ILIPOISHIA:
“Chukua taulo pale kabatini ingia bafuni
ukaoge,” alisema akiwa amekaa juu ya kitanda kikubwa cha kisasa akihangaika
kufungua zipu ya gauni alilokuwa amevaa, nikaelekea pale kwenye kabati
aliponielekeza, nikachukua taulo na kuanza kuelekea kwenye lile bafu la ndani
kwa ndani kule chumbani kwake.
Nililazimika kuingia na nguo zote bafuni kwani
nilikuwa naona aibu kuvua hata shati mbele ya macho yake.
SASA ENDELEA...
“Sasa utaingiaje bafuni na nguo? Hebu toa
ushamba wako hapa,” alisema Junaitha huku akicheka, nikajikuta nikiwa kwenye
wakati mgumu sana. Japokuwa nilikuwa nimeshaingia, ilibidi nitoke, nikajikaza
kisabuni na kuvua fulana niliyokuwa nimeivaa, bandeji iliyofungwa juu ya jeraha
langu ikaonekana vizuri.
“Mh! Kumbe uliumia kiasi hicho, hebu njoo
nikuangalie,” alisema, nikavungavunga kwa aibu mwishowe nikasogea mpaka pale
kitandani alipokuwa amekaa. Akanisogelea na kuanza kunitazama vizuri pale
kifuani.
“Unajisikiaje kwani?” aliniuliza huku
akiligusa jeraha langu kwa juujuu.
“Sasa hivi nina afadhali kubwa,” nilimjibu,
akaendelea kulitazama jeraha hilo kwa muda kisha akaniambia nisiwe na wasiwasi,
kuna dawa atanipaka ambayo itanifanya nipone haraka kuliko kawaida, niliitikia
kwa kutingisha kichwa.
“Halafu mbona kama unaniogopa? Kwani nina
tofauti gani na hao wanawake zako unaotoka nao? Au unaniona mimi mzee?” alisema
huku mkono wake mmoja akiwa amenishika shingoni kwa upole. Kiukweli nilikuwa
najisikia aibu sana kiasi kwamba sikuweza hata kumtazama usoni.
“Haya malizia kuvua nguo zako ukaoge na mimi
nataka kuoga,” alisema huku akiniachia, nikashusha pumzi ndefu na kusogea
pembeni ambapo niligeukia pembeni, nikalifunga lile taulo juu ya suruali kisha
nikavua juu kwa juu, nikamsikia akiangua kicheko kutokana na ujanja
nilioutumia.
“Mbona mimi sijishtukii kama wewe? Hebu
niangalie,” alisema, nikageuka na kumtazama, nikamuona akilishusha gauni lake
kwa maringo ya kikekike, macho yangu yakatua kwenye kifua chake, japokuwa
alikuwa mtu mzima, alikuwa na kifua kama kigori. ‘Braa’ ya rangi ya zambarau
iliyahifadhi vizuri maembe bolibo mawili yaliyokuwa yamejaa vizuri kama mtu
ambaye hajawahi hata kuwa na mtoto.
Nikiwa bado nimepigwa na butwaa, nilimuona
akimalizia kulitoa gauni lake lote, nilichokiona kilinifanya nipoteze ‘network’
kwa sekunde kadhaa, akaifungua na ile ‘braa’ aliyokuwa ameivaa, akabakia na
nguo ya mwisho tu, mapigo ya moyo wangu yakawa yananienda mbio kuliko kawaida,
nikameza funda la mate kama fisi aliyeona mfupa.
Japokuwa kwa nje alikuwa akionekana kama mtu
mzima flani hivi, ndani Junaitha alikuwa tofauti kabisa, kwa makusudi kabisa
akageuka kama anayetafuta kitu fulani, macho yangu yakatua kwenye mlima mkubwa
uliokuwa upande wa nyuma, nikashusha pumzi ndefu huku kijasho chembamba
kikianza kunitoka.
Ni kama alishaona kwamba ndege mjanja nimenasa
kwenye tundu bovu kwani alisimama na kuanza kutembea kama wanamitindo
wanavyotembea jukwaani, akanisogelea mpaka pale nilipokuwa nimesimama,
akaipitisha mikono yake nyuma ya shingo yangu, tukagusanisha ndimi huku mikono
yangu ikiwa bado haijui ishike wapi.
“Sitaki uniogope, mimi ndiyo mtu sahihi
unayepaswa kuwa naye, nitakulinda na kukuepusha na matatizo yote unayoweza
kuyapata kwa kubadili wanawake ovyo,” alisema kwa sauti ya kunong’ona, mdomo
wake ukiwa sentimita chache kutoka kwenye sikio langu, sauti yake ikapenya hadi
kwenye ngoma zangu na kuniongezea msisimko wa kipekee.
Nikajikuta mikono yangu imeenda kushikilia
mlima wake, nikashtushwa na jinsi alivyokuwa na ngozi laini, nikamuona naye
akishtuka kidogo kisha akaachia tabasamu pana, akaniachia shingoni na kunishika
mkono, akawa ananivuta kama kondoo anayepelekwa machinjioni, nikawa namfuata,
safari yetu ikaishia kwenye kitanda kikubwa cha kifahari.
Sikuelewa kilichoendelea mpaka nilipokuja
kushtuka muda mfupi baadaye na kujikuta nikiwa kama nilivyokuja duniani, naye
akiwa katika hali hiyohiyo, ‘Jamal’ wangu akiwa amechachamaa kupita kawaida.
