Saturday, August 28, 2010
LAND ROVER MYSTERY!
Land Rover: Gari maarufu lenye ‘roho ya paka’
• Ni maarufu katika nchi maskini
• Linapita sehemu ‘zisizopitika’
• Lilitengenezwa 1948 Uingereza
JE, unalikumbuka gari aina ya Land Rover hususani lile lililokuwa maarufu kama ‘Series 109’? Kwa wasiolifahamu, gari hilo lililotengenezwa kwa mara ya kwanza nchini Uingereza mwaka 1948 na Rover Company ambayo ilibadili jina baadaye na kuwa Land Rover.
Makao makuu ya kampuni hilo ambalo sasa linamilikiwa na Tata Motors la India ni Gaydon, Warwickshire, Uingereza.
Ni gari lenye uwezo mkubwa kupita maeneo magumu kwani lina uwezo wa kuzizungusha gurudumu zake zote nne na lina gia maalum za kulipitisha sehemu ngumu kama vile kwenye tope au maji mengi.
Land Rover limekuwa na limeendelea kwa miaka mingi kuwa gari muhimu kwa nchi maskini zenye miundo mbinu hafifu ambapo lilikuwa maarufu katika shughuli nyingi za kiserikali hususani katika nchi zilizokuwa zimetawaliwa na Uingereza.
Mbunifu wa gari hilo alichochewa na utendaji wa gari aina ya Jeep (ya Marekani) yalivyokuwa yana uwezo wa kupita katika maeneo magumu, na huo ukawa ujio wa Land Rover ambalo lilizinduliwa Aprili 30, 1948 kwenye Maonyesho ya Magari huko Amsterdam, Uholanzi.
Mbali ya magari ya Jeep, Land Rover ni ya pili miongoni mwa magari yenye kuzungusha gurudumu zote nne (4WD) ambayo yamekuwepo na yanaendelea kuwepo duniani kwa muda mrefu zaidi.
Kampuni la Land Rover ambapo limetoa magari mengi ya aina mbalimbali yakiwemo yale ya Discovery, Freelander, Defender, Ranger Rover, na kadhalika, limepitia kwa wamiliki mbalimbali baada ya Rover Company kati ya 1948 hadi sasa.
Wamiliki hao ni Leyland Motor Corporation, British Leyland Motor Corporation, Rover Group, British Aerospace, BMW, Ford Motor Company ambalo mnamo Juni 2008, liliuza hisa zake kwa Tata Motors.
Kampuni hilo ambalo mwenyekiti wake ni Ratan Tata, lina wafanyakazi 13,000 duniani kote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1
Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...
-
Ni wiki nyingine ambapo mwenyezi Mungu ametujaalia kukutana katika busati letu la mahaba ambapo tunajadiliana mambo mbalimbali yanayohusu ...
-
HASH POWER 7113 NI matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko poa. Ni wiki nyngine tunapokutana kwenye busati letu ambapo tunajuzana na kuja...
No comments:
Post a Comment