ILIPOISHIA:
“Ulisema unasomea IT, hebu chukua ile
laptop pale uje hapa unisaidie kitu,” nilimtega, naye ni kama alikuwa
akiisubiri nafasi hiyo, harakaharaka aliinuka pale alipokuwa amekaa, akaenda
kuchukua laptop ya Shamila na kuja nayo kwenye lile kochi nililokuwa nimekaa,
akaja kukaa karibu kabisa na mimi kiasi cha kunifanya niwe nalisikia joto la
mwili wake, lililonakshiwa kwa manukato mazuri aliyokuwa amejipulizia.
Mara mlango wa jikoni ukafunguliwa.
SASA ENDELEA...
“Vipi?” Shamila aliuliza huku akiwa ni
kama ameshtuka f’lani hivi kuniona nikiwa nimekaa jirani namna ile na Firyaal.
“Kuna kazi namuelekeza anisaidie.”
“Ooh! Tena huyo atakufaa zaidi, si
amesema anajuajua mambo ya IT?”
“Ndiyo japo bado sijathibitisha,”
nilisema huku nikijifanya kumkandamiza Firyaal ili kuua soo, naye ni kama
alijua kilichokuwa ndani ya akili yangu, akatulia kiasi cha kufanya iwe vigumu
kwa Shamila kuelewa kilichokuwa kikiendelea kati yangu na msichana huyo mdogo
lakini mrembo.
Akaenda kwenye friji na kuchukua baadhi
ya vifaa kisha akarudi jikoni, akaniacha nikiwa bize nikijifanya namuelekeza
kitu Firyaal ambaye naye alikuwa akiitikia kwa umakini, alipoingia jikoni
tukatazamana.
“Hapa siyo sehemu sahihi, watatushtukia
sasa hivi,” nilimnong’oneza, harakaharaka akanikubalia kwa kutingisha kichwa.
Nikamwambia anisaidie kutafuta majina ya watu wote ambao walikuwa ‘wamesaidiwa’
na Shirika la Black Heart lililokuwa likiongozwa na baba yake kwenye zile data
tulizoziiba kwenye ile ‘hard disk’ aliyonipa.
Akahama pale alipokuwa amenifuata na
kurudi kwenye kiti chake, akajiinamia kwenye laptop na kuanza kufanya ile kazi
niliyomuagiza. Shamila alitoka tena jikoni na alipoona kweli Firyaal
amejiinamia na kompyuta, wala hakuhisi jambo lolote baya, akawa ananitazama kwa
macho fulani hivi ambayo nilimuelewa alichokuwa anamaanisha.
Firyaal aliendelea na kazi, Shamila na Raya
nao waliendelea na kazi, mimi nikawa nimekaa zangu pale kwenye kochi nikiwa
naendelea kuwaza hili na lile. Nikiri wazi kwamba kabla ya matatizo hayo
hayajaanza kunikumba, sikuwa napenda kukaa karibu na wasichana kabisa, yaani
kama ungekuja kwangu, kama usingenikuta natazama ‘movie’ basi ungenikuta
nacheza gemu za ‘Playstation’.
Tangu nilipoanza kukutana kimwili na
Raya, akili zilikuwa ni kama zimezibuka, nikawa najilaumu kwa kuchelewa
kuvumbua ‘hazina’ iliyojificha kwa kipindi chote hicho. Kabla sijaendelea,
naomba niliweke wazi hili kwa manufaa ya wengine. Wanaume wengi huwa
wanaharibikiwa maishani kwa sababu ya kuruka vipengele fulani katika hatua za
ukuaji.
Unakuta mtu ule muda ambao alitakiwa
afanye mambo ya ‘kitoto’ yeye anakuwa bize na masomo au kazi. Akishaingia
kwenye ndoa ndiyo anazibuka na kuanza kuona kama alikuwa anachelewa, matokeo
yake ndiyo unakuta mwanaume ana mke mzuri lakini kila siku anasaliti ndoa yake
kwa sababu kuna hatua ya ukuaji aliiruka.
