“Kumbe unajua kuimba vizuri hivyo, itabidi
nikupeleke studio,” nilimchombeza, akacheka sana, tayari tulishafika maana
konda alipaza sauti akisema hapo ndiyo mwisho wa gari, abiria wengine wakawa
wanateremka lakini mimi nikajikuta nikipata uzito na kubaki nimekaa, naye
hakuonesha kuwa na haraka sana, akawa amekaa akiwa ni kama anayenisubiri
niinuke ili na yeye ainuke.
Ndani ya muda mfupi tu tayari tulishakuwa
tumezoeana f’lani hivi, akili fulani ndani ya kichwa changu ikawa inaniambia
‘jaribu kutupia mistari’.
SASA ENDELEA...
“Twende
basi tushuke jamani,” alisema huku akinigusa begani, nikamgeukia nakumtazama,
safari hii tukiwa tumesogeleana sana maana alishaanza kuinuka.
“Mbona
unaniangalia hivyo mpaka mwenzako najisikia aibu,” alisema huku akijichekesha,
nikaona huo ndiyo muda mzuri wa kutekeleza kile ambacho akili yangu ilikuwa
ikinituma sana.
“Wewe ni
mzuri sana, hivi mumeo huwa anakusifia kila siku kabla hujatoka nyumbani?”
nilimwambia, akacheka kwa nguvu na kwa kuwa abiria wote walikuwa bize kuteremka
kwenye gari, hakuna aliyemjali sana, nikasimama, na yeye akasimama kwani tayari
abiria walikuwa wamepungua sana ndani ya gari.
“Umejuaje
kama nina mume?” aliniambia huku akinitazama kwa macho ya bashasha.
“Mwanamke
mrembo kama wewe utakosaje mume?” nilizidi kumchombeza, akazidi kufurahi.
Miongoni mwa udhaifu mkubwa wa wanawake, huwa wanapenda sana kusifiwa na
wajanja kama sisi tunaojua namna ya kuzifikisha hizo sifa zenyewe kwa staili ya
kuchombeza, huwa inakuwa rahisi sana kuwanasa.
Hata
mwanamke aweje, ukishaanza kumsifia tu, lazima atafurahi, hicho ndicho
kilichotokea kwa mwanamke huyu ambaye kama nilivyoeleza, sikuwahi kumuona
sehemu yoyote na asubuhi hiyo ndiyo kwanza tulikuwa tumekutana.
Niliposimama,
nilitumia ujanja wa kiume wa kumpisha yeye ndiyo atangulie mbele, lengo langu
lilikuwa ni kutaka kumtazama vizuri, hasa kwenye ‘plate numbe’ ambao kiukweli
umekuwa ugonjwa sugu unaonisumbua.
Nilijikuta
nikijishika mdomo kwa mshangao, kwa kuwa muda wote alikuwa amekaa wala sikuweza
kumuona yupoje akisimama lakini kumbe alikuwa na umbo ambalo hakuna mwanaume
yeyote aliyekamilika anayeweza kupishana naye halafu asigeuke!
Alikuwa
amejaaliwa haswaa, nikazidi kuchanganyikiwa na ile nadhiri niliyokuwa
nimejiwekea, ya kukaa mbali na mali za watu ikayeyuka kama bonge la mafuta
kwenye kikaango.
“Dah!
Shemeji atakuwa anafaidi kinoma, kumbe ndiyo umeumbika kiasi hicho,”
nilimchombeza wakati akimalizia kushuka ngazi ya mwisho ya gari, alipokanyaga
chini, ule mtikisiko ukasababisha ‘msambwanda’ nao utingishike kwa namna iliyoyapa
raha ya kipekee macho yangu.
Alicheka
na kunigeukia, akanipiga kakibao kepesi begani, tukawa tunatazama huku aibu za
kikekike zikiwa zimemjaa usoni.
“Wewe
umeniuliza mimi jina, mbona wewe hujaniambia unaitwa nani?”
