SHED NO MORE TEARS GENEVIV… USILIE TENA GENEVIV
Na Aziz Hashim-Hash power
UTANGULIZI
Geneviv ni binti mdogo ambaye amezaliwa katika familia yenye maisha mazuri sana.Mungu amemjaalia kuwa na sura nzuri yenye mvuto.Bahati mbaya kuzaliwa kwake akiwa na sura nzuri na urembo usio na kifani kunamfanya apate mateso makubwa sana kutoka kwa wanaume ambao kila mmoja akiwemo hata baba yake mzazi wanamtumia kimapenzi na baadae kumuacha akipata mateso makubwa mno.
Uzuri ambao Mungu alimjaalia unageuka kuwa sumu kali ambayo inammaliza taratibu mpaka anakaribia kupoteza uhai wake, akiwa katika hatua za mwisho kabisa za uhai wake.Ni mateso,maumivu, machozi,majeraha mtimani na kilio ndivyo vinavyotawala maisha yake.Anaichukia dunia,anawachukia wanaume…hawezi kulipa kisasi,anachoweza kufanya ni kutoa machozi muda wote,analia lakini hakuna anayemsikia! Anapokaribia kukata pumzi anasikia sauti ikimfariji…Shed no more tears Geneviv!
Ungana nami ufahamu mkasa mzima
SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ni alfajiri tulivu,miale ya jua ikianza kuchomoza kwa mbali kuashiria mwanzo wa siku mpya,siku ya jumatatu.Milio ya ndege wa angani waliokuwa wakiimba na kurukaruka kutoka tawi moja hadi tawi jingine juu ya miti waliufanya mwanzo wa siku uwe wakuvutia sana.Jua lilikuwa likizidi kuchomoza huku nuru yake ikilifukuzia mbali giza la alfajiri.Wakati kukizidi kupambazuka,upande wa pili alikuwepo binti mdogo aliyekuwa amejilaza chini ya mti mkubwa,mahali ambapo yamekuwa makazi yake kwa muda mrefu sasa,akishinda kutwa nzima akiwa amejilaza chini kivulini na giza likiingia alikuwa akilala na kujifunika kipande cha gunia palepale mpaka asubuhi.Mwili wake wote ulikuwa umejawa na vidonda vilivyokuwa vinatoa usaha na kumsababishia maumivu makali kupita kiasi.Harufu kali ya majeraha yaliyokuwa yakiendelea kuuozesha mwili wake na harufu ya haja kubwa aliyokuwa anajisaidia hapo hapo, vilipafanya pale chini ya mti panuke mithili ya mzoga wa mnyama aliyejifia.
Binti yule mdogo hakuwa na msaada wowote,hakuweza hata kuinuka kutoka pale chini alipokuwa amelala…alichoweza ilikuwa ni kufumba na kufumbua macho na kufukuza nzi waliokuwa wakivizonga vidonda vyake.Alishakata tamaa ya kuishi na alionekana kama anayengojea pumzi yake ya mwisho ikatike aondokane na mateso makali yaliyokuwa yanamuandama.Kwake maisha yalipoteza maana kabisa,aliichukia dunia na vyote vilivyomo ndani yake.Mara kwa mara alikuwa akimkufuru Muumba wake kwa kumsababishia mateso makali kiasi kile kwani aliamini anateseka kwa sababu Mungu alimuumba akiwa mrembo kupita kiasi. Aliamini anapata mateso makali kiasi kile kwa sababu ya uzuri wake aliopendelewa na Mungu,na huo ndio ulikuwa ukweli.Miaka michache tu aliyoishi duniani ilikuwa ni kama karne nzima kwani alipitia mateso makubwa sana ambayo kama angepata nafasi ya kuusimulia ulimwengu hakika kila mtu angemwonea huruma na kudondosha machozi.Aliendelea kuwaza akiwa amelala pale chini huku macho yake yakilitazama jua lililokuwa linazidi kuchomoza na kuanza kuwa kali.
Dunia aliiona kama shimo la hewa na zaidi aliwachukia wanaume.Aliapa kuwa kama angepata nafasi ya kulipa kisasi,angewateketeza wanaume wote duniani.Aliamini wanaume ni mashetani kwa waliyomfanyia na akazidi kukufuru dini kwa kumlaumu Mungu kwa kuwaumba wanaume.
“ I hate the world,I hate men…”
alijisemea Geneviv pale chini alipolala kwa sauti ya kunong’ona.
Kumbukumbu zake zilimrudisha nyuma alipokuwa bado mdogo.
Aliyakumbuka maisha ya furaha aliyoishi na familia yake kabla mambo hayajaanza kubadilika.Alishindwa kuyazuia machozi ambayo yalianza kuuloanisha uso wake mchanga uliochakazwa na mateso… soo many tears…hakika alitia huruma.
Geneviv alikuwa ni mtoto wa kipekee kwenye familia ya mzee Manuel Rwakatare na Bi. Patricia mahiza.Alizaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa kifedha