Muda mfupi baadaye, chakula kilikuwa
tayari, Raya na Shamila wakaandaa chakula, Raya akiwa hajui kabisa kwamba
aliyekuwa akishirikiana naye kwa kila kitu alikuwa ni ‘mke mwenzie’, Firyaal
naye akijifanya anawaheshimu sana dada zake hao kumbe na yeye alikuwa
akijilengesha kwangu.
Baada ya kumaliza kuandaa, tulianza kula
huku Shamila akitusisitiza kwamba tusiwe na wasiwasi kuhusu Shenaiza,
akatuambia kwamba atamshughulikia na baada ya muda mfupi atarejewa na fahamu
zake. Sote tulikuwa kimya kabisa, mtu pekee aliyekuwa akizungumza alikuwa ni
Shamila.
Baada ya kumaliza kula, tulikaa pamoja
sebuleni hapo na kuanza kupanga namna ya kukabiliana na baba yake Shenaiza.
Nilimuuliza Firyaal amefikia wapi kwenye kazi niliyompa, akaniambia ameshapata
majina ya watu wote waliosaidiwa na shirika hilo pamoja na anuani zao za makazi
pamoja na ndugu zao waliokuwa hapa nchini.
“Basi naomba uunganishe na yale majina
ambayo nilishayapata kuanzia mwanzo,” nilisema, Firyaal naye akaitikia kwa adabu
kabisa, watu wote wakazidi kutuamini kwamba kweli tulikuwa kikazi zaidi.
Bado ule mchezo wake wa kunitazama kwa
kuibia hakuwa ameuacha lakini kwa kuwa sasa Raya na Shamila walikuwa pale
sebuleni, nilijifanya sijui chochote kinachoendelea kwa sababu nilihofia
wanaweza kutufuma tukitazamana halafu wakatufikiria vibaya.
Tuliendelea kupanga mipango yetu na
mwisho tukakubaliana kwamba kwa kuwa ushahidi wote tayari tulikuwa nao, twende
tukatoe taarifa polisi ili watusaidie kupambana na genge hatari la baba yake
Shenaiza.
Kilichonipa moyo kwamba kila kitu
kitafanikiwa, ni jinsi Firyaal alivyoonesha kuchukizwa na vitendo vya baba
yake, akatuhakikishia kwamba japokuwa anajua baba yake anaweza hata kufungwa,
yupo tayari kwa chochote mpaka tufanikiwe.
Wazo hilo lilipitishwa, tukakubaliana
kwamba usiku ule Shamila anatakiwa kurudi kule hospitalini ili kuhakikisha
hakuna anayeshtukia kama mimi na Shenaiza tumetoroshwa hospitalini, na asubuhi
na mapema ya siku inayofuatia, mimi nitaongozana na Raya mpaka kituo kikuu cha
polisi kwa ajili ya kwenda kutoa taarifa.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeshaenda,
Shamila alimwambia Firyaal amrudishe mpaka hospitalini kwa kutumia gari lake
kisha arudi nyumbani kwao, Kurasini ili asije akashtukiwa lakini msichana huyo
alikataa katakata, akasema alishamuaga mama yake kwamba anakwenda kwenye
‘birthday’ ya rafiki yake na kwamba hatarudi mpaka asubuhi na aliruhusiwa.
“Twende nikupeleke wewe kazini mi
nitakuja kulala hapahapa na dadaa’ngu Shenaiza,” alisema, Shamila na Raya
wakamkubalia bila kujua kwamba kuna kitu alichokuwa anakifuata.
Raya naye alipoulizwa kama atarudi
nyumbani kwao, naye alisema atakaa na mimi mpaka asubuhi ya kesho yake. Shamila
alikubali ingawa nilimuona kama wivu unamsumbua sana, akainuka na kwenda kuanza
kuandaa mazingira ya sisi sote kulala.
