Makala: Hashim Aziz
Jamaa anaitwa Kevin Liles, alizaliwa
Februari 27 pande za Baltimore, Maryland nchini Marekani. Japokuwa jina na sura
yake havijulikani kiivyo, Kevin ndiye ‘mastermind’ wa wasanii wakubwa wanaopeta
kwenye levo za kimataifa wakiwemo Jay Z, Diddy, Kanye West, Trey Songz, Big
Sean, Rick Ross, Rihanna na wengine wengi kibao.
KEVIN
NI NANI HASA?
Naamini wengi hawamjui Kevin lakini
ukweli ni kwamba jamaa ndiye ‘mchawi’ wa muziki wa Hip Hop, R&B na Pop, akimpenda
msanii na kumkubali, akaamua kumsimamia kimuziki, lazime atusue na kupaa levo za mbalai sana, hiyo haina ubishi.
msanii na kumkubali, akaamua kumsimamia kimuziki, lazime atusue na kupaa levo za mbalai sana, hiyo haina ubishi.
ALIKOTOKEA
Alianza kujihusisha na muziki akiwa
meneja wa wasanii mbalimbali miaka kibao iliyopita lakini nyota yake ilianza kung’ara
mwaka 1999 alipochaguliwa kuwa rais wa kampuni kubwa ya kurekodi muziki, Def
Jam Recordings na makamu wa rais wa kampuni mama, The Island Def Jam Music
mpaka mwaka 2004.
Baada ya hapo, Kevin alihamia kwenye
kampuni nyingine kubwa zaidi ya kurekodi muziki, Warner Music Group ambako
alisimama kama makamu wa rais akiwa chini ya bosi wake wa zamani, Lyor Cohen.
MJASIRIAMALI
WA MUZIKI
Baadaye, Septemba 2009 baada ya
kuiongoza kampuni hiyo kwa mafanikio makubwa na kuwaibua wasanii kibao kutoka
sifuri mpaka kuwa mastaa wakubwa duniani, Kevin aliamua kuachana na ajira,
akajiajiri kwenye ujasiriamali wa muziki.
Kutokana na heshima kubwa aliyoipata
katika kipuindi chote alipokuwa anafanya kazi na kampuni hizo kubwa, Kevin
ambaye ni mume halali wa Erika, aliendelea kutusua kivyakevyake, akaendelea
kuzalisha wasanii wapya na kuwapa mafanikio makubwa kila kukicha huku akikodiwa
na kampuni nyingine kibao kama Sony na Atlantic Music.
YEYE
NA DIAMOND
Juni Mosi, 2014 , Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ziarani nchini Marekani, ‘aligumiana’
na Diamond ambaye naye alikuwa kwenye mishemishe zake za kimuziki.
Wakala chakula cha jioni pamoja ambapo
mbali na mambo mengine, usiku huo mheshimiwa alimkutanisha Diamond na Kevin
(tazama picha), wakajadili kwa kirefu jinsi ya kumsaidia bwa’ mdogo huyo pamoja
na wasanii wengine wa Kitanzania katika Bongo Fleva na Bongo Muvi.
NYOTA
NJEMA KWA DIAMOND
Kitendo cha rais kumkutanisha mkali
huyo wa Ngololo na mtu mkubwa duniani kama Kevin, ilikuwa ni sawa na nyota
njema iliyowaka kwenye maisha ya Diamond. Kumbuka nimeeleza kwamba Kevin
akimpenda msanii na akakidhi viwango anavyovitaka, lazima ambadilishe na kuwa
staa mkubwa duniani kama ilivyotokea kwa Jay Z, Rihanna, Trey Songz, Big Sean
na wengine kibao.
KWAKO
DIAMOND
Ninachotaka kushadadia hapa ni kwamba,
kama Diamond kwa miaka mingi ulikuwa ukihangaika kwa waganga wa kienyeji
kung’arisha nyota yako kama ambavyo baadhi ya watu wanakutuhumu (sina hakika na
madai hayo yasiyo na msingi), basi ulikuwa ukipoteza muda.
Mganga au mchawi wako ambaye unapaswa
kumng’ang’ania kwa sasa ni Kevin. Mheshimiwa Rais Kikwete ameshakufungulia
milango, kazi ni kwako sasa.
KEVIN
ANAKUJA BONGO
Katika salamu zake alizozitoa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Juni 14, 2014
kwenye tamasha kubwa lililoandaliwa na Clouds Media Group, Rais Kikwete
aliahidi kumdondosha Bongo Kevin pamoja na wadau wengine, akiwemo mmiliki wa
kituo cha runinga cha E! News pamoja na msanii Usher Raymond kuwanoa wasanii wa
nyumbani ili nao wapae kimataifa.
Wasanii wa Bongo, mpewe nini tena?
Changamkieni fursa ili Bongo Movie ifike Hollywood na Bongo Fleva ipae
kimataifa zaidi, ‘mchawi’ anakuja, mtumieni kusafisha nyota zenu.
No comments:
Post a Comment