Kuongezeka kwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
kwa vijana na wanaume kumesababisha wengi kuhaha huku na kule kutafuta madawa
makali ya kutibu tatizo hilo.
Dawa nyingi za hospitali ambazo hutumika kumaliza au
kupunguza tatizo hili, zimebainika kuwa na madhara (side effects) hivyo
kusababisha wataalamu kuanza kuhangaika kugundua tiba kwa njia ya vyakula.
CHANZO
CHA TATIZO
Tatizo la upungufu wa kiume mara nyingi husababishwa
na matatizo ya kimwili au ya kisaikolojia ambapo mwanaume huwa dhaifu wakati wa
tendo na wakati mwingine kushindwa kabisa kufanya chochote.
Sababu za kimwili (Physical) zinaweza kuwa ni kwa
sababu mishipa ya damu inashindwa kufikisha damu yenye msukumo kwenye viungo
vya uzazi.
Kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini
husababisha mafuta hayo kuganda kwenye kuta za mishipa ya damu na kuzuia damu
kutiririka vizuri, tatizo ambalo kitaalamu huitwa atherosclerosis.
Pia wagonjwa wa kisukari nao wapo kwenye hatari
kubwa ya kukumbwa na tatizo hili. Upungufu wa madini ya Zinc na vitamin pia
husababisha tatizo hili.
Sababu za kisaikolojia ni pamoja na kuwa na msongo
wa mawazo, hofu, uchovu wa akili au kama mtu aliwahi kukumbwa na tatizo kubwa
siku za nyuma ambalo limemuathiri kisaikolojia au kama ana dosari katika mfumo
wake wa homoni.
Sababu nyingine zinazoweza kusababisha tatizo hili
ni matumizi ya madawa ya kulevya, pombe au kuchanganya vyote viwili kwa pamoja.
Uvutaji wa sigara nao ni sababu nyingine ya tatizo hili, pamoja na kuendesha
baiskeli kwa muda mrefu.
VYAKULA
VINAVYOSAIDIA KUMALIZA TATIZO
Vyakula ambavyo vimethibitishwa kitaalamu kwamba
vina uwezo wa kumuongezea mwanaume nguvu za kiume ni pamoja na:
1.
Vitunguu swaumu
Vitunguu hivi vinaelezwa kuwa na kirutubisho
kiitwacho allicin ambacho huongeza msukumo wa damu kuelekea kwenye viungo vya
uzazi.
2.
Ndizi mbivu
Inaelezwa kuwa ndizi mbivu zina kirutubisho
kiitwacho bromelain ambacho husaidia kuupa mwili nguvu wakati wa tendo,
kuongeza msukumo wa damu kwenye viungo vya uzazi na kuongeza hamu ya kufanya
tendo. Pia ndizi zina Vitamin B ambayo huupa mwili nguvu.
3.
Karanga
Mbali na kuwa na mafuta mengi, karanga zina
virutubisho viwili muhimu, Amino Acid na L-Arginine ambavyo humuongezea
mwanaume nguvu wakati wa tendo na kuchochea uzalishwaji wa mbegu za kiume na
kuongeza hamu ya tendo.
4. Chocolate
Chocolate zina vichocheo vya phenylethylamine na
alkaloid ambavyo huongeza mhemko wakati wa tendo. Pia huongeza nguvu kwa
wanaume hivyo kuleta ufanisi wakati wa kufanya mapenzi.
5. Kunazi (Blueberries)
Haya ni matunda madogomdogo jamii ya zabibu ambayo
huliwa na binadamu. Matunda haya yanaelezwa kuwa na nguvu kama ilivyo dawa ya
Viagra. Tafiti za kitaalamu zinaeleza kuwa matunda haya yana vichocheo ambayo
hulaainisha mishipa ya damu na kufanya damu isambae kwa kasi kuelekea kwenye
viungo vya kiume.
Pia matunda haya yana kambalishe (fiber) ambayo
huyeyusha lehemu (cholesterol) kwenye mishipa ya damu na kuitoa nje ya mwili
kabla haijaleta madhara kwa binadamu hivyo kuongeza ufanisi wakati wa tendo.
6. Pilipili
Pilipili zinao uwezo mkubwa wakumaliza tatizo hili.
Unaweza kuchanganya kwenye chakula au ukala hivyohivyo kwa kutafuna kiasi
kidogo mara kwa mara. Pilipili zina virutubisho ambavyo husaidia kuufanya mzunguko
wa damu uwe mkubwa na kuamsha hisia kali za mapenzi.
7. Pweza na chaza
Aina hizi za viumbe wa baharini, huwa na madini ya
zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinavyohamasisha
msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa. Jenga utaratibu wa kunywa supu ya
pweza mara kwa mara na matokeo yake utayaona.
8. Parachichi
Parachichi lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E
ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume. Inatajwa kuwa watu
wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkubwa wa kimapenzi.
8. Tikitimaji
Matunda haya pia yana uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu
za kiume. Wengi hufanya makossa wanapokula matunda haya kwa kutema mbegu zake.
Tikiti linapaswa kuliwa pamoja na mbegu zake, angalau vipande viwili au vitatu
kwa siku.
9. Maji
Maji safi ya kunywa, yanatajwa pia kuwa na uwezo
mkubwa wa kusafisha mwili, hasa mfumo wa uzazi na kukupa nguvu za kufanya tendo
la ndoa. Unapaswa kunywa maji kwa wingi lakini pia, kila mkojo unapokubana, ni
muhimu kwenda kuutoa kwani kukaa na mkojo kwa muda mrefu, husababisha baadhi ya
misuli ambayo ni muhimu kwenye tendo, kulegea.
10. Komamanga
Haya ni aina fulani ya matunda, ambayo ndani yana
mbegu nyekundu. Komamanga linatajwa kuwa na virutubisho muhimu vya kusisimua
misuli na kuamsha hisia za kushiriki tendo la ndoa.
11. Mvinyo mwekundu
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa
kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu
uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa. Pia unatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa
kuamsha hisia baada ya kumaliza raundi ya kwanza ya tendo la ndoa.
12. Mbegu za maboga
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali, hasa za maboga huongeza
nguvu na ufanisi wa kufanya tendo la ndoa.
Nimeenjoy na elimu yako nzuri aiseeee,Kuna siku nilikunywa Tanzania kinyagi mizinga midogo mbili ya 4000 nikimix na soda Aina ya Fanta manzee mashine haikusimama na ikisimama inakuwa legelege,ndo maana ikabidi nitembelee hii page nipate maarifa sbb hii Hali haikuwwa ya kawaida kwangu,Tangia siku hiyo nazichukia pombe Kali walai
ReplyDelete