Monday, May 10, 2010

TYLOR SWIFT ATOA DOLA 500,000 KUSAIDIA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO


Kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na kusababisha wengine maelfu kukosa makazi, yaliyotokea huko Nashville, mwanadada mwanamuziki na mwanamitindo, Taylor Swift ametoa kitita cha dola za Kimarekani 500,000 kama msaada kwa waathirika wa mafuriko hayo yaliyotokea hivi karibuni. Nashville ndiko Swift anakoishi tangu akiwa na umri wa miaka 14.

“Nilikuwa nyumbani wakati janga hili likitokea. Sikuyaamini macho yangu kwa kile nilichokishuhudia kikiwatokea watu wa nyumbani kwetu, wakiwemo wale niliokuwa nawapenda sana,” aliongea Swift katika ujumbe wa barua pepe alioutuma kwa waandishi wa habari. Na kuongeza, "Nashville ni nyumbani kwetu na najivunia kuwa mkazi wa Nashville. Niko pamoja na wote waliopatwa na janga hili.”

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...