Monday, January 29, 2018

KIVURUGE WA TANDALE- 2



ILIPOISHIA:
Alimpungia mkono kichokozi huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, akatoka zake na kumuacha Ashrafu akiwa bado ameganda palepale kama barafu.
“Ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu,” alijisemea huku tabasamu hafifu likichanua kwenye uso wake, akashusha pumzi ndefu na kuinuka kuelekea kaunta kulipa.
SASA ENDELEA...
“USHALIPIWA na yule dada uliyekuwa umekaa nae,” alisema yule mhudumu aliyekuwa mapokezi.
“ooh! Ahsante,” alisema Ashrafu huku akijisikia aibu kupindukia. Kwa lugha nyepesi, alichokifanya mrembo yule ilikuwa sawa na matusi makubwa kwake, yaani akatae kumpa namba yake ya siku kisha akamlipie bili?
“Samahani, kwani wewe ni mwenyeji hapa,” Ashrafu alimuuliza yule mhudumu ambaye alikuwa bize kupokea fedha na kurudisha chenji kwa wateja wake.
“Kaka samahani, niko bize sana, naomba uniache nihudumie wateja.”
“Kwani ugomvi dada’angu? Nilitaka kukuuliza swali dogo tu.”

“Unasemaje?”
“Kuna kipindi nilikuwa mteja wenu mkubwa hapa lakini sijawahi kukuona, ndo maana nikakuuliza wewe hapa ni mgeni?”
“Kwa hiyo wewe kazi yako ukija hapa ni kuchunguza kama kuna wafanyakazi wageni na siyo kuja kula kama wateja wengine?”
“Eeh! Dada basi yaishe, hata hivyo hilo halikuwa swali langu, ishu ya msingi nilitaka kujua huyu dada unayesema amenilipia, ni mteja wenu wa kila siku?”
“Nyoo! Nilijua tu ndicho kilichokuleta hapa, mwanaume una tabia mbaya wewe sijapata kuona. Hivi unafikiri hicho unachokifanya ni ujanja?” alisema yule dada kwa sauti ya juu, nikaona nikiendelea kujibizana naye anaweza kunidhalilisha maana watu walishaanza kututupia macho, wakitaka kujua nini kinaendelea. Niliondoka nikiwa nimetahayari, uso wangu nikauinamisha chini huku nikijiapiza kwamba sitarudi tena kula kwenye kantini hiyo.
Kwa ilivyoonesha, hiyo ilikuwa siku mbaya sana kwangu kwani matukio mawili ya udhalilishaji mkubwa yalikuwa yamenitokea, tena mfululizo, kibaya zaidi kutoka kwa wanawake wawili warembo sana.
Hakuna kitu ambacho kilikuwa kinanikasirisha kama mwanamke mrembo kunidharau, hakukuwa na sababu yoyote ya mimi kudharaulika, hasa ukizingatia kwamba nilikuwa na historia nzuri ya kumfanya mwanamke yeyote mrembo anipende, na si kunipenda tu bali aoze kabisa kwangu na siku zote sikuwa nikifanya ajizi linapokuja suala la malavidavi na watoto wazuri.
“Julieth mtoto wa masaki ananiheshimu, tena mtoto kwao mambo safi kwelikweli, inakuwaje ‘cashier’ wa kwenye kantini ya kishamba kama hii anidharau? Inakuwaje mdada anayefanya kazi kwenye kampuni ya kuuza vifaa vya solar anidharau mpaka eti anilipie msosi wa buku mbili jero?” nilijisemea huku nikitembea kinyonge kurudi ofisini.
Nilipanda ngazi kinyonge huku nikiendelea kujiuliza kauli nzito zilizotolewa na yule dada mhudumu pale kantini. Kiukweli sikuwa namjua lakini yeye ilionesha wazi kwamba ananijua, na pia anajua mambo mengi kuhusu mimi.
Nilijiuliza, hata kama ananijua kwani kosa langu mimi ni nini? Kwa nini awe mkali kwangu kiasi kile wakati niliyekuwa namuulizia ni mteja tu kama mimi? Uamuzi nilioufikia, ilikuwa ni kumtafuta baada ya muda wa kazi tuzungumze, anieleze kisa mkasa ni nini? Sikuzoea kuishi na vinyongo.
Nilipanda ngazi mpaka ghorofa ya tatu, ilipokuwa sehemu yangu ya kufanyia kazi. Ile naingia tu, dada wa mapokezi alinifuata.
“Ulikuwa wapi, bosi alikuwa anakutafuta halafu nakupigia simu hupatikani, lakini unakuwaje wewe?”
“Aah, sasa dada Salma kwani ugomvi? Mbona umekasirika namna hiyo?”
“Ndiyo! We unaona unachokifanya ni kizuri? Mimi nafokewa kwa ajili yako? Na kwa nini hupatikani hewani wakati simu yako hujaizima?” alisema Salma ambaye kihaiba ni mzuri sana lakini tatizo lake moja kubwa, ni kisirani sana. Yaani muwa wote ukimkuta ana ‘stress’ za kutosha, uso umekunja ndita mpaka ule urembo wake asili hauonekani. Tabia yake hiyo ilikuwa ikisababisha akorofishane sana na bosi wetu, Isabella Kishimba au Madam Bella kama wenyewe tulivyozoea kumuita.
Nikiwa najiuliza nijitetee nini, aliichukua simu yangu kwa nguvu kutoka mikononi mwangu, kwa kuwa nilikuwa nimetoka kuifungua password muda huohuo, alifanikiwa kuingia sehemu ya kupigia simu, nikawa namtazama nikiwa sijui cha kufanya.
Akabonyeza namba fulani kisha nikaona anaiweka simu sikioni, nikahisi labda anampigia simu bosi kumwambia kwamba amesharudi. Sasa kwa nini afanye hivyo? Kwa nini asipige kupitia simu ya mezani? Nilijiuliza maswali yaliyokosa majibu.
Ilita kidogo halafu akaikata, akanitazama huku akiwa bado amekunja sura yake nzuri ya mviringo.
“Nenda kwa bosi, alisema ukija tu ukamuone,” alisema, akaiweka ile simu yangu kwenye meza yangu kisha akageuka na kuanza kutembea harakaharaka, viatu virefu alivyokuwa amevaa, sketi fupi ya kike iliyoishia juu kidogo ya magoti na blauzi nyeupe aliyokuwa ameivaa, vilimfanya azidi kuwa mrembo, hasa ukimtazama kutokea nyuma.
Alitembea harakaharaka huku akitingishika mwili mzima, nikajikuta nimeganda namtazama, alipofika hatua kadhaa aligeuka na katika hali ambayo sikuitegemea, alinibamba nikiwa namuangalia, nikakwepesha macho yangu haraka na kuzuga na kikohozi cha uongo, akaachia msonyo na kuingia ofisini kwake.
“Hivi hii siku ya leo nimeamkaje jamani? Kila mtu ananichukia na kunifanyia vituko, sijui huyo bosi naye ataenda kunifokea kama kawaida yake maana daah! Mabosi wa kike wanakuwa wanoko sana,” nilijisemea huku nikisimama, kabla sijaanza safari ya kuelekea ofisini kwa bosi, ghorofa ya tatu, nilipata wazo la kuitazama vizuri simu yangu.
Nilitaka kujua Salma alimpigia simu nani na kwa nini alitumia simu yangu? Nilipofungua simu, nilikutana na namba ngeni, nikaitazama kwa makini lakini sikuweza kuikumbuka.
Miongoni mwa kasoro nilizonazo, huwa siwezi kabisa kukariri namba ya mtu ya simu kichwani. Hata hiyo namba yangu yenyewe ilikuwa mtu akiniuliza, lazima nianze kwanza kupekua simu mpaka mahali nilipoisevu ndiyo naitaja.
Ili isinichanganye hata huyo aliyempigia atakaponipigia tena, niliamua kuisevu Salma Kisirani. Basi nikapanda mpaka ofisini kwa bosi huku nikijishtukia mwenyewe, moyoni nikawa naandaa majibu ‘nilienda kula mara moja bosi, si unajua huu ni muda wa lunch?’
Niliingia ofisini kwenye ofisi yake ya kisasa na tofauti na siku zote ambapo huwa anakaa kwenyekiti chake cha kuzunguka, leo hii alikuwa amekaa kwenye masofa ya wageni, tena amekaa amejiachia kwelikweli maana viatu alikuwa amevivua na kupandisha miguu juu.
“Shikamoo Madam!”
