NOLLYWOOD; NAYA: KAZI KWANZA, MAPENZI BAADAYELagos- Nigeria
Msanii anayefunika kunako kiwanda cha filamu Nollywood, ambaye pia anafanya kazi zake huko Uingereza na Marekani, Beverly Naya, amewatahadharisha wanaume wanaompigia misele kuwa, safari yake ya kutoka Uingereza hadi Lagos Nigeria, ni kwa sababu ya kazi na si mapenzi, hivyo amewatahadharisha wasimsumbue kuhusu mapenzi kwa sasa kwa sababu mpenzi wake mkubwa ni kazi yake.

Mwanadada huyo aliyekulia jijini London, alirejea Nigeria mwaka jana na kushiriki katika movie ya Home in Exile ambayo kwa kiwango kikubwa ilimtambulisha kwenye ulimwengu wa filamu nchini Nigeria. Licha ya kukulia Uingereza, Beverly ana asili ya kutoka Ibuzo, jimboni Delta State huko Nigeria. Beverly ambaye pia ni mwanamitindo, amesema kuwa tangu atue nchini Nigeria mwaka jana, amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume, ambao kila mmoja anamtaka kimapenzi.

No comments:

Post a Comment