Wednesday, July 9, 2014

OCHUNESS; MAPINDUZI KATIKA BONGO FLEVA

Makala: Hashim Aziz
“Wanaotaka shindana nami sema... watapata zero! Tena na tena, tena na tena...” hicho ni kibwagizo maarufu kilichopo katika ngoma ya mwanadafada Witness Mwaijaga ‘Witnesz The Fitnes’, mwanadada pekee anayekaza kunako gemu la Hip Hop tangu kitambo hicho!
Wengi wanamfahamu vyema tangu kipindi alichong’ara kwenye mashindano ya Cocacola Pop Star ambapo alikutana na Langa Kileo (R.I.P) na mwanadada mwingine, Sarah Kais ‘Shaa’, wakakimbiza kinoma na ngoma yao ya Kiswanglish.
Hata hivyo, kundi hilo halikudumu kutokana na sababu za kimaslahi, kila mmoja akawa anafanya kazi kama solo artist, Witnesz akazidi kukaza kimpango wake, akafanya tour nyingi za nje ya nchi, akarelease ngoma kibao ikiwemo Zero ambayo ilimfanya apate tuzo ya Channel O (Wimbo Bora wa Afrika Mashariki) pamoja na Tuzo za Kili.


Miaka ikakatika, Witnesz akawa dizani kama amepotea kwenye gemu lakini kumbe alikuwa akiendeleza harakati kimataifa zaidi.
KIMATAIFA ZAIDI
Ndoto zake za siku nyingi za kukutana na Busta Rhymes ambaye ndiye aliyemvutia kuingia kwenye gemu, zilitimia mwaka 2010 ambapo alipata bahati ya kukutana naye uso kwa uso, akapiga naye picha na kumuwekea sahihi yake kwenye Biblia.
“Mwaka 2012 nilichaguliwa kuwa mwakilishi wa mpango wa Ubalozi wa Marekani uitwao IVLP (International Visitors Leadership Programme) nikiwa kama mwakilishi wa wasanii wa Hip Hop wa Tanzania, nikapata nafasi ya kufanya ziara ya wiki tatu nchini Marekani ambapo nilitembelea sehemu kibao zikiwemo Washington DC, New Orleans, Los Angeles California, New York, Detroit (Michigan).
“Katika sagfari hiyo, nilipata bahati ya kukutana na wakongwe kibao kunako gemu la kimataifa, nikaweka historia ya aina yake,” anasema Witnesz ambaye kwa sasa amerejea kwa staili nyingine kabisa, Ochuness.
OCHUNESS NI NINI?
“Mwaka 2007 nilikutana na mchizi anaitwa Ochu Sheggy (mtoto wa msanii mkongwe, marehemu Eggy Sheggy) katika studio moja Bongo. Kiukweli tukafanya kazi pamoja mbili tatu lakini baadaye tukafall in love na kuanzisha safari ya kimapenzi.
“Hayakuwa mapenzi tu bali mapenzi na kazi, jamaa naye ni msanii wa kuimba, prodyuza, mchoraji na mwalimu wa sauti. Kwa pamoja tukakubaliana kuanzisha project ambayo itaakuwa ikitushirikisha sote wawili, mimi (Witnesz) na Ochu, tukachagua jina tuliloona linafaa ndiyo Ochuness ikazaliwa ikiwa ni muunganiko wa majina yetu mawili, Ochu na Witness,” alifafanua Witnesz.
UJIO MPYA
“Tayari kunakazi mpya ya Ochuness iitwayo Think About It ambayo audio yake na video vinabamba kinoma kwenye media za ndani na nje ya nchi. Mimi na Ochu tumefanya kazi kubwa sana na kile mtu anayeisikia ngoma hiyo anakubaliana na viwango vya ngoma hiyo.
MKAKATI WA KUSAIDIA CHIPUKIZI
“Ujio wetu mpya umelenga pia kuwasaidia wasanii wanaochipukia ambapo tumeandaa bonge la project iitwayo Rekodi kwa Shilingi Elfu Ishirini ambayo itakuwa endelevu.

“Katika project hiyo, tutakuwa tukiwafanyia usaili wasanii chipukizi ambao watakuwa wakichukua fomu kwetu kila baada ya wiki mbili, baada ya hapo, wale watakaokidhi viwango, tutawaingiza kwenye studio yetu lakini kabla ya hapo watapewa mafunzo ya sauti na Ochu kisha tutawarekodia ngoma mojamoja kwa gharama ya shilingi elfu ishirini tu.
“Hii ni fursa kwa wasanii ambao wana dreams za kuwa mastaa lakini wanakosa njia ya kutokea, nawasihi waje kwa wingi katika ofisi zetu zilizopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam na tunaanza rasmi Julai hii.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...