Makala: Hashim Aziz
Kilometa 75, Kaskazini mwa Jiji la Dar es Salaam, ndipo unapopatikana mji mkongwe na wa kihistoria wa Bagamoyo ambao ni miongoni mwa miji yenye vivutio vya kipekee duniani, ulioanzishwa karne ya 18, ukiwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi.
Kilometa 75, Kaskazini mwa Jiji la Dar es Salaam, ndipo unapopatikana mji mkongwe na wa kihistoria wa Bagamoyo ambao ni miongoni mwa miji yenye vivutio vya kipekee duniani, ulioanzishwa karne ya 18, ukiwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi.
Historia inaonesha kuwa Bagamoyo
iliyopo mkoa wa Pwani ndiyo kilikuwa kituo kikuu cha biashara ya watumwa na
bandari ya kwanza katika mwambao wa Afrika Mashariki, achilia mbali magofu ya kale, makaburi ya karne nyingi
zilizopita, msikiti wa kwanza na kanisa la kwanza Afrika Mashariki pamoja na
njia za watumwa (caravans).
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Gazeti la
Uwazi lilisaga lami mpaka Bagamoyo, lengo kubwa likiwa ni kuangalia jinsi
wakazi wa eneo hilo wanavyonufaika na utajiri mkubwa wa kihistoria unaowavutia
watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani, ahadi za mbunge na jinsi
anavyozitekeleza pamoja na matatizo ya wananchi.
Uwazi lilijipenyeza mpaka kwenye Kata
za Dunda, Magomeni, Yombo, Kiromo, Zinga, Kerege na Vigwaza zinazounda jimbo
hilo linaloongozwa na Mheshimiwa Shukuru Kawambwa (CCM) ambaye pia ni Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kubaini mambo mbalimbali.
MATATIZO
YA WANANCHI
Katika ziara yake, Gazeti la Uwazi lilibaini
matatizo yakiwemo ukosefu wa madawati, vyumba vya madarasa na vifaa vya
kujifunzia katika baadhi ya shule. Uvuvi haramu ni tatizo lingine linalotishia
afya ya wananchi wa jimbo hilo nauhai wa viumbe vya baharini ambapo wavuvi hutumia
‘kokoro’ na wakati mwingine baruti.
Kukosekana kwa uwazi wa mapato ya
utalii katika Kijiji cha Kaole na Ngome Kongwe kwenye magofu ya kale, ukosefu
wa masoko ya uhakika ya mazao ya wakulima yakiwemo mpunga na matunda, mgogoro
wa ardhi katika Vijiji vya Buma na Mataya na ukosefu wa huduma bora za afya ni
miongoni mwa matatizo mengine yanayowasumbua wakazi wa Bagamoyo.
MAPATO
YA UTALII
Uwazi lilichanja mbuga mpaka kwenye
Kijiji cha Utalii cha Kaole na kufanikiwa kuzungumza na mkuu wa kituo hicho,
Siyawezi Hungo ambaye alifafanua kwamba kwa kawaida, kituo chake hupokea wageni
wengi katika miezi ya Julai mpaka Desemba ambapo kwa wastani, watalii 4466
huingia kila mwezi.
“Watalii kutoka nje hulipa shilingi
20,000 kwa watu wazima na 10,000 kwa watoto chini ya miaka 16, kwa wazawa
hulipa shilingi 1,000 na watoto ni shilingi 500. Fedha zote zinazopatikana,
huwa tunazikabidhi kwa idara ya mambo ya kale ambayo yenyewe ndiyo inayojua
namna zinavyotumika,” alisema mama Siyawezi.
MAELEZO
YA MBUNGE
Uwazi lilisaga lami hadi kwenye ofisi
ya mheshimiwa Kawambwa ambapo lilipokelewa na katibu wa mbunge huyo, Magreth
Masenga aliyekuwa na haya ya kuzungumza:
“Kwenye elimu, mbunge amejenga shule
tatu, chenji ya rada imenunua vitabu kwa wingi kwenye shule karibu zote za hapa
jimboni, shule nyingi zimeingiziwa umeme na wanafunzi wanaokaa chini ni
wachache sana, tena kwenye baadhi ya shule.
“Kwenye afya, mbunge amewezesha
kujengwa kwa chumba cha kisasa cha upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya
Bagamoyo na kupatikana kwa vitanda ingawa suala la manesi na madawa bado ni
tatizo. Pia zahanati zote zimepatiwa umeme wa solar kwa msaada wa Shirika la
Jewish Heart for Africa (JHFA).
“Wananchi hawana kabisa tatizo la maji,
mbunge amechimba visima zaidi ya 200 na mradi wa Ruvu Chini pia unatusaidia. Katika
kilimo, kuna ‘scheme’ kubwa za umwagiliaji katika Vijiji vya Chaulo na Jaika na
pia ameshughulikia migogoro ya ardhi.
“Kuhusu uvuvi haramu,mbunge ametoa
mafunzo maalum kwa wavuvi pamoja na kuwapa vifaa vya kisasa zikiwemo boti za
uvuvi. Pia amewapa ajira vijana wengi kwa kuwakopesha bodaboda na kuwapa
mafunzo ya ujasiriamali wanawake wengi.
“Kuhusu mapato ya utalii, fedha huwa
zinaingizwa kwenye mapato ya halmashauri na ndizo zinazojenga barabara za
mitaa, si unaona hapa Bagamoyo barabara nyingi ni za lami, pia matumizi mengine
ya fedha hizo nafikiri utayapata ukienda halmashauri.
“Kwenye michezo kuna mashindano ya
Kawambwa Cup ambayo yanawapa ajira vijana wengi, kimsingi mheshimiwa
anajitahidi sana kuwatumikia wananchi na kuwakwamua kutoka kwenye umaskini. Pia
anawasomesha wanafunzi wengi sana hapa jimboni, wananchi ni mashahidi wa jinsi
anavyowatumikia,” alihitimisha Masenga.
No comments:
Post a Comment