Kilichoendelea baada ya hapo, ilikuwa ni ‘experience’ nyingine mpya kabisa
maishani mwangu.
Waliosema usidharau kitabu kwa kutazama kava
lake hawakukosea, japokuwa kwa mwonekano Junaitha alikuwa akionekana mtu mzima
flani hivi, alikuwa ‘fit’ mno, mpaka chombo kinatia nanga kwenye bahari ya huba
kuashiria kufika mwisho wa safari, nilikuwa sijitambui, ukichanganya na ule
uchovu wa kazi ya kumuokoa Shamila, nilijikuta nikipitiwa na usingizi mzito
ambao nikiri kuwa sijawahi kuupata tangu nizaliwe.
Nilikuja kuzinduka baadaye na kujikuta nikiwa
nimelala juu ya kitanda kilichotandikwa shuka jeupe na juu yake karatasi laini
la nailoni, nikiwa nimefungwa taulo kubwa jeupe huku Junaitha naye akiwa amevaa
nguo kama ya kulalia hivi, yenye rangi nyeupe.
Nilitaka kuinuka lakini akaniwahi na
kunituliza, akaniambia ananisafisha kidonda changu na kunipaka dawa kama
alivyoniambia, nikatulia. Nilimuona akichanganya dawa fulani kama mafuta hivi,
akaja kuinyunyiza juu ya ile bandeji, muda mfupi baadaye akaitoa taratibu. Wala
sikuhisi maumivu yoyote kama ilivyokuwa hospitali au wakati Shamila
akinisaidia.
“Ungechelewa sana kupona kwa dawa za
hospitali, inaonekana hili jeraha lilimaanishwa kuyakatisha maisha yako,”
alisema huku akinimwagia dawa nyingine juu ya jeraha langu na kuanza kunichua
taratibu, nikakosa cha kujibu zaidi ya kuwa namtazama tu usoni, kumbukumbu za
yote yaliyotokea zikirudi kwa kasi kichwani mwangu.
“Nisamehe kwa kutangulia kukudharau, kumbe
wewe siyo wa mchezomchezo,” alisema Junaitha, nikaachia tabasamu pana,
aliendelea kunitibu lile jeraha na baada ya muda, aliniambia niinuke.
“Mbona hunifungi bandeji?” nilimuuliza huku
nikijitazama pale kifuani.
“Wala hakuna haja, kitapona chenyewe, nakupa
siku mbili tu lazima kiwe kimekauka ila inabidi upate muda wa kutosha wa
kupumzika,” alisema, akaniongoza mpaka bafuni ambako kwa umakini mkubwa
aliniogesha kama mtoto mdogo huku akizingatia maji yasiguse jeraha langu.
“Wameshaamka?”
“Ndiyo, ila ilibidi niwadanganye kwamba
ulizidiwa tukiwa kule kwenye kazi kwa hiyo ndiyo nipo kukutibu, nakuomba sana
uitunze hii siri, si unajua Shamila mimi ni mwanangu japokuwa sijamzaa
mwenyewe, akijua itakuwa fedheha sana kwangu,” aliniambia, nikamtoa wasiwasi
huku nikitaka kujua kwa nini tendo la mimi na yeye lilikuwa tofauti sana?
“Ni kama nguvu chanya na chanya zimekutana,
hata mimi kuna mambo yamenitokea ambayo hayajawahi kunitokea tangu nipate akili
zangu,” alisema Junaitha huku safari hii yeye ndiyo akiwa ananionea aibu,
akishindwa hata kunitazama usoni mara mbili.
“Wewe ni mwanaume wa shoka,” alisema huku
akinibusu kwenye paji la uso wangu, tukarudi chumbani ambapo nilivaa nguo
zangu, akanishika mkono na kuniambia natakiwa ‘kuekti’ kama nasikia maumivu makali,
akanitoa mpaka sebuleni ambako niliwakuta Shamila, Firyaal na Raya wakiwa
wanatazama runinga kubwa ya ukutani.
Waliponiona tu, wote waliinuka haraka na
kunikimbilia, kila mmoja akitaka awe wa kwanza kunifikia, nikamuona Junaitha
akinitazama kwa macho yaliyoonesha kuwa na viulizo vingi, akawawahi:
“Bado hajapona, msimkumbatie kwa nguvu
mtamtonesha!” Nikaona wote wameishiwa pozi, wakaishia kunishika mikono tu huku
wakinitazama usoni, kila mmoja alionesha kuguswa mno na hali yangu, hakuna
aliyekuwa anajua kwamba nilikuwa ‘nikiwaektia’, Junaitha ambaye pale ndiyo
alikuwa mkubwa kuliko sisi wote, akawa ananitazama kama anayenisisitiza nisije
nikaharibu.
Nikaenda kukaa kwenye sofa la peke yangu, wote
wakanipa pole na nikawahakikishia kwamba nitakuwa sawa. Tukaanza kuulizana
maana ya kile kilichofanyika mpaka tukafanikiwa kumuokoa Shamila ambapo
Junaitha alianza kutufundisha mambo ambayo hakuna aliyekuwa akiyajua kati yetu,
ambayo kama hujui ungeweza kusema ni uchawi wa hali ya juu.
“Hata ukitaka kuingia benki na kuchukua
kiwango chochote cha fedha unachotaka, inawezekana, mbona rahisi tu,
nitawafundisha,” alisema.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment