Na Hashim Aziz
Wengi wamezoea kuiona picha yake kama
alama ya ukombozi na mapinduzi ya kweli lakini ni wachache wanaomjua vizuri.
Jina lake halisi anaitwa Ernesto ‘Che’ Guevara, alizaliwa Juni 14, 1928,
Rosario, Argentina na yafuatayo ni mambo kumi kumhusu:
1. Alikuwa mwanaharakati na
mwanamapinduzi aliyezisaidia nchi nyingi kupata uhuru kupitia vita vya msituni,
zikiwemo Cuba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji na nyingine nyingi.
Ernesto Che Guevara |
2. Licha
ya kusumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu, aliweza kusafiri sehemu mbalimbali,
zikiwemo zenye baridi kali na kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kuwasaidia
wanyonge.
3. Alisomea udaktari katika Chuo Kikuu
cha Buenos Aires alikohitimu na kupata digrii (shahada) ya udaktari wa binadamu.
4. Akiwa bado anasomea udaktari,
alifunga safari kwa kutumia pikipiki ambapo alisafiri umbali wa kilometa 4,500
na baadaye kilometa nyingine 8,000 kutembelea nchi mbalimbali za Amerika ya
Kusini. Hali ya umaskini na ukandamizaji aliyoikuta huko ndiyo iliyomfanya awe
mpiganaji wa msituni.
5. Harakati za kwanza za kimapinduzi
zilizompa umaarufu, ni pale alipomsaidia Fidel Castro wa Cuba kumpindua Dikteta
Fulgencio Batista wa nchi hiyo kupitia vita vya msituni akiwa mkuu wa jeshi.
6. Amewahi kufika Dar es Salaam mwaka
1966 ambapo alikutana na wapigania uhuru wa Msumbiji, Frelimo na kukubaliana
kusaidiana kupigania uhuru wa nchi hiyo.
7. Baadaye aliondoka Afrika na
kuelekea Bolivia kuendelea na harakati za kumtoa madarakani kiongozi aliyekuwa
akitawala kimabavu nchi hiyo, René Barrientos ambapo aliunda jeshi la porini
kwa ajili ya kumpindua lakini ikashindikana.
8. Baada ya kushindwa kwa mapinduzi ya
Bolivia, Che Guevara alikamatwa eneo liitwalo Yuro baada ya kuzingirwa na
wanajeshi wa Bolivia.
9. Baada ya kukamatwa kwake, aliteswa
sana na siku chache baadaye akauawa kwa kupigwa risasi nyingi na mwanajeshi
mlevi aitwaye Mario Terán.
10. Kufuatia kifo chake, mataifa mengi
duniani yalitangaza siku kadhaa za maombolezo, ikiwemo Cuba ambapo Fidel Castro
alitangaza siku tatu za maombolezo.
aendelee kupumzika kwa amani che guevara
ReplyDeletekamwe hawezi sahaulika mioyoni mwetu.
Kusudi tuliloletewa duniani huwa ni gumu na wengi huwa wanabadilika wanaogopa na wanasahaulika Leo Leo.
ReplyDelete