Timu
ya soka ya Simba, imemtimua kazi aliyekuwa kocha wa timu
hiyo, Mzambia Patrick Phiri pamoja na msaidizi wake, Suleiman Matola kufuatia matokeo mabovu ambayo timu hiyo imeendelea kuyapata.
Phiri aliwahi kuwa kocha wa klabu hiyo mnamo mwaka 2003-2005 kabla hajaondoka na kurudi kwao Zambia kuifundisha timu yake ya taifa mnamo 2005-2008 baada ya hapo alirejea tena kuinoa Simba 2008-2011 kabla hajatimuliwa kwa mara nyingine tena. Phiri atakumbukwa kwa mengi sana ikiwemo ya kucheza ligi kuu bila ya kufungwa hata mechi moja rekodi aliyoiweka mwaka 2010-2011.
Kutimuliwa kwa Phiri kunakuja siku chache baada ya kutimuliwa kwa kocha wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo.