Sunday, October 11, 2009


JAY Z NA SHAMPENI BORA KULIKO ZOTE DUNIANI
Mkali wa Hip hop duniani kutoka jijini New York Marekani, Shawn Carter jay Z, hivi karibuni amezindua kinywaji cha shampeni iitwayo Armand de Brignac, shampeni inayodhaniwa kuwa bora kuliko zote ulimwenguni kwa sasa.
Kwa mujibu wa vipimo vya kitaalamu vilivyofanywa na wataalamu zaidi ya watatu kwa nyakati tofauti, Shampeni ya Armand de Brignac, imegunduliwa kuwa na ubora wa hali ya juu, na imeshika namba moja katika chati ya vinywaji bora zaidi duniani.
“Imepimwa zaidi ya mara moja, na kurudiwa tena na tena, lakini bado imeonekana kuwa bora wa asilimia 100…nafurahia sana mafanikio haya”,
Jay Z alikuwa akiielezea na kuinadi Shampeni hiyo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio huko New York
Mafanikio hayo makubwa anayoyapata mkali jay z yamekuja siku chache baada ya kuzindua albamu yake mpya iitwayo ambayo nayo inaonekana kuwa albamu kali zaidi ya HipHop. Hakika huu ni muda wa mafanikio ya juu kwa Jay Z.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...