HASH POWER 7113
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, mbunge wa
Jimbo la Arumeru kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Jeremia Sumari
amefariki dunia leo.
Mbunge huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa kipindi kirefu
na wakati anakutwa na mauti leo alfajiri alikuwa amelazwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Jeremia Sumari ni mbunge wa pili kwa bunge la Jamhuri ya
muungano wa Tanzania
kufariki kwa mwaka huu 2012 baada ya kutanguliwa na mbunge wa viti maalum
Chadema, Regia Mtema.
Inna Lilahhi wa Inna illaih Rajiun
No comments:
Post a Comment