Tuesday, September 7, 2010

MY HEART IS BLEEDING!

Baada ya kukaa kwa muda mrefu ndani ya kisiwa cha Zanzibar, Khaleed anapanga mikakati madhubuti ya namna ya kurudi nchini kwao, kwa ajili ya kazi moja tu! Kulipa kisasi cha damu kwa wote waliohusika na mauaji ya ndugu zake bila ya hatia.

Ilikuwa ni lazima arudi nyumbani kwao kulipa kisasi kwani damu ya ndugu zake iliyomwagika bila ya hatia ilikuwa ikimuandama muda wote, na tayari alishajiapiza tangu kipindi, kuwa lazima alipe kisasi.
‘I must revenge! The blood revenge to whoever may concern.”

Licha ya kuwa tayari Khaleed alikuwa ameanza ukurasa mpya wa maisha , hasa baada ya wazazi wake wote kufariki dunia, bado aliamini hakuna kitu ambacho kingeweza kuziba pengo la wazazi wake hapa duniani. Ni hali hii ndiyo iliyomfanya apitie mateso makubwa sana duniani kabla ya Mungu kumbariki kwa kumuangazia nuru ya maisha alipokuwa huko machimboni Mererani, alikofanikiwa kuondoka na jiwe kubwa la madini ya tanzanite, madini ambayo kwa kiasi kikubwa yaliyabadilisha maisha yake, kutoka maisha ya uchokoraa hadi kufikia kuwa milionea mtoto.



Aliendela kukaa ndani ya visiwa vya Zanzibar, kwenye hoteli moja ya kifahari iliyokuwa pembezoni mwa bahari ya hindi. Aliendelea kukaa pale kwa wiki kadhaa akiumiza kichwa namna atakavyoitekeleza operesheni aliyoipa jina la ‘Blood revenge 7113’. Muda wa jioni alikuwa akitoka na kwenda kukaa peke yake ufukweni, akiwa na kijitabu chake kidogo (Note book) akiandika kila kitu kuhusu namna ambavyo angeendesha kazi ile kubwa iliyokuwa mbele yake.

Pesa kibao alizozipata baada ya kuuza madini ya Tanzanite, zilitosha kumfanya aishi maisha aliyoyataka aliendelea kusuka mipango kwa umakini wa hali ya juu ili kuhakiksha anakamilisha zoezi lile gumu na la hatari bila ya kushtukiwa. Alikuwa akiandika majina ya watu wote waliohusuka kuiangamiza familia yao, akianza na mashetani watatu wa kundi hatari la wafanya biashara wa Holly Trinity. Aliandika majina yao kwenye kijitabu chake cheusi, akitumia kalamu nyekundu.

Aliwaandika pia watu wote walioshirikiana na The Holly Trinity, kuanzia na kamanda mkuu wa polisi wa kanda maalum, Luteni Lauden Kambi ‘Fuvu’ ambaye hkaleed alikuwa akiamini kuwa ameshiriki kwa kiwango kikubwa kwani kama angeifanyia kazi taarifa ya mapema iliyotolewa na wazazi wake, yale yote yasingetokea. Aliwaandika pia watu wengine wengi ambao kwa pamoja walitengeneza orodha ndefu ya watu ambao walikuwa wakistahili kufa kwa mikono yake.
“They deserve to die f*c them to hell” (Wanastahili kufa mashetani hawa), Khaleed aliongea kwa sauti ya juu wakati akiitazama upya ile orodha yake.

Kwa kuwa aliongea kwa sauti ya juu, bila kujua kuwa kulikuwa na mtu aliyekuwa amekaa jirani yake, ilibidi aanze kuvunga akiwa na lengo la kupindisha ukweli kwani hakutaka mtu yeyote ajue kuwa alikuwa akiandaa mikakati kabambe ya kuua. Jirani na pale alipokuwa amekaa, pembeni alikuwa amekaa binti mmoja, ambaye kiumri walikuwa wakishabihiana na Khaleed. Kauli ile ya Khaleed “They deserve to die…’ Ilimshtua sana kiasi cha kugeuza sura yake kuelekea pale Hkaneed alipokuwa amekaa.

