HASH POWER 7113
Mchezaji wa Barcelona Lionel Messi (24) alitunukiwa tuzo ya
FIFA Ballon d’O kwa mara ya tatu mfululizo na kuwashinda wachezaji wenzake kama Xavi na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo katika tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwaka.
Messi, man of the match katika champions league final mwaka
2011, pia alishinda kombe la La Liga, Spanish Supercopa, UEFA Super Cup na
Kombe la klabu bingwa ya dunia mwaka uliopita.
Manager wa Manchester United Sir Alex Ferguson na Xavi wote
walitoa maneno ya heshima kwa Messi.
Ferguson alisema Messi anaweza kuwekwa katika mizani ya
magwiji wa soka duniani katika miaka mingi ijayo, hata kama bado ana miaka 24.
Kocha wa MAN U Alex Ferguson alizawadiwa FIFA Presidential
award for services to football, kocha wa Barcelona Pep Guardiola alitajwa kama
kocha bora wa Dunia 2011 baaada ya kuiongoza Barcelona kushinda makombe matano.
mchezaji MBRAZIL NEYMAR alishinda tuzo ya Puskas kwa kufunga
goli bora la mwaka wakati Wyne Rooney alipewa tuzo ya kuwa mmoja kati ya
wachezaji wanaounda kikosi cha mwaka.
jana hiyo hiyo kilitangazwa kikosi bora cha mwaka kwa mujibu
wa FIFA, huku kikosi hicho kikitawaliwa na wachezaji wa Barcelona, Manchester
United na Real Madrid pekee.ambao ni Iker Casillas (Real Madrid), Dani Alves
(Barcelona), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Nemanja
Vidic (Man Utd), Andres Iniesta (Barcelona).
wengine ni Xabi Alonso (Real Madrid), Xavi (Barcelona),
Lionel Messi (Barcelona), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Wayne Rooney (Man
Utd).
No comments:
Post a Comment