Sunday, October 11, 2009
MTV AFRICA MUSIC AWARDS 2009
YALIYOJIRI MTV AWARDS NAIROBI…
AY, SHAA WATOKA BILA-BILA
NAMELESS, AMANI, M.I, D’BANJ WANG’ARA
Hatimaye lile tukio lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa la utoaji wa tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMA), limefanyika usiku wa Jumamosi tarehe 10, Oktoba 2009 huko jijini Nairobi, katika ukumbi wa Moi International Sports Complex, Kasarani, nchini Kenya, huku wawakilishi wa Tanzania katika Tuzo hizo, Ambwene Yessaya ‘AY’ na Sara Kais ‘Shaa’ wakiambulia patupu baada ya kushindwa kuondoka na tuzo hata moja.
Katika event hiyo iliyowakutanisha mastaa kibao kutoka mamtoni na Afrika, wasanii Nameless (Kenya) na M.I. (Nigeria) wameng’ara vilivyo baada ya kila mmoja kunyakua tuzo mbili kwa mpigo. Nameless amechukua tuzo ya Msanii bora wa kiume (Best Male artist) na tuzo ya chaguo la wasikilizaji (Listener’s Choice), wakati M.I. ameondoka na tuzo ya Msanii bora anayechipukia na tuzo ya msanii Bora wa HipHop.
Tuzo ya msanii bora wa kike kwa mara ya pili mfululizo imebakia nchini Kenya kwa Msanii Amani baada ya mwaka jana kuchukuliwa na Wahu (Kenya) huko Abuja Nigeria. Tuzo ya msanii bora wa RnB imeenda kwa Darey Art Alade (Nigeria), Tuzo ya msanii bora wa mwaka imechukuliwa na D’Banj( Nigeria) hii ikiwa ni mara ya tatu kwa D’ Banj kuibuka kidedea kufuatia mwaka jana kunyakua tuzo mbili kwa mpigo na mwaka juzi 2007 kunyakua tuzo ya MTV Europe Music Awards.
Tuzo ya kundi bora imeenda kwa P Square (Nigeria), wakati msanii Samini (Ghana) amenyakua tuzo ya msanii anayefanya shoo kali jukwaani (Best Performer).Wengine waliong’ara ni Lucky Dube (South Africa) aliyetunukiwa tuzo ya Heshima, HHP (Soth Africa) tuzo ya Video bora na kundi la Zebra & Giraffe( South Africa) wamechukua tuzo ya wasanii mbadala. Tuzo ya MY VIDEO imechukuliwa na Patricke-Stevie Moungondo (Congo Brazzaville)
Ma-entertainer wa sherehe hiyo waliwapagawisha vcilivyo mashabiki waliohudhuria, wakiongozwa na Wyclef Jean aliyefanya kweli na single yake inayofunika mbaya ‘Sweetest Girl’, na nyingine za ‘No Woman No Cry‘ na ‘Ready or Not’. Msanii wa kimataifa kutoka nchini Senegal, Aliaune Badara “Akon” aliwapagawisha mashabiki na ngoma yake ya Beautiful, na kuzipendesha vilivyo sherehe za utoaji wa tuzo hizo chini ya mtandao wa Zain. Wengine waliopata nafasi ya kuburudisha jukwaani ni Wahu, M.I., Samini, HHP, Da L.E.S, Zebra & Giraffe, Lizha James, STL, Amani, Nameless, A.Y., Lira, 2FACE na Blu3.
Naye Dr Saad Al Barrak, bosi (CEO) wa kampuni ya Zain, ambayo ilikuwa mdhamini mwenza wa tuzo za MAMA, aliilezea event hiyo kuwa imekuwa ya muhimu sana kuvumbua vipaji vikubwa vya waafrika na kuwatangaza katika soko la muziki dunia nzima.
“Tumeamua kudhamini shughuli hii muhimu sana kwa waafrika wote, na kwa kufanya hivi tumelifanya bara letu litambulike na kuheshimika dunia nzima”, alikaririwa Dr Saad.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1
Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...
-
Ni wiki nyingine ambapo mwenyezi Mungu ametujaalia kukutana katika busati letu la mahaba ambapo tunajadiliana mambo mbalimbali yanayohusu ...
-
HASH POWER 7113 NI matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko poa. Ni wiki nyngine tunapokutana kwenye busati letu ambapo tunajuzana na kuja...
No comments:
Post a Comment