Aliendelea kumtazama lakini Khaleed alikuwa akijitahidi kupoteza mada baada ya kugundua kuwa alikuwa amefanya kosa kuropoka kwa sauti bila ya kujua kuwa kulikuwa na mtu pembeni yake pale ufukweni, kando ya hoteli ya kifahari aliyokuwa amefikia. Aliendelea kupunga upepo wa baharini huku mawazo mengi yakipishana akilini mwake. Yule binti aliendelea kumtazama Hkaleed kwa jicho la kumsoma, lakini Khaleed alijifanya hana habari naye.

Baada ya kuona yule binti akizidi kumtazama, Khaleed aliinuka na kuondoka pale alipokuwa amekaa na kuanza kurudi kwenye hoteli aliyokuwa amefikia. Hakutaka hata kumtazama usoni. Alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake alikofikia ambapo alijitupa juu ya kitanda na kujilaza, huku mawazo yakizidi kupishana akilini mwake.

Kwa kadri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, ndivyo hamu ya kulipa kisasi ilivyokuwa ikizidi kuongezeka akilini mwa Khaleed. Baaada ya kukaa kwa zaidi ya wiki tatu pale kisiwani Zanzibar, kwenye Hoteli ya kifahari aliyokuwa amefikia, safari ya kurudi nyumbani kwao Blazinia ilikuwa imekamilika. Maandalizi yote muhimu yalikuwa yamekamilika na sasa alikuwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza rasmi kazi yake, kazi ya kulipa kisasi cha damu.

Ikiwa ni jioni ya mwisho aliyopanga kukaa kisiwani Zanzibar, Khaleed alitoka na kwenda ufukweni kama kawaida yake, safari hii akiwa na matumaini makubwa kuwa hatimaye kazi nzito iliyokuwa mbele yake alikuwa akienda kuikamilisha. Jioni hii alionekana kuwa mchangamfu kuliko siku zote alizokaa pale hotelini. Furaha yake ilitokana na ukweli kwamba karibu taratibu zote zilikuwa zimekamilika na kilichokuwa kimesalia ilikuwa ni utekelezaji tu. Alitoka na kwenda moja kwa moja kukaa ufukweni kupunga upepo huku akichezea mchanga wa baharini.

Alikuwa akijaribu kukumbuka kila kitu kilichotokea maishani mwake mpaka akajikuta akiwa mpweke chini ya jua, akiwa hana ndugu hata mmoja aliyesalia akiwa hai. Alikumbuka kila kitu kuanzia siku ya kwanza jinamizi la mikosi lilipoanza kuiandama familia yao, akakumbuka kila kilichoendelea baada ya hapo mpaka muda ule akiwa pale ufukweni.

Kumbukumbu mbaya zilizokuwa zikipita kwa kasi ndani ya ubongo wake zilimuongeza uchungu mtimani, na akajikuta akianza kutokwa na machozi, hasa alipomkumbuka mama yake mzazi na jinsi alivyouliwa kikatili kwa kuchomwa sindano ya sumu na kumfia mikononi mwake.

Alikumbuka pia jinsi baba yake alivyouliwa kikatili kwa kupigwa risasi mbele ya macho yake, akiwa na kaka yake wa hiyari, Girbons, wakati wakijaribu kutoroka. Picha za matukio ya wadogo zake walioliwa na simba wa Gamutu usiku wa siku ya kwanza walipotekwa kutoka nyumbani kwao usiku wa manane, na mwisho kumbukumbu za kaka yake mwenye ulemavu wa ngozi ambaye mpaka muda huo alikuwa akiamini kuwa tayari ni marehemu… alishindwa kuyazuia machozi yasiuloanishe uso wake, moyo wake ulikuwa ukivuja damu.

Khaleed akijikuta akizama kwenye dimbwi zito la mawazo na hisia za maumivu makali zilizokuwa zikiuchoma mtima wake kiasi cha kutosikia wala kuona kuwa kuna mtu alikuwa akimsogelea. Alitoa kitambaa chake cha mfukoni (handkerchief) na akawa anafuta machozi, ambayo sasa yalikuwa yameuloanisha uso wake wote.

