Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, kinatarajia kuendesha utafiti maalum (Research) juu ya tatizo la wanafunzi wengi wa kike kukatisha masomo yao kutokana na kupewa ujauzito. Utafiti huo utahusisha waandishi wa habari, ambao watasafiri hadi mikoani (Tanzania Bara na Visiwani) kwenda kufanya utafiti shule hadi shule, kijiji hadi kijiji, kata, tarafa na wilaya za mikoa iliyochaguliwa, ili kubaini chanzo cha tatizo hilo na kuona kama jitihada za makusudi zinachukuliwa ili kuwanusuru wanafunzi wa kike na ‘mafataki’ wanaowaharabia masomo yao.
1. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Ananilea Nkya akifafanua jambo katika semina ya waandishi wa habari watakaoenda mikoani kufanya utafiti, katika semina fupi iliyofanyika kwenye Ofisi za Tamwa, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
2. Mwezeshaji Nyaronyo Kicheere, akitoa semina juu ya jinsi ya kufanya utafiti kwa waandishi wa habari, leo.
3. Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria semina hiyo.
KAZI NA DAWA
4. Washiriki wakipata kifungua kinywa, wakati wa semina hiyo.
Picha: Hashim Aziz/ GPL.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1
Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...
-
Ni wiki nyingine ambapo mwenyezi Mungu ametujaalia kukutana katika busati letu la mahaba ambapo tunajadiliana mambo mbalimbali yanayohusu ...
-
HASH POWER 7113 NI matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko poa. Ni wiki nyngine tunapokutana kwenye busati letu ambapo tunajuzana na kuja...
No comments:
Post a Comment