TAMASHA LA MATUMAINI 2014 LANUKIA


Watumishi wa Mungu wanaofanya kazi ya kusambaza injili kupitia karama ya uimbaji wa nyimbo za injili, Upendo Nkone
, Ambwene Mwasongwe, Angela, Paul Clement, Martha Mwaipaja na wengine wengi wanatarajiwa kushusha upako wa nguvu ndani ya Uwanja wa Taifa, Agosti 8, 2014 katika Tamasha la Matumaini.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo la kila mwaka, Luqman Maloto wasanii hao watafanya shoo ya kumtukuza Mungu katika uwanja huo kama ilivyokuwa katika Tamasha la Matumaini 2013 ambapo mashabiki waliohudhuria waliburudika vya kutosha.

“Nawasihi wale wapenzi wa nyimbo za injili waje kwa wingi kwani orodha ya wasanii wa nyimbo za injili inazidi kuongezeka kila siku, watakuwepo wengi kushusha upako,” alisema Maloto.
Mbali na burudani hiyo ya nyimbo za injili, pia kutakuwa na ‘package’ tofautitofauti za burudani kama vile mpira wa miguu na ndondi ambapo mwaka huu Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba atazichapa na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala.
“Tutakuwa na mwanamuziki Khalid Chokoraa ambaye atazichapa ulingoni na Said Memba huku Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Thomas Mashali akizitwanga na ‘mbunge mtarajiwa’, Mada Maugo.
“Ushindani mkali pia utawekwa na mastaa wa Bongo Movie, Cloud 112 na Jacob Steven ‘JB’ ambao siku hiyo watazipiga katika pambano la raundi 4,” alisema Maloto.
Maloto aliongeza kuwa ukiachilia mbali mechi za mpira wa miguu kati ya Wabunge Mashabiki wa Yanga dhidi ya wenzao wa Simba, timu ya Bongo Movie itapepetana na Bongo Fleva sambamba na Azam watakaokipiga dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
“Pia katika muziki,Yemi Alade kutoka Nigeria atachuana vikali na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ huku wasanii wengine wa Bongo Fleva wakiendelea kuongezeka wakiwemo Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Ali Kiba na kwa mara ya kwanza Wema Sepetu atapanda jukwaani na kuimba nyimbo za bebi wake ‘Diamond’ jukwaani,” alisema Maloto.
Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, E FM (93.7), Clouds FM (88.5), Sycorp pamoja na Times FM (100.5).
USIKU WA MNYAMA NA WANYAMA KUTINGISHA DAR LIVE IDD PILI
Stori: Showbiz
Shoo kubwa ya Mnyama na Wanyama ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo katika Sikukuu ya Idd Pili, wasanii kibao wakiongozwa na TID watakinukisha kinoma ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar.
Akipiga stori na Showbiz, mratibu wa burudani wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, wanyama watakaotimba ndani ya nyumba siku hiyo ni pamoja na Naaziz kutoka Kenya, Jay Mo, Inspector Haroun ‘Babu’, Yakuza Mobb, Jeez Mabovu, Jafarai na Meninah! Patachimbika.
“Itakuwa ni bonge la shoo ambapo Mnyama TID atafanya yake akiwa sambamba na wanyama wengine kibao kukamilisha burudani katika msimu wa Sikukuu ya Idd Pili,” alisema Abby Cool.

No comments:

Post a Comment