“kaka habari yako!”, Khaleed alisikia sauti laini ya kike ikimsabahi kutoka nyuma yake, lakini kutokana na halialiyokuwa nayo, hakuitikia salamu ile, na akawa anazidi kujifuta machozi.
“Kaka nakusalimu! Mbona kimya”, yule binti alirudia salamu yake na akawa anahoji kwa nini Khaleed alikuwa haitikii salamu yake. Alimsogelea kwa jirani zaidi na ndipo alipogundua kuwa alikuwa amezama kwenye hisia zilizoonekana kuuchoma moyo wake.

“Jamani pole kaka’angu, it seems you got serious problem, can I help you?” ( Inaonekana una matatizo makubwa! Naweza kukusaidia?) yule binti aliuliza kwa sauti ndogo ya upole huku akimgusa begani Khaleed. Kwa kifupi Khaleed alikuwa katika wakati mgumu sana kiasi ambacho aliona kama ni usumbufu mkubwa kwa mtu mwingine kuja kumvurugia utulivu wake, alihitaji kuwa peke yake. Alimgeukia na macho yao yakagongana. Alikuwa ni yule binti ambaye siku chache zilizopita walikuwa wamekaa jirani palepale beach ingawa hakuna ambaye alimsemesha mwenzake.

Khaleed na yule binti waliendelea kutazamana kwa dakika kadhaa bila ya kusemeshana chochote. Yule binti aliuvunja ukimya kwa kurudia kumuuliza Khaleed kama angeweza kuhutaji msaada wake.
“ Can I help you?”, aliuliza tena yule binti kwa sauti ya upole na yenye kubembeleza kanini Khaleed akaitikia kwa kichwa kuonesha kuwa alikuwa haitaji msaada wake.

Khaleed aliinuka na kuanza kuelekea kwenye hoteli aliyokuwa amefikia, akimuacha yule binti ameduwaa kwa mshangao huku akimuonea huruma. Hakugeuka nyuma mpaka aliopotelea ndani ya hoteli ya kisasa aliyokuwa amefikia kwa takribani wiki tatu sasa, tangu alipowasiri kutoka machimboni Mererani, huko Arusha Tanzania. Yule binti alimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kabisa kwenye upeo wa macho yake.
*******
Ndani ya chumba cha hoteli ya kimataifa ya Isles Sand Resort, Khaleed alikuwa akipanga zana zake kwa ajili ya kuanza rasmi kazi yake ya kulipa kisasi, ambayo alikuwa amepanga aianze siku iliyokuwa ikifuata. Alikuwa akipanga vitu vyake vichache ndani ya mkoba wake mdogo wa rangi nyeusi.

Miongoni mwa vitu alivyokuwa anavimiliki, ilikuwepo bastola ndogo aliyofanikiwa kutoroka nayo kutoka mikononi mwa jambazi hatari huko Arusha Tanzania, aliyekuwa akifanya kazi hatari ya kuteka magari yanayosafirisha madini na vito vya thamani kutoka kwenye machimbo ya Tanzanite, huko Mererani.

“Hii itanisaidia sana! Where a metal must meet a meat” Aliongea Khaleed akimaanisha kuwa lazima risasi za mashine ile ndogo zikutane na nyama za wabaya wao.

Licha ya bastola, alikuwa na kichupa kidogo kilichokuwa ndani ya Kiboksi cheusi kilichokuwa na maandishi mekundu yaliyosomeka, ‘Ampethamine cyanide serum’. Kwa haraka alikikumbuka kiboksi kile na akakumbuka jinsi alivyokipata. Alikuwa amemuibia yule jambazi aliyemteka wakati akitoka Mererani, ambaye baadae aligeuka na kuwa rafiki yake akimtaka Khaleed aungane naye kwenye kazi yake ya ujambazi.

Alipokuwa akimuonesha vifaa vyake vya kufanyia kazi, alimuonesha pia na kile kichupa na akamueleza kuwa ile ni sumu hatari sana ambayo huchanganywa kwenye aina Fulani ya pafyumu, na inapopulizwa hewani na binadamu kuvuta hewa yake, ilikuwa ikifanya kazi katika hali ya kutisha sana. Alimpa maelekezo ya namna ya kuichanganya sumu ile na aina ya manukato yenye kemikali iitwayo “Dopamine Venule rapture” ambapo kwa pamoja mchanganyiko huo ulikuwa ukitengeneza sumu kali sana iitwayo ‘Mankind Homocidal Perfume’.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...