Monday, January 9, 2012

SAKATA LA MADAKTARI MUHIMBILI: THE SAGA CONTINUES

Dk. Namala
HASH POWER 7113
Chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimesema kitendo cha wizara ya afya na ustawi wa jamii kuwaondoa madaktari 229 katika hospital ya taifa ya Muhimbili kimeathiri upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa na kusababisha kutokea vifo vingi kwa kukosa matibabu.

Chama hicho (MAT) kimesema huduma katika hospital hiyo kubwa nchini zimezorota kwa kiwango kikubwa kutokana na madaktari wachache waliopo kushindwa kukidhi kutoa huduma ya matibabu hata nusu ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.


Akizungumza jijini Dar-Es-Salaam, Rais wa chama hicho Dk. Namala Mkopi amesema kitendo cha madaktari hao kupewa barua ya kurejeshwa wizara ya afya na ustawi wa jamii huku maelfu ya watanzania wakiihitaji huduma yao ni cha hatari kwa kuwa kimeathiri utendaji na upatikanaji huduma za afya hospitalani hapo.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...