeweza kufikiria
hivyo kwa sababu kabla ya mfululizo wa mambo yote hayo, nilikuwa nikiishi
maisha ya kawaida kabisa, nikifanya kazi kwa bidii nikiwa na ndoto nyingi
maishani. Nilikuwa nikiishi kama kijana wa kisasa anavyotakiwa kuishi lakini
kila kitu kilibadilika baada ya kukutana na Shenaiza.
Yaani ni kama nilikuwa nimelala na
asubuhi kulipopambazuka kila kitu maishani mwangu kilikuwa kimebadilika.
Nilimfikiria Raya na jinsi tulivyokuwa tukiishi naye kabla mambo hayajaanza
kwenda mrama, nikamfikiria Shamila nilivyokutana naye nikiwa hospitalini na
jinsi alivyotokea kunipenda na yote yaliyotokea mpaka muda huo ambao sasa
nilikuwa kwenye himaya ya Junaitha, mwanamke ambaye hata sijui nimuelezee vipi.
Nilizinduka kutoka kwenye lindi la
mawazo baada ya kusikia mlango ukifunguliwa, Junaitha akaingia huku akionesha
kuchoka sana, nikamuona akiufunga mlango kwa funguo kisha akanisogelea pale
nilipokuwa nimekaa.
“Nimechoka sana mume wangu,” alisema na
kunibusu mdomoni, nikabaki nimeduwaa. Niliduwaa kwanza kwa kitendo chake cha kuniita
‘mume wangu’ kwa sababu kiumri alikuwa sawa na mama yangu mdogo au shangazi
yangu lakini pia alinibusu mdomoni, miongoni mwa mambo ambayo yalikuwa
yakiufanya mwili wake uwe kama umepigwa na shoti ya umeme.
“Yaani wewe pamoja na yote haya
tuliyoyafanya pamoja bado tu hunizoei?” alisema baada ya kugundua kwamba
nilikuwa nimepigwa na butwaa, nikajichekesha na kuvunga. Kiukweli baada ya
kuuona upande wa pili wa Junaitha, nilikuwa hata sielewi mwanamke huyo ni mtu
wa aina gani.
Kuna wakati hata nilikuwa nahisi kwamba
hata kitendo cha mimi kujikuta nikifanya mapenzi na mwanamke huyo kilikuwa cha
hatari sana kwa sababu kumbe alikuwa na uwezo mkubwa mno wa nguvu zisizoonekana
kwa macho.
Kumbukumbu za tukio lililotokea muda
mfupi uliopita la kumkamata yule mwanamke kichawi na kufanikiwa kumleta mle
ndani, huku pia tukifanikiwa kulikimbia joka kubwa la kutisha katika ule
ulimwengu wa giza, ziliufanya moyo wangu uwe na hofu kubwa mno.
“Leo umenifurahisha sana kwa sababu
tumefanya kazi mbili kubwa ambazo zinatumia nguvu kubwa lakini katika zote,
wewe ndiyo umekuwa kama steringi, si unaona wenzako hakuna aliyezinduka hata
mmoja wakati hakuna kazi yoyote ya maana waliyoifanya?” alisema Junaitha huku
akifungua vifungo vya blauzi yake na kuanza kuivua.
Wala hakuwa na wasiwasi wowote au
hakuhisi aibu yoyote licha ya mimi kuwepo pale, akaivua na kuitupia kwenye kapu
la nguo chafu, akabaki kifua wazi.
“Mbona unaniangalia hivyo wakati mimi
nakusemesha mambo ya maana,” alisema huku akiachia tabasamu baada ya kugundua
kuwa akili na mwili wangu havikuwa kwenye ushirikiano mzuri.
“Unajua mimi nina dharau sana kwa
wanaume lakini sijui kwa sababu gani wewe nimetokea kukuamini na kukupenda
ndani ya muda mfupi namna hii,” alisema huku akianza kuvua za chini, akatoa
zote akiwa hana hata chembe ya wasiwasi, eti mimi ndiyo nikawa na kazi ya
kukwepesha macho yangu kwa aibu mpaka alipochukua upande wa khanga na
kujifunga.
“Hizi nguo ukishaenda nazo kule kwenye
ulimwengu mwingine hutakiwi kuzivaa tena mpaka zifuliwe kwa maji yenye udi,
mdalasini na karafuu, hebu acha ushamba wako,” alisema huku akinipiga
kimasihara begani, akanishika mkono na kunisimamisha, akaanza kufungua vifungo
vya shati langu.
