GENEVIV anaamua kujitoa sadaka kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama yake. Anathubutu kuuweka utu wake rehani kwa kujitumbukiza katika biashara hatari ya uchangudoa. Anajua fika kuwa anachokifanya hakikubaliki mbele ya wanadamu wala mbele ya muumba, lakini kwa kuwa hana msaada wowote kutoka kwa walimwengu, ukizingatia umri wake bado ni mdogo, anaamua kujitoa mhanga kuokoa maisha ya mama yake mpendwa.
Anatumia pesa anazozipata katika biashara yake haramu kumpeleka mama yake hospitali, na baada ya muda mfupi anaanza kupata ahueni.
Upande mwingine aanaendelea kumuasi Muumba wake, huku uzuri wa sili aliojaaliwa ukiwa kama mtaji wenye thamani zaidi ya almasi. Anakuwa mzoefu wa biashara ya uchangudoa, lakini wahenga walisema…Dhambi ikikomaa huzaa mauti…hili linajidhihirisha miezi michache baadae kwa Geneviv baada ya kuanza kuhisi dalili za ujauzito. Kwa kuwa hamjui ni nani hasa aliyempa ujauzito ule, rafiki yake Alice anamshauri wakaitoe bila ya mtu yeyote kushtukia , hasa mama yake, naye anaridhia kwa shingo upande. Je atafanikiwa? Ini kitatokea? Shuka nayo mwenyewe…
Bi Patricia Alitambua kuwa mwanae Geneviv na Alice walikuwa marafiki tangu enzi wakiwa bado wadogo, lakini wakaja kutengana kutokana na Geneviv kuwa bize na shule. Pamoja na hayo alikuwa akizifahamu vizuri tabia za Alice na hasa ile ya uchangudoa. Akaanza kuingiwa na wasiwasi juu ya usalama wa mwanae, hasa baada ya kuona ukaribu wao ukizidi kuimarika siku baada ya siku . Hakutaka kuendelea kuumiza kichwa kwa kumhoji maswali Geneviv kwani alihisi huenda akajikuta akirudi kwenye ugonjwa wake wa moyo. Akawa anangoja apone kabisa ndio akae na binti yake, lakini moyoni alishaanza kuhisi kitu.
Pamoja na hayo alikuwa akijiuliza ni nani aliyemleta kwenye Hospitali ya gharama namna ile ambayo imeokoa maisha yake. Alikuwa bado hajajua kuwa ni jitihada za mwanae kujitoa sadaka ndio zimemfanya apone. Alikuwa akimshukuru zaidi Mungu kwa kumpa nguvu mpya na kumrudishia uhai. Mawazo juu ya kuondokewa na mumewe yalishaanza kupotea na akawa anawaza jinsi atakavyoanza maisha mapya na mwanae Geneviv.
*****
Geneviv na Alice walikuwa wakielekea kwenye Dispensari moja ya uchochoroni iliyokuwa ikisifika kwa kufanya kazi ya utoaji mimba. Machangudoa wote na wanafunzi wa kike waliokuwa wakipata mimba bila kutarajia pale ndio kilikuwa kituo chao cha kufanyia mauaji ya vichanga. Daktari Maguru alikuwa akipata pesa nyingi sana kwa kazi ile haramu. Japokuwa kila mtu alikuwa anafahamu kuhusu kinachofanyika pale, bado hakuna sheria zozote zilizokuwa zinachukuliwa dhidi yake.
Mabinti wengi walikuwa wakipoteza maisha kila uchao wakati wakitolewa ujauzito na wengine walikuwa wakiachwa na vilema vya maisha. Mapigo ya moyo ya Geneviv yalikuwa yakienda mbio kupita kawaida walipokuwa wakiikaribia Dispensari ile. Alice alimshika mkono na wakaingia mpaka ndani ambako walikuta foleni kubwa ya wasichana wengine, nao wakiwa wanasubiri huduma. Kidogo wasiwasi ulipungua baada ya kuona kuwa hakuwa peke yake, na zaidi kulikuwa na wasichana wengi ambao kiumri walikuwa wadogo kwake.
Alibaki akijiuliza bila kupata majibu inakuwaje watoto wadogo kama wale aliokuwa anawaona mle ndani, tena wengi wakiwa ni wanafunzi, walikuwa hawaogopi kufanya dhambi kama ile ambayo yeye aliiona kama mbaya zaidi na ni sawa na kuua kiumbe kisicho na hatia. Baada ya kungoja kwa muda mrefu kwenye foleni, hatimaye zamu yao ya kukutana na daktari Maguru ilifika.
Chumba cha daktari kilikuwa kikitoa harufu kali ya damu kama machinjioni. Kitanda kilikuwa kimeloa damu na hata nguo alizovaa daktari zilikuwa na damu. Kilichomtisha zaidi Geneviv ni vifaa vilivyokuwa vinatumika. Mikasi mikubwa, visu na vyuma vya ajabu-ajabu vilivyokuwa vimetapakaa damu vilimtisha mno.
“Mungu wangu… im finished! Alice mi naondoka, siwezi, siwezii”
Aliongea Geneviv kwa sauti kubwa na akawa anataka kukimbia na kutoka nje. Daktari Maguru alimuwahi na kumrudisha ndani. Alice akaanza ‘kuwaka’ baada ya kuona Geneviv anataka kumwaibisha.
“Ni mara yake ya kwanza etii” Daktari Maguru alimuuliza Alice huku akiwa anasafisha vifaa vyake tayari kwa kumshughulikia Geneviv. Alice aliitikia kwa ishara na wote wakacheka. Geneviv alikuwa akitetemeka kupita kiasi, hakuamini kama angeweza kutoka hai kwenye kile chumba kilichokuwa kinatisha kama machinjioni. Baada ya kumtuliza, daktari Maguru alianza kumhoji maswali machache huku akiendelea kuandaa vifaa vyake na kuvisogeza karibu na kitanda…
“Wenzio wanatoa hata zaidi ya mara nne na bado wanadunda mitaani, itakuwa wewe? Tulia nikufanyie mambo, mimi ndio Maguru mtaalamu mwenyewe, hakiharibiki kitu hapa,” Alikuwa akijisifia yule daktari huku akivaa gloves ndefu tayari kwa kazi. Alimtoa Alice nje na kubaki na Geneviv. Akamuamuru kuvua nguo na kubaki kama alivyozaliwa ili afanye kazi yake vizuri. Kwa kuwa alikuwa na shida, Geneviv alitii amri huku akijificha uso wake kwa aibu.
“Mtoto mzuri huyu sijapata kuona, lazima nimuonje kwanza kabla ya kazi… nikimuachia watanicheka sana.” Daktari Maguru alikuwa akijisemea kimoyomoyo huku udenda ukimtoka. Ikabidi atumie mbinu uchwara za kidaktari kumuweka sawa Geneviv. Alimdanganya kuwa njia yake ilikuwa ndogo hivyo ilikuwa ni lazime ailainishe kwa kumuingilia ndio aendelee na kazi. Geneviv hakuwa mbishi, akamuacha afanye anachokitaka mradi mimba itoke. Baada ya kumfaidi bila huruma, Daktari Maguru aliendelea na kazi yake. Muda mfupi baadae alikuwa ameshamaliza kazi. Akafungua mlango na kumuita Alice aje amchukue rafiki yake.
“Pole shosti huo ndio ukubwa. Ulikuwa unaogopa nini,mbona hujafa sasa!” alikuwa akiongea Alice kwa masihara hali iliyozidi kumkasirisha Geneviv. Alikuwa akisikia maumivu makali kupita kiasi. Akajikaza na kushuka kitandani, Alice akamshika mabegani na kuuzungusha mkono mwingine kiunoni, wakawa wanatoka huku Geneviv akichechemea. Walipofika nje ilibidi wakodi taksi kwani Geneviv alishindwa kabisa kutembea. Ikawapeleka mpaka kwa Alice ambako baada ya kufika tu, Alice alimchemshia maji ya moto na kuanza kumkanda. Geneviv alikuwa akilia sana kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia.
***
Je nini Kitaendelea? Usikose wiki ijayo…
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1
Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...
-
Ni wiki nyingine ambapo mwenyezi Mungu ametujaalia kukutana katika busati letu la mahaba ambapo tunajadiliana mambo mbalimbali yanayohusu ...
-
HASH POWER 7113 NI matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko poa. Ni wiki nyngine tunapokutana kwenye busati letu ambapo tunajuzana na kuja...
No comments:
Post a Comment