ILIPOISHIA:
Mara nikasikia mlango unafunguliwa, nikashtuka na
kuinuka haraka kutaka kutazama ni nani aliyekuwa akiingia, nikashtuka kumuona
Salma, mtoto wa kike akiwa ameingia kwenye vyoo vya wanaume, nilipomtazama
vizuri alikuwa akilia, machozi yakawa yameulowanisha uso wake.
SASA ENDELEA...
Harakaharaka
niliacha kila nilichokuwa nakifanya, nikalishika shati na kutaka kulivaa lakini
nilikuwa nimechelewa, Salma alifunga mlango wa maliwatoni kwa ndani kisha
akanisogelea mpaka mwilini, huku machozi yakiendelea kumtoka.
“Umepatwa na
nini Salma?”
“Kwa nini
unanitesa? Ina maana hujui kama nakupenda? Kwa nini unanitesa Ashrafu,” alisema
Salma huku akipitisha mkono wake na kunishika kiunoni, akanisogelea na kujilaza
kwenye kifua changu.