Wednesday, May 19, 2010

TO MY VALENTINE -18

. Alitambua moja kwa moja kuwa walepolisi walikuwa wakimtafuta yeye, na sababu ubwa ikiwa ni ugomvi katia ya Nancy na Ritta.
“Mungu wangu, huyu Nancy kazua balaa gani tena mpaka naanza kusakwa na polisi?” Brian alikuwa akijiuliza mwenyewe huku akizidi kutimua mbio.

Baada ya kuhakikisha amefika mbali kabisa, ambako isingekua rahisi kwa polisi kumuona, alitoa simu yake na kumtafuta Nancy hewani.
“Uko wapi Nancy? Kwani kumetokea ini mbona polisi wamekuja nyumbani kwangu?”
“Niko stendi ya mabasi Ubungo nakata tiketi ya kuelekea Arusha leoleo, nilishakwambia kuwa siku nikikutanaa Ritta nitapata murder case, nimetekeleza ahadi yangu.”
“Mbona siwaelewe? Kwani kumetokea nini?”
“Nimemchoma Ritta na kisu, hivi sijui hali yake ikoje. Tutaonana Mungu akipenda,” alijibu Nancy kisha akakata simu.

Brian hakuyaamini masikio yake kusikia Nancy amemchoma kisu Ritta. Kwa jinsi alivyokuwa akimfahamu Nancy, hakuwa katili kiasi cha kushika kisu na kukizamisha mwilini mwa mwezake. Alijikuta akiijuta nafsi yake kwa kushindwa kusuluhisha ugomvi ule wakati alikuwepo eneo la tukio. Lakini zaidi alijikuta akiijutia nafsi yake zaidi kwani yeye ndiyo alikuwa sababu ya yote yale yaliyokuwa yanatokea. Laiti kama asingemsaliti Nancy wake na kuanzisha uhusiano usiofaa na Ritta, yale yote yasingetokea.

Wazo pekee lillomjia akilini mwake ilikuwa ni kumuwahi Nancy
Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, ili akapate picha nzima ya tukio lilivyokuwa, ili hata kama ni kujiteteta mbele ya vyombo vya sheria ajue anaanzia wapi. Alifanikiwa kufika Ubungo muda mfupi baadaye, lakin kwa bahati mbaya, ile anaingia tu kwenye lango kuu, alipishana na basi lililokuwa linatoka kuelekea Arusha. Alipoinua macho yake na kuwatazama wasafiri waliokuwa ndani ya basi lile, macho yake yaligongana na ya Nancy, aliyekuwa akimpungia mkono wa kwaheri huku machozi yakimtirirka mashavuni mwake.

“Bye my Love, if God wishes we shall meet again. Forgive me for what ive done. Its because I love you, bye!” (Kwa heri mpenzi wangu, Mungu akipenda tutaonana tena. Nisamehe kwa yote niliyoyatenda, ni kwa sababu nakupenda, kwaheri!”

ZBrian hakutaka kuyaamini macho yake kuwa ni kweli Nancy alikuwa akiondoka. Alijikuta nguvu zikimuishia na kuanza kutokwa na machozi kama mtoto mdogo anapoagana na mama yake. Alimsindika kwa macho mpaka lile basi lilipopotea kabisa kwenye upeo wa macho yake.

Alihisi kichwa chake kikianza kumgonga kwa nguvu kutokana na mawazo yaliyokuwa yanapita kwa kasi akilini mwake. Hakujua afanye nini kwa wakati ule ili kunusuru hali ya mambo, kwani kama Nancy aliyefanya tukio lile alikuwa ameshakimbia, moja kwa moja yeye ndiye angeangukiwa na jumba bovu la kuisaidia polisi, kitu ambacho hata yeye hakuwa tayari. Aliondoka eneo lile la stendi na kutafuta mahali palipotulia. Alikaa na kauzana kutafakari nini cha kufanya. Akili zake kwa upande mmoja zilikuwa zikimtuma kuwa nay eye atoroke, lakini alipofikiria kazi yake, aliona wazo hilo ni gumu kutekelezeka.

Akil nyinghine ikawa inamtuma kuwa ni bora amtafute Ritta popote alipo, hata kama yuko mahututi akamuombe radhikwa yaliyotokea, na akamuombe wenda kufuta kesi kabla haijafikishwa mahakamani. Japokuwa alitambua wazi kuwa kwenda kumuomba radhi Ritta kungemaanisha kurudiana naye kimapenzi, aliamua kupiga moyo konde.

“Potelea mbali, liwalo na liwe. Mimi ni mwanaume na lazima nioneshe uanaume wangu katika hili.”
Alitoa simu yake ya mkononi na kuitafuta namba ya simu ya rafiki yake Ritta aliyempigia simu awali kumpa taarifa ya uongo kuwa Ritta anaumwa. Aliipiga na ikawa inaita. Iliita mara ya kwanza bila kupokelewa mpaa ikakatika. Hakukata tama, alijua fika kuwa yule rafgiki yake anaogopa kupokea kutokana na vitisho alivyowatolea mchana. Baada ya dakika chache, aliijaribu tena na ikawa inaita.

“Hallow unasemaje?”
“Samahani dada ‘angu, kwanza nisamehe kwa yote yaliyotokea leo. Naomba kuuliza hali ya Ritta na mahali alipo kwa sasa.”
“Ritta yuko hospitali. Hali yake sio nzuri ila madaktari wanajitahidi kumsaidia. Aliumia vibaya begani baada ya yule shetani wako kumchoma na kisu”
“Nieleze tafadhali Hospital aliyolazwa, nataka kuja sasa hivi kumjulia hali”
“Hata usihangaike kuja kwani mpaka sasa suala liko polisi, na wewe na huyo kicheche wako mnasakwa ile mbaya”

Itaendelea wiki ijayo

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...