Tuesday, September 7, 2010

MAZOEZI YA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME (PHYSIOTHERAPY FOR MALE IMPOTENCE)

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ambayo mwanaume au mvulana anapungukiwa au kukosa kabisa nguvu za kusimamisha viungo vyake wakati wa tendo la kujamiiana. Pia inaweza kuwa ni hali ya mwanaume kuwahi kumaliza wakati wa tendo, au kuwa na nguvu hafifu.Utafiti unaonyesha kuwa Wanaume wengi duniani wanasumbuliwa na tatizo hili ingawa hakuna uwazi wa kutosha wa kulielezea tatizo lenyewe.

Idadi kubwa ya wanaume wana nguvu ndogo, nguvu ambayo haikidhi matakwa ya wenzi au wake zao, huku idadi nyingine kubwa wakiwa hawana kabisa nguvu hata kidogo. Inaelezwa kuwa tatizo hili limepelekea ndoa nyingi kuvurugika na limesababisha maumivu makubwa kwa watu ambao wako kwenye uhusiano.

Watafiti wa mambo ya mahusiano na mapenzi wamejaribu kutafuta vyanzo mbalimbali vya tatizo hili na mbinu za namna ya kulitatua. Licha ya kiusababisha ndoa yingi kuvurugika inaelezwa kuwa tatizo hili limepunguza kwa kiwango kikubwa uwezo wa wanaume kujiamini na kushusha ufanisi wao majumbani mwao na sehemu za kazi.


Watafiti mbalimbali wamejaribu kwa miaka mingi kutafuta tiba ya kudumu ya tatizo hili. Miongoni mwa watafiti ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwarudishia wanaume uwezo wao, ni Daktari Arnold Kegel. Daktari huyu aligundua aina ya mazoezi ambayo yamethibitishwa ulimwenguni kote kuwa na uwezo mkubwa wa kumrudishia mwanaume nguvu zake, hata yule ambaye hakuwa nazo kabisa ( hanithi).
Mazoezi hayo yamepewa jina la mgunduzi wake na yanafahamika duniani kote kwa jina la Kegel.

KEGEL NI NINI?
Kama nilivyoeleza , haya ni mazoezi maalum ambayo huhusisha misuli ya Pelvic inayopatikana kwenye eneo lililozunguka viungo vya uzazi vya mwanaume, kwa upande wa ndani wa mwili.
Mazoezi ya Kegel huhusisha kuibana na kuiachia misuli hii kwa utaratibu maalum, hivyo kuiongezea uwezo a kutanuka na kuwa na nguvu kubwa.

Namna ya kuanza kufanya mazoezi haya ni kwanza kutambua mahali ilipo misuli inayotakiwa kufanyishwa mazoezi. Hili linawezekana kwa kujibana haja ndogo kila unapokwenda kujisaidia.Jibane kwa nguvu kuzuia haja ndogo na wakati huohuo kuwa makini kuigundua misuli inayojibana. Rudia zoezi hili kwa mpaka wiki moja mpaka uhakikishe umeitambua vizuri misuli yako. Ni misuli hiyohiyo ndiyo inayohusika na nguvu za kiume.

Ukishaifahamu vizuri misuli yako, anza kwa kuifanyisha mazoezi kama ifuatavyo:
-Hakikisha huna haja ndogo hata kidogo. Simama wima au kaa kwenye kiti na utulie kabisa. Jifanye kama umebanwa na haja ndogo na kubwa kwa wakati mmoja na uko mbali na choo. Jibane kwa kadri ya nguvu zako zote ukiwa kama unazuia haja zisikutoke, Kisha hesabu mpaka tano (Sekunde tano) ukiwa umejibana, kisha jiachie na urudi katika hali yako ya kawaida.



Rudia zoezi la hapo juu kwa kufuatisha mzunguko wa kujibana kwa sekunde tano na kujiachia. Rudia kwa dakika zisizopungua tano kwa mara ya kwanza. Fanya zoezi hili mara mbili kila siku kwa muda maalum ulioupanga na endelea kuongeza muda wa kufanya mazoezi kwa kadri ya nguvu zako zitakavyokuwa zinaongezeka.

Utashangaa kuona kuwa baada ya muda wa takribani wiki sita hadi miezi mitatu tangu uanze kufanya mazoezi haya rahisi, nguvu zako zitaongezeka kwa kiasi ambacho hukutegemea na utakuwa na nafasi nzuri ya kukidhi haja za mkeo au mpenzi wako. Kumbuka kuwa ukishazoea namna ya kufanya mazoezi haya unaweza kuyafanya mahali popote, wakati wowote bila ya mtu mwingine kufahamu unachokifanya.


Angalizo
Mazoezi haya ni kwa wanaume wenye umri wa kuanzia miaka kumi na nane.

Unapaswa kuanza taratibu kufanya mazoezi haya, na uongeze taratibu kadri siku zinavyoenda. Epuka kufanya kwa muda mrefu hatika siku za mwanzoni.

Mazoezi haya hayana athari zozote kwa afya ya mtumiaji kwani hutumii dawa

2 comments:

  1. je kwa kipindi hicho cha mazoezi naruhusiwa kufanya mapenzi?

    ReplyDelete
  2. samahani administrator nadhani unahaja ya kupiti a marejeo zaidi kutoka kwa mgunduzi wa zoezi hili ambaye ni Dr. Arnold H. Kegel Mwaka 1940 mtaalamu wa magonjwa ya wanawake alitembelewa na mgonjwa aliyejulikana kwa jina la Doris Wilson.

    Huyu mama alikuwa na tatizo baada ya kuzaa mtoto wake wa tatu ilikuwa kwamba kila kibofu chake cha mkojo kikijaa tu basi akicheka tu, au akikohoa tu, au akiruka tu ghafla mikojo anaanza kuchuruzika yenyewe bila uwezo wa kuizuia. Hivyo alianza kuvaa pad ili kujizuia na mikojo tatizo ambalo lilimpeleka kwa Dr. Kegel.
    Kutokana na uchunguzi wa Dr. Kegel aligundua kwamba tatizo lake linasababishwa na kulegea kwa misuli inayozuia mikojo isitoke bila matatizo na hivyo alihitaji upasuaji.
    Lakini kabla ya kufanya upasuaji alimshauri afanye mazoezi ya kuimarisha hiyo misuli iliyokuwa dhaifu.

    UNAPOFANYA ZOEZI HILI NAVYO JUA LAZIMA MKOJO UWE NAO NA SI UFANYE UKIWA HUJABANWA NA MKOJO KISHA UNAFUATA HATUA ZINGINE KAMA ULIVYO ELEZA IF AM NOT MISTAKEN.

    ReplyDelete

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...