“Si unaona unaelekea kupona, hebu sogea
hapa ujiangalie,” alisema huku akilitazama vizuri jeraha langu la kifuani,
nikasogea kwenye kioo na kujitazama. Ni kweli nilikuwa nimeanza kupona haraka
kuliko hata nilivyotegemea.
Jeraha ambalo nilikaa kwa muda mrefu
hospitalini lakini likawa bado hata haliponi, leo ndani ya saa chache tu
lilikuwa likielekea kupona! Ilikuwa ni zaidi ya maajabu kwangu.
“Na pale mguuni alipokujeruhi yule
mshenzi panaendeleaje?” alisema, nikataka nipandishe suruali juu ili nimuoneshe
lakini badala yake, alinipa taulo na kuniambia nivue tu suruali kwa sababu kuna
dawa nyingine alikuwa anataka tuitumie ili kutoa nuksi zote tulizotoka nazo
kule kwenye ulimwengu wa giza.
Kwa jinsi Junaitha alivyokuwa anajua
kunibembeleza kama mtoto mdogo, nilijikuta nikiishiwa na ile hofu iliyokuwa
ndani ya moyo wangu, nikawa nafanya kila kitu alichonigiza. Muda mfupi baadaye,
nilibaki na taulo tu, na yeye alibaki na upande wa khanga.
Akatembea kimikogo huku mwili wake
uliojengeka vizuri kikekike ukitingishika kwa namna ya kuvutia sana, akaenda
kufungua droo iliyokuwa pembeni ya kitanda, akatoa vichupa viwili vilivyokuwa na
vitu kama mafuta, akanisogelea.
“Hii dawa inabidi ukaogee na hii
ntakupaka tena kwenye kidonda chako, sawa baba’angu,” alisema huku akiwa
amenisogelea sana, tukajikuta tumekumbatiana tena, tukagusanisha ndimi zetu.
“Nataka suala la yote tunayofanya mimi
na wewe liwe siri yetu, umenielewa mume wangu,” alirudia tena kutamka neno
lile, safari hii kwa sauti iliyokuwa inasikika kwa mbali kama mtu
anayejilazimisha kuzungumza, nikaitikia kwa kutingisha kichwa, akanishika mkono
na kunipeleka kwenye bafu la ndani ambapo alinielekeza namna ya kuogea ile
dawa.
Cha ajabu, japokuwa yale mafuta hayakuwa
na rangi, nilipoyajaribu kunawia mikono tu kama alivyonielekeza mwenyewe,
nilishangaa mwili wangu ukitoa uchafu mwingi mweusi kama maji yaliyochanganywa
na mkaa, nikawa nashangaa kwa hofu.
“Ule ulimwengu mwingine una mambo mengi
machafu sana, usipojisafisha kwa hii dawa vizuri mwili mzima, unaweza kujikuta
unabadilika na kuwa kiumbe wa ajabu sana,” alisema na kunifanya nishtuke sana.
“Oga fastafasta nakusubiri,” alisema
huku akitoka na kuniacha bafuni, nikafanya kama alivyoniambia ambapo nilijipaka
ile dawa mwili mzima na kusogea kwenye bomba la mvua, nikafungulia maji ambayo
uchafu mwingi ulikuwa ukitiririka kutoka mwilini mwangu. Nilikaa kwenye maji
kwa zaidi ya dakika tatu ndiyo uchafu wote ukaisha, nikashangaa ule uchovu wote
niliokuwa nao umeyeyuka kama barafu juani.
Nikajifuta kwa taulo na kutoka mpaka
chumbani ambako nilimkuta Junaitha naye ameshaenda kuoga, nadhani alitumia bafu
la chumba kingine maana vyumba vingi ndani ya nyumba hiyo vilikuwa ‘self
contained’, akanipokea kwa mabusu motomoto na kunitaka nijilaze kidogo pale
kitandani kwake ‘tupunguze uchovu’.
Hata sijui nini kilitokea lakini muda
mfupi baadaye, wote tulikuwa kama tulivyoletwa duniani, tukaianza safari tamu
kwenye ulimwengu wa huba, ambayo lazima niwe mkweli, iliukonga mno moyo wangu,
nikajikuta nimepitiliza na kuuchapa usingizi mzito.
“Jamal! Jamal! Amka, kuna tatizo,” sauti
ya Junaitha ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye usingizi fofofo, nikakurupuka
nikiwana shauku kubwa ta kutaka kujua kumetokea nini tena.
Je, nini kitafuatia? Usikose Ijumaa
kwenye gazeti la Championi Ijumaa.
No comments:
Post a Comment