ILIPOISHIA:
“Una..ta..ka
kufa...nya ni...ni,” sikumalizia kauli yangu, akawa tayari ameshafika pale
kitandani, tukagusanisha ndimi zetu huku Shamila akionesha kweli kudhamiria
kile alichokitaka. Hakuogopa kabisa kwamba pale ni wodini.
SASA
ENDELEA...
Nilijaribu kumzuia lakini haikusaidia
kitu, alishadhamiria na kwa ilivyoonesha, alikuwa tayari kufanya chochote ili
apate alichokuwa anakitaka. Tuliendelea kugusanisha ndimi zetu huku mikono yake laini ikitalii kwenye
viunga mbalimbali vya mwili wangu, nikaanza kuhisi hali ya tofauti.
Unajua jambo ambalo nitaendelea kulisema
kila siku, hakuna jambo baya kama kuyajaribu mapenzi. Wazee wetu waliosema
kwamba mapenzi hayajaribiwi, walikuwa sahihi kabisa. Wakati naanza uhusiano wa
kimapenzi na Shamila, nilikuwa najua kabisa kwamba tayari ninaye Raya ambaye
ananipenda sana na tumeshaahidiana vitu vingi, tena kibaya zaidi mimi ndiyo
nikiwa mwanaume wa kwanza maishani mwake.
Akilini mwangu nilijua kwamba hata
nikimkubalia Shamila, haiwezi kuwa na tatizo lolote kwa sababu kiukweli sikuwa
nimempenda kutoka ndani ya moyo wangu na nilipanga kumtumia kama daraja tu la
kunifanya nipate nilichokuwa nakitaka kwa urahisi.
Hata hivyo, tangu Shamila alipoanza kua
karibu na mimi, nilijikuta akiingia kwa kasi kwenye moyo wangu kuliko hata
nilivyotegemea. Jambo ambalo sikuwahi kulijua tangu awali ni kwamba kumbe
Shamila alikuwa mzuri kuliko Raya, kuanzia mwonekano, shepu, uchangamfu, uelewa
wa mambo mpaka kwenye ufundi wa ‘uwanja wa fundi seremala’.
Ilifika mahali mwenyewe nikawa najiona
kabisa kwamba nimeanza kumpenda Shamila kuliko Raya, jambo ambalo sikujua
mwisho wake utakuja kuwa nini. Nawasihi kwa mara nyingine wanaume, hasa vijana
kama sisi, hakuna kosa baya kama kucheza na hisia za wanawake wanaokupenda kwa
wakati mmoja.
Basi Shamila aliendelea na mbwembwe,
‘Jamal’ wangu akachaji ile mbaya, nikajikuta mimi ambaye mwanzo nilikuwa
navungavunga ndiyo nimekuwa nyota wa mchezo, kwa umakini wa hali ya juu
nikajibinua, Shamila akawa chini mimi juu, tukawa tunatazamana kama majogoo yanayotaka
kupigana, kila mmoja pumzi zikimtoka kwa nguvu.
Sikuwa na muda wa kusubiri, nilianza
kusakata kambumbu kwa mtindo wa kushambulia mfululizo, huku nikiwa makini
nisijitoneshe jeraha langu la kifuani, Shamila akawa anayapokea mashambulizi
yangu kwa miguno flan’ hivi ambayo ilizidi kunipandisha wazimu.
Ilifika mahali nikabadili mfumo wa
kusakata kabumbu, nikawa nakimbia na mpira kwenye chaki kama Christiano Ronaldo
vile, nikawa nahama pande zote na kumfanya Shamila apoteze ‘netiweki’, akaanza
kutoa miguno kwa nguvu akiwa amesahau kabisa kwamba hatukuwa kwenye mazingira
rafiki.
Niliongeza kasi, naye akaongeza kasi ya
kunikaba, dakika chache baadaye nilitangaza kuzifumania nyavu zake lakini kabla
sijamuwahi, na yeye alishatangaza kuzifumania zangu, ikawa ngoma droo!
Harakaharaka nilishuka pale kwenye
kitanda changu na kuvaa vizuri nguo zangu ambazo hata sikumbuki nilizitupa saa
ngapi sakafuni. Harakaharaka nikajiweka vizuri na kumsogelea Shamila ambaye eti
tayari alikuwa ameanza kukoroma kwa mbali, akionesha kuchoshwa mno na mpambano
ule wa kushtukiza.
Nikamtingisha kwa nguvu, akawa
ananisukuma kama anayesema ‘niache nipumzike bwana’. Nilipozidi kumsumbua,
aliinuka, naye akavaa magwanda yake, safari hii akiwa hataki kabisa kunitazama
usoni. Akajizoazoa mpaka kwenye ofisi ya manesi ambako nako kulikuwa na
kitanda, akajitupa kitandani.
Ilibidi mimi ndiyo niwe na kazi ya ziada
ya kuondoa ushahidi wote eneo la tukio, nikaenda kufungua mapazia, nikafungua
na milango na kuiweka kama inavyotakiwa kuwekwa, nikaongeza spidi ya feni na kurudi
kitandani, nikajilaza huku moyoni nikijipongeza kwa kumtolea uvivu Shamila
ambaye alikuwa akicheza na sharubu za simba.