“Hujaniuliza!
Kwani unataka kunijua?” aliniuliza huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye
uso wake. Nilichokigundua ni kwamba alikuwa anapenda sana kucheka na kufurahi
na katika kipengele hicho, Mungu alikuwa amenipa kipaji cha aina yake maana
usingeweza kukaa na mimi halafu usitabasamu au kucheka.
Basi
aliniambia kwamba anaitwa Ruqaiya au mama Abdul, akaniambia kwamba anasimamia
maduka mawili ya simu ya mumewe yaliyopo mtaa wa Aggrey Kariakoo na kwamba muda
huo ndiyo alikuwa akienda kazini.
Sikupoteza
muda, nilimwambia mimi ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta lakini pia nilikuwa
na ujuzi wa ‘kuzi-program’ simu, hasa hizi za kisasa zinapotoka kiwandani,
akafurahi sana na kuniambia kwamba eti kukutana kwetu ulikuwa ni mpango wa
Mungu.
“Naomba
namba yako basi bosi!” nilimwambia, akawa mjanja katika hilo, akaniambia kwamba
mimi nimtajie ya kwangu halafu yeye atanipigia.
Mbinu hii
huwa inatumiwa sana na wanawake wajanja ambapo badala ya kukukatalia kukupa
namba, anakwambia wewe ndiyo umpe halafu anazuga kama anaiandika kwenye simu,
ukimpa mgongo tu anaifuta na huwezi kumpata tena, hasa katika mazingira kama
yale niliyokutana nayo.
Nilimtajia
namba yangu, akaiandika kwenye simu yake kisha akaniaga juu kwa juu huku
akionesha kuwa na furaha sana, nilishindwa nifanye nini, nikawa namsindikiza kwa
macho akitembea kwa maringo.
Alipopotea
kabisa kwenye upeo wa macho yangu, harakaharaka na mimi niliendelea na hamsini
zangu, nikakata mitaa na muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nimewasili kazini,
nikapanda ngazi mpaka juu, wa kwanza kukutana naye alikuwa ni Salma.
Ofisi yetu
jinsi ilivyo, unapoingia lazima upitie kwamba mapokezi kusaini kitabu cha
mahudhurio kwa hiyo hakukuwa na namna ambayo ningeweza kumkwepa Salma.
Aliponiona tu, alinitazama huku tabasamu pana likichanua kwenye uso wake, jambo
ambalo siyo kawaida yake.
Kama
nilivyoeleza awali, Salma alikuwa na sifa moja kubwa ya kununa muda mwingi na
kutoa majibu ya hovyo kwa mtu yeyote hata pale unapomuuliza mambo muhimu ya
kikazi.
“Mambo!”
nilimsabahi huku na mimi nikijitahidi kuvaa tabasamu la uongo usoni. Hakunijibu
zaidi ya kuendelea kujichekeshachekesha mwenyewe pale kwenye kiti cha kuzunguka
alichokuwa amekalia.
Nilipomaliza
kusaini, wakati nataka kwenda ofisini kwangu kuendelea na majukumu yangu,
aliniita kwa jina langu halisi, nikamgeukia maana tayri nilishampa kisogo.
“Kwa hiyo
unadhani ukipokea simu zangu nitanenepa sana au?” alisema huku akitoa bahasha
kubwa aliyokuwa ameiweka chini ya meza yake. Nikiwa bado sijui nimjibu nini,
alinikabidhi na kuniambia kwamba eti hiyo ni zawadi yangu, nikatabasamu na
kumshukuru huku nikiwa na shauku ya kutaka kujua ndani yake kuna nini.
“Na ole
wako usiwe unapokea tena simu zangu,” alisema huku akionesha dhahiri jinsi
alivyokuwa na furaha ndani ya moyo wake.
Niliingia
ofisini na kitu cha kwanza ilikuwa ni kufungua bahasha hiyo, nikajikuta
natabasamu mwenyewe kwa furaha, alikuwa ameninunulia zawadi ya ‘boksa’ za kiume
nzuri, ambazo eti alikuwa amezipulizia pafyumu yake anayojipulizia kila siku.
Nilichukua
simu yangu na kumtumia meseji ya kumshukuru, hakujibu kwa wakati, ikabidi
nianze kazi kwa sababu nilikuwa na majukumu mengi siku hiyo. Kuna kompyuta
kadhaa za ofisi zilikuwa na matatizo na ilikuwa ni lazima nizitengeneze asubuhi
hiyo ili kazi ziendelee.
Mara simu
yangu ya mkononi ilianza kuita, kutazama namba ya mpigaji, nilishtuka kidogo
baada ya kugundua kwamba ni bosi ndiyo alikuwa akinipigia, harakaharaka
nikapokea.
“Shikamoo
bosi,” nilimsalimia kwa adabu.
“Si
nishakwambia hizo shikamoo zako sizitaki, una udogo gani wa kunipa shikamoo,
unataka kunizeesha bure! Njoo ofisini kwangu haraka,” alisema Madam Bella kisha
akakata simu. Harakaharaka nikaacha kila nilichokuwa nakifanya na kutoka
kuelekea ofisini kwake.
Nilipoingia
ofisini kwake, Madam Bella aliinuka kutoka pale alipokuwa amekaa na kuja
mwilini, akanikumbatia kwa hisia huku akinibusubusu sehemu mbalimbali za mwili
wangu.
“Ndiyo
nini ulichonifanya jana? Yaani nimekuja kuzinduka saa moja jioni, najikuta
nimebaki peke yangu ofisini,” alisema huku akiachia tabasamu pana, akanibusu
tena mdomoni, safari hii kwa hisia kali zaidi.
“Leo
sitaki ufanye kazi yoyote, kajiandae kuna mahali nataka twende tukapumzike,”
alisema huku akinitazama kwa macho yaliyokuwa yamebeba hisia nzito za
kimapenzi, nikajua kazi ninayo maana ukweli ni kwamba sikuwa nimepumzika hata
kidogo tangu jana yake.
Nilimkubalia,
nikatoka kwa lengo la kurudi ofisini kwangu kuweka vitu sawa kwa sababu tayari
ilishaonekana hakuna kazi itakayofanyika tena, ile natoka kumbe Salma alikuwa
amenifuata ofisini kwangu na kunikosa, tukakutana kwenye korido.
“Zawadi
yangu hujaipenda?”
‘Kwa nini
unasema hivyo Salma jamani, nimeipenda na nimekutumia meseji kukushukuru.”
“Muongo,
halafu hata kama hujaipenda, ndiyo uiache juu ya meza jamani, yaani unataka
nani aione? Sawa nashukuru sana Ashrafu, ahsante sana,”alisema huku akianza
kulengwalengwa na machozi, ghafla macho yake yakatua kwenye shingo yangu.
“Mh! Hii
lipstiki imetoka wapi? Halafu mbona kama unanukia pafyumu ya...” kabla hata
hajamalizia alichotaka kukisema, wote tulishtuka baada ya kusikia mlango wa bosi
ukifunguliwa, macho yake yakatua moja kwa moja kwangu mimi na Salma aliyekuwa
akiendelea kunikagua pale kwenye korido.
Madam
Bella hakusema lolote zaidi ya kusimama, akawa anatutazama huku akionesha
kushtuka sana kutokana na hali aliyotukuta maana Salma alikuwa amepeleka mkono
wake shingoni kwangu kwa lengo la kunikagua ile aliyosema mwenyewe lipstiki,
kwa hiyo mazingira yalionesha ni kama tulikuwa tumekumbatiana.
Je, nini
kitafuatia? Usikose Jumamosi kwenye Risasi Jumamosi.
No comments:
Post a Comment