Watumishi wa Mungu wanaofanya kazi ya kusambaza injili kupitia karama ya uimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone
, Ambwene Mwasongwe, Angela, Paul Clement, Martha Mwaipaja na wengine wengi wanatarajiwa kushusha upako wa nguvu ndani ya Uwanja wa Taifa, Agosti 8, 2014 katika Tamasha la Matumaini.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha
hilo la kila mwaka, Luqman Maloto wasanii hao watafanya shoo ya kumtukuza Mungu
katika uwanja huo kama ilivyokuwa katika Tamasha la Matumaini 2013 ambapo
mashabiki waliohudhuria waliburudika vya kutosha.
“Nawasihi wale wapenzi wa nyimbo
za injili waje kwa wingi kwani orodha ya wasanii wa nyimbo za injili inazidi
kuongezeka kila siku, watakuwepo wengi kushusha upako,” alisema Maloto.
Mbali na burudani hiyo ya nyimbo
za injili, pia kutakuwa na ‘package’ tofautitofauti za burudani kama vile mpira
wa miguu na ndondi ambapo mwaka huu Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba
atazichapa na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala.
“Tutakuwa na mwanamuziki Khalid
Chokoraa ambaye atazichapa ulingoni na Said Memba huku Bingwa wa Afrika
Mashariki na Kati, Thomas Mashali akizitwanga na ‘mbunge mtarajiwa’, Mada
Maugo.
“Ushindani mkali pia utawekwa na
mastaa wa Bongo Movie, Cloud 112 na Jacob Steven ‘JB’ ambao siku hiyo
watazipiga katika pambano la raundi 4,” alisema Maloto.
Maloto aliongeza kuwa ukiachilia
mbali mechi za mpira wa miguu kati ya Wabunge Mashabiki wa Yanga dhidi ya
wenzao wa Simba, timu ya Bongo Movie itapepetana na Bongo Fleva sambamba na
Azam watakaokipiga dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
“Pia katika muziki,Yemi Alade
kutoka Nigeria atachuana vikali na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ huku wasanii
wengine wa Bongo Fleva wakiendelea kuongezeka wakiwemo Madee, R.O.M.A
Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Ali Kiba na
kwa mara ya kwanza Wema Sepetu atapanda jukwaani na kuimba nyimbo za bebi wake
‘Diamond’ jukwaani,” alisema Maloto.
Tamasha hilo limedhaminiwa na
kampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, E FM (93.7), Clouds FM (88.5), Sycorp
pamoja na Times FM (100.5).
USIKU WA MNYAMA NA WANYAMA KUTINGISHA DAR LIVE IDD PILI
Stori: Showbiz
Shoo kubwa ya Mnyama na Wanyama
ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo katika Sikukuu ya Idd Pili, wasanii kibao
wakiongozwa na TID watakinukisha kinoma ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala
Zakhem jijini Dar.
Akipiga stori na Showbiz, mratibu wa burudani wa
Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, wanyama watakaotimba ndani ya nyumba
siku hiyo ni pamoja na Naaziz kutoka Kenya, Jay Mo, Inspector Haroun ‘Babu’,
Yakuza Mobb, Jeez Mabovu, Jafarai na Meninah! Patachimbika.
“Itakuwa ni bonge la shoo ambapo Mnyama TID
atafanya yake akiwa sambamba na wanyama wengine kibao kukamilisha burudani
katika msimu wa Sikukuu ya Idd Pili,” alisema Abby Cool.
No comments:
Post a Comment