Makala: Hashim Aziz
“Katika project hiyo, tutakuwa tukiwafanyia usaili wasanii chipukizi ambao watakuwa wakichukua fomu kwetu kila baada ya wiki mbili, baada ya hapo, wale watakaokidhi viwango, tutawaingiza kwenye studio yetu lakini kabla ya hapo watapewa mafunzo ya sauti na Ochu kisha tutawarekodia ngoma mojamoja kwa gharama ya shilingi elfu ishirini tu.
“Wanaotaka shindana nami sema... watapata
zero! Tena na tena, tena na tena...” hicho ni kibwagizo maarufu kilichopo katika
ngoma ya mwanadafada Witness Mwaijaga ‘Witnesz The Fitnes’, mwanadada pekee
anayekaza kunako gemu la Hip Hop tangu kitambo hicho!
Wengi wanamfahamu vyema tangu kipindi
alichong’ara kwenye mashindano ya Cocacola Pop Star ambapo alikutana na Langa
Kileo (R.I.P) na mwanadada mwingine, Sarah Kais ‘Shaa’, wakakimbiza kinoma na
ngoma yao ya Kiswanglish.
Hata hivyo, kundi hilo halikudumu
kutokana na sababu za kimaslahi, kila mmoja akawa anafanya kazi kama solo
artist, Witnesz akazidi kukaza kimpango wake, akafanya tour nyingi za nje ya
nchi, akarelease ngoma kibao ikiwemo Zero ambayo ilimfanya apate tuzo ya
Channel O (Wimbo Bora wa Afrika Mashariki) pamoja na Tuzo za Kili.
Miaka ikakatika, Witnesz akawa dizani
kama amepotea kwenye gemu lakini kumbe alikuwa akiendeleza harakati kimataifa
zaidi.
KIMATAIFA
ZAIDI
Ndoto zake za siku nyingi za kukutana
na Busta Rhymes ambaye ndiye aliyemvutia kuingia kwenye gemu, zilitimia mwaka
2010 ambapo alipata bahati ya kukutana naye uso kwa uso, akapiga naye picha na
kumuwekea sahihi yake kwenye Biblia.
“Mwaka 2012 nilichaguliwa kuwa mwakilishi
wa mpango wa Ubalozi wa Marekani uitwao IVLP (International Visitors Leadership
Programme) nikiwa kama mwakilishi wa wasanii wa Hip Hop wa Tanzania, nikapata
nafasi ya kufanya ziara ya wiki tatu nchini Marekani ambapo nilitembelea sehemu
kibao zikiwemo Washington DC, New Orleans, Los Angeles California, New York, Detroit
(Michigan).
“Katika sagfari hiyo, nilipata bahati
ya kukutana na wakongwe kibao kunako gemu la kimataifa, nikaweka historia ya
aina yake,” anasema Witnesz ambaye kwa sasa amerejea kwa staili nyingine
kabisa, Ochuness.
OCHUNESS
NI NINI?
“Mwaka 2007 nilikutana na mchizi
anaitwa Ochu Sheggy (mtoto wa msanii mkongwe, marehemu Eggy Sheggy) katika
studio moja Bongo. Kiukweli tukafanya kazi pamoja mbili tatu lakini baadaye
tukafall in love na kuanzisha safari ya kimapenzi.
“Hayakuwa mapenzi tu bali mapenzi na
kazi, jamaa naye ni msanii wa kuimba, prodyuza, mchoraji na mwalimu wa sauti.
Kwa pamoja tukakubaliana kuanzisha project ambayo itaakuwa ikitushirikisha sote
wawili, mimi (Witnesz) na Ochu, tukachagua jina tuliloona linafaa ndiyo
Ochuness ikazaliwa ikiwa ni muunganiko wa majina yetu mawili, Ochu na Witness,”
alifafanua Witnesz.
UJIO
MPYA
“Tayari kunakazi mpya ya Ochuness
iitwayo Think About It ambayo audio yake na video vinabamba kinoma kwenye media
za ndani na nje ya nchi. Mimi na Ochu tumefanya kazi kubwa sana na kile mtu
anayeisikia ngoma hiyo anakubaliana na viwango vya ngoma hiyo.
MKAKATI
WA KUSAIDIA CHIPUKIZI
“Ujio wetu mpya umelenga pia
kuwasaidia wasanii wanaochipukia ambapo tumeandaa bonge la project iitwayo
Rekodi kwa Shilingi Elfu Ishirini ambayo itakuwa endelevu.
“Katika project hiyo, tutakuwa tukiwafanyia usaili wasanii chipukizi ambao watakuwa wakichukua fomu kwetu kila baada ya wiki mbili, baada ya hapo, wale watakaokidhi viwango, tutawaingiza kwenye studio yetu lakini kabla ya hapo watapewa mafunzo ya sauti na Ochu kisha tutawarekodia ngoma mojamoja kwa gharama ya shilingi elfu ishirini tu.
“Hii ni fursa kwa wasanii ambao wana
dreams za kuwa mastaa lakini wanakosa njia ya kutokea, nawasihi waje kwa wingi
katika ofisi zetu zilizopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam na tunaanza rasmi
Julai hii.
No comments:
Post a Comment