“Mh! Yaani wewe kila ukiniona shikamoo shikamoo, unajua maana ya shikamoo wewe?” alisema huku akitabasamu, tofauti kabisa na anavyokuaga siku zote, basi nikawa najiumauma, akanionesha kwa ishara kwamba nisogee na kukaa kwenye sofa lililokuwa jirani na pale alipokaa.
“Nimeambiwa unaniita bosi.”
“Ndiyo, nimekuita maana najihisi upweke sana, nataka mtu wa kunipigisha stori walau nicheke,” alisema Madam Bella huku akiinuka na kukaa vizuri pale kwenye sofa lake.
 Katika hali ambayo sikuitegemea, kwa kuwa alikuwa amevaa sketi fupi na upande aliokuwa akigeukia ndipo nilipokuwa nimekaa mimi, nilijikuta nimeiona kufuli nyeupe aliyokuwa ameivaa, japokuwa kiumri Madam Bella alikuwa ameniacha kama miaka kumi hivi, kitendo kile kilinifanya nisisimke mno, nikameza mate kama fisi aliyeona mfupa, kumbe mwenyewe alikuwa akinitazama usoni aone ‘nita-react’ vipi, aliponiona ninavyomeza mate akacheeeka!
“Nasikia sifa zako jinsi unavyowachangamkia mabinti huko kwenu Tandale, nasikia wanakuita Kivuruge jinsi unavyowavuruga, kama kweli we kidume mbona mimi hujawahi kunitongoza hata mara moja?” bosi alizungumza kauli ambayo sikuwahi kutegemea inaweza kutoka kwenye kinywa chake hata mara moja.
“Unataka nikutongoze ukinifukuza kazi je?” nilijitutumua kiume, akazidi kucheka mpaka akanipa mkono tugonge. Nilishangaa sana maana haikuwa kawaida yake, nikawa najiuliza amepatwa na nini?
“Siwezi bwana, nikufukuze kazi kwani nani amekwambia kutongozana kunahusiana na kazi? By the way hata mimi ni mwanamke, nina hisia kama wanawake wengine, siyo kwa sababu ya ubosi basi uniogope kiasi hicho,” alisema huku akiinuka, akanipiga kakofi begani kisha nikamuona akielekea maliwatoni, nikakaa vizuri pale kwenyekiti maana ‘Ashrafu’ wangu naye alishaanza kuonesha tabia mbaya mbele ya bosi, kama nyau aliyeona samaki.
Hakukaa sana, akarudi na moja kwa moja alienda kufunga mlango kwa ndani, tena kwa funguo kabisa, akainua mkonga wa simu na kupiga upande wa pili, nadhani alipiga mapokezi, akazungumza kwa sauti ya chini ‘natoka kidogo’ akija mgeni yeyote mwambie anisubiri hapo mapokezi’ kisha akaja mpaka pale kwenye kochi nilipokuwa nimekaa huku mkononi akiwa ameshika kitu.
Mara alinirushia kitu hicho, nikashtuka baada ya kugundua kuwa lilikuwa ni lile kufuli lake jeupe, likiwa na harufu f’lan hivi ‘amaizing’ kuoneshakwamba lilikua limetoka mwilini muda huohuo, akacheka sana jinsi nilivyokuwa nalitazama kwa makini huku wakati mwingine nikilisogeza kabisa kwenye pua, akasogea na kujitupa kwenye sofa huku akiinua miguu yake na kuiweka kwenye miguu yangu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.

1 comment:

  1. Baada ya kuona chapisho kwenye mtandao la Jenna kutoka USA akisema jinsi alivyosaidiwa na Dk. DAWN, niliamua pia kuwasiliana naye kwa msaada kwa sababu sikuwa na chaguo nilichotaka ni kumrudisha mpenzi wangu na furaha. Kwa mshangao mkubwa mpenzi wangu alifika nyumbani akiwa amepiga magoti kwamba nitafute nafasi moyoni mwangu kumsamehe, hakika nilistaajabu na kushtuka mpenzi wangu alipopiga magoti akiomba msamaha na mimi nimkubalie tena. Kweli nimepungukiwa na maneno, na sijui ni kiasi gani cha kukushukuru wewe Dr. DAWN. Wewe ni Mungu aliyetumwa kurejesha uhusiano uliovunjika, Na sasa mimi ni mwanamke mwenye furaha. mawasiliano yake ni Whatsapp +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...