Mimi aliniandalia kwenye chumba cha peke
yangu, Firyaal akamwambia atalala na dada yake kwenye chumba cha wageni na Raya
atalala kwenye chumba chake, wote tukamkubalia kwani kwa wakati huyo yeye ndiye
aliyekuwa bosi wetu.
Alienda kuoga na kuanza kujiandaa kisha
akatuaga na kututaka tuwe makini, hasa mimi, akatoka na Firyaal kuelekea
hospitali huku akiniachia maagizo kwamba Firyaal akirudi, nikamsaidie kufungua
geti aingize gari kisha baada ya hapo, nifunge milango yote na kuzima taa zote
za ndani na nje, nikamkubalia.
Walipotoka, ndani nilibaki na Raya tu
ambaye ilionesha alikuwa na hamu kubwa ya mimi na yeye kubaki wawili tu.
Alipohakikisha wameshaingia ndani ya gari na kuondoka, harakaharaka alinifuata
na bila kuzungumza chochote, alianza fujo zake akitaka nikamalizane naye fasta
kabla Firyaal hajarejea.
Hata hivyo, kwa kuwa tayari nilikuwa na
ratiba nyingine kichwani, nilimdanganya kwamba siku hiyo nilikuwa nimechoka
sana na jeraha langu lilikuwa likima kwa sababu ya purukushani za kutwa nzima,
nikamuomba kama hatajali, tukapumzike kwanza mpaka baadaye.
Nilimuona akikubali kwa shingo upande,
akaenda kuoga na kuniacha niko pale sebuleni najifanya niko bize na laptop.
Baada ya kumaliza kuoga alinifuata tena, nikaendelea kumsisitizia kwamba hali
yangu haikuwa nzuri, akaniomba basi tukalale kitanda kimoja ambapo pia
nilimkatalia na kumwambia nitamfuata usiku sana wakati Firyaal ameshalala ili
tusije kuonesha picha mbaya.
“Basi naacha mlango wazi,” alisema,
nikatingisha kichwa kuonesha kumkubalia, akaondoka kwa shingo upande na kwenda
kulala. Kutokana na uchovu aliokuwa nao wa pilikapilika za kutwa nzima,
hakuchukua raundi, akapitiwa na usingizi mzito.
Nusu saa baadaye, alikuwa akikoroma, hata
niliponyata na kwenda kumchungulia, alionesha ameshalala fofofo, moyoni nikawa
nachekelea. Harakaharaka nilienda kwenda chumba nilichopangiwa kulala, nikaingia
bafuni na kujimwagia maji kupunguza uchovu kisha nikatoka na kwenda kukaa
sebuleni nikimsubiri Firyaal kwa shauku kubwa, nikiwa nimejifunga taulo tu!
Shetani wa mahaba alikuwa amenizidi nguvu.
Dakika kadhaa baadaye, nikasikia honi ya
gari, harakaharaka nikatoka na kwenda kufungua geti, alikuwa ni Firyaal, aliponiona
nimejifunga taulo tu, alijifanya kushtuka kisha nikamuona akitabasamu, akaingiza
gari na kulipaki, nikafunga mageti kama Shamila alivyoniagiza, tukaingia ndani
na kwenda mpaka sebuleni.
“Dada Raya yuko wapi?” aliuliza Firyaal
kwa sauti ya chini, nikamwambia ameshalala na sasa anakoroma, nikamuona
akishusha pumzi ndefu na kunitazama usoni, tukawa tunatazamana.
“Nataka nikalale na dada Shenaiza,”
alisema kwa sauti ya kudeka huku akinisogelea na kujilaza kifuani kwangu,
nikapitisha mkono wangu na kumshika kiunoni, nikamuona akiruka kama aliyepigwa
na shoti ya umeme.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
No comments:
Post a Comment