Sehemu ya shehena ya madawa yaliyokamatwa |
(Kwa msaada wa Michuziblogspot.com)
Jumla ya kilo
209 za dawa za kulevya aina ya Heroine zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi
ya shilingi Bilioni 9, zimekamatwa katika Kijiji cha Mchinga mkoani Lindi na
watu … wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na dawa hizo haramu.
Akizungumza na
waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polis wa Mkoa wa Lindi, George
Mwakajinga, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Morine Amatus Liyumba (21),
Pendo Mohamed Cheusi (67) ambaye ni mkazi na mkulima katika kijiji hicho, Hemed Said (27), dereva na mkazi wa Mtoni, jijini, Dar es Salaam, Ismail Adam (Athuman Mohamed Nyaubi ,28,) ambaye ni mfanyabiashara wa magari jijini Dar es Salaam.

Inaelezwa kuwa
kiwango walichokamatwa nacho, ni kikubwa na hakijawahi kutokea katika historia tangu
kuanzishwa kwa kitengo cha kupambana na kuzuia dawa za kulevya nchini mwaka
1990. Shehena hiyo iliyokuwa imefichwa kitaalamu ndani yamadumu makubwa,
inadaiwa kuwa ilikuwa ikisafirishwa kuelekea nchini Afrika Kusini. Watuhumiwa
walisafirishwa hadi jijini Dar es
Salaam na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku
chache zijazo kujibu tuhuma zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment