Monday, May 10, 2010

LIL WAYNE AMTUMIA MAMA YAKE UJUMBE MAALUM KUTOKA JELA


Wiki kadhaa baada ya kutuma waraka wa kwanza kutoka jela, msanii anayetumikia kifungo Jela, Lil Wayne ametuma barua nyingine, na tofauti nay a kwanza, hii ameidedicate kwa mama yake mzazi. Barua hiyo imetumwa kutoka jela siku ya Mei 7, ambayo ni maadhimisho ya siku ya kina mama duniani. Katika barua hiyo, Lil Wayne ameshow love kichizi kwa mama yake mzazi.
“Kwangu mimi, thamani yako mama ni kubwa kiasi cha kutoelezeka. Dhumuni kubwa ya kukuandikia siku ya leo, ni kukuonesha upendo hususan katika siku ya kina mama ambayo inasherekewa leo dunia nzima,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
Japokuwa amefungwa jela, Lil Wayne bado anawasiliana mara kwa mara na watu wake wa karibu na mashabiki wake dunia nzima kwa njia ya mtandao wa internet.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...