Monday, August 9, 2010

CHINA KUFUNGA VIWANDA 2087 KUDHIBITI MATUMIZI YA NISHATI


HONG KONG — Waziri Mkuu wa Jamhuri ya watu wa China, Wen Jiabao ametangaza kuwa serikali yake italazimika kuvifunga viwanda zaidi ya 2087 nchini humo, ili kudhibiti matumizi ya nishati nchini humo. Viwanda vitakavyokumbwa na gahrika hilo ni vile vinavyotumia nishati kubwa, ikiwemo migodi ya Hefei, jimboni Anhui, viwanda vya kufua vyuma, na viwanda vya kutengenezea vifaa vya ujenzi. Hatua hiyo inakuja baada ya China kukabiliwa na tatizola matumizi makubwa ya nishati kuliko uwezo wake wa kuzalisha. China inaongoza duniani kwa kutumia nishati kubwa zaidi kwa siku, ikifuatiwa na Marekani.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...