Muda mfupi baadaye, niliona kivuli cha
mtu akipita dirishani kwa nje, akaenda upande mmoja kisha muda mfupi baadaye
akarudi na kusimama pale mlangoni, ilionesha kama ni mtu ambaye hakuwa na
uhakika sana wa mahali anakokwenda. Kwa kuwa pale nje ya wodi za ‘private’
kulikuwa na walinzi, nilisikia wakimsemesha.
Kama kawaida yangu, nikawahi kujihami
kwa kushuka pale kitandani haraka na kwenda kujibanza nyuma ya mlango ili hata
kama ni miongoni mwa wale wanaoisaka roho yangu, akiingia tu niwahi kuchomoka.
Katika mahojiano yake, niligundua kwamba
ni msichana, tena bado mdogo na alikuwa akitaka kuniona mimi maana niliwasikia
akiwatajia mpaka jina langu. Baada ya kumhoji sana, wale walinzi walimruhusu
kuingia, nadhani ni kwa sababu walishapewa maelekezo na Shamila juu ya kuwa
makini na watu wanaokuja kwa lengo la kuniona. Akafungua mlango na kuanza
kuangalia juu ya vitanda viwili vilivyokuwa ndani ya wodi hiyo.
“Firyaal,” nilisema baada ya kumtambua
kuwa ni yule mdogo wake Shenaiza ambaye nilipewa maagizo ya kwenda nyumbani
kwao kuonana naye, ambaye ndiye aliyenipa ‘hard disk’ iliyokuwa na siri nyingi
kuhusu ushetani uliokuwa ukifanywa na baba yake.
“Jamal! Alisema huku akitetemeka, uso
wake ukionesha dhahiri jinsi alivyokuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.
“Vipi mbona hivyo? Tulia kisha uniambie
nini kinachokusumbua,” nilisema huku nikifunga mlango na kusogea naye mpaka
pale kwenye kitanda changu.
“Baba anatarajiwa kurudi kesho nchini na
tayari walinzi wake wamegundua kwamba kuna kitu kwenye kompyuta yake
kimechomolewa, wakijua kwamba mimi na dada Shenaiza tunahusika hata sijui
itakuwaje.
“Nipo chini ya miguu yako nakuomba
unirudishie ile ‘hard disk’, nimefanya kazi kubwa sana kukutafuta, hospitali
nzima hawajui umelazwa wodi gani,” alisema Firyaal, nikashusha pumzi ndefu na
kumtazama.
“Usijali Firyaal kila kitu kitakuwa
sawa,” nilimwambia na kuanza kumtuliza, nikamhakikishia kwamba kabla ya hiyo
kesho, ataipata ‘hard disk’ yake, pia nikamwambia kuhusu matatizo yaliyokuwa
yanamkabili dada yake.
“Tusaidie kama unaweza, najua baba akija
maisha ya dada yapo hatarini sana, anaweza hata kuamuru auawe, yaani sijui baba
siku hizi amekuwaje,” alisema Firyaal huku akianza kuangua kilio. Niliendelea
kumtuliza huku nikitafuta mbinu ya kuwasaidia wote kwani kwa jinsi
ilivyoonesha, baba yao alikuwa mtu hatari hata ndani ya familia yake mwenyewe.
Nadhani mazungumzo yetu yalimzindua
Shamila aliyekuwa usingizini, akakurupuka na kutoka, akapigwa na butwaa kumuona
mdogo wake Shenaiza. Alimkumbuka vizuri kwa sababu hata siku niliyoenda
kuichukua ile ‘hard disk’, nilikuwa nimeongozana naye ingawa yeye alibaki ndani
ya teksi.
“He, vipi imekuwaje? Binti nani
amekuruhusu kuingia humu?” alihoji Shamila huku akijiweka vizuri nguo zake
pamoja na nywele ambazo bado zilikuwa zimevurugika. Ilibidi nimtulize na
kumweleza kilichomleta pale. Kwa bahati nzuri Shamila ni mwelewa sana, harakaharaka
alielewa, kwa pamoja tukawa tunajadiliana nini cha kufanya.
“Inabidi kwanza hiyo ‘hard disk’ yake
irudishwe haraka kisha baada ya hapo inabidi tufanye mpango wa kumtorosha
Shenaiza wodini haraka iwezekanavyo, hayo yote yanatakiwa kufanyika usiku wa
leo.
“Hata wewe hapa siyo mahali salama tena
pa kuendelea kukaa, ngoja kwanza nimesahau kuuliza kitu muhimu. Wewe binti upo
upande upi? Unamuunga mkono baba yako au na wewe unamsimamo kama wa dada yako?”
Shamila alimuuliza swali muhimu.
Msichana huyo mdogo alituhakikishia,
tena kwa kujiapiza kwamba kamwe hajawahi kumuunga mkono baba yake lakini
amekuwa akikosa mtu wa kumsaidia kupambana naye.
Kauli yake hiyo ilitufurahisha sana mimi
na Shamila, tukawa na uhakika kwamba sasa kazi itakuwa nyepesi kwa sababu
tayari tutakuwa na mtu kutoka ndani kabisa, ambaye angetusaidia kutimiza lengo
letu la kupambana na mtu huyo hatari.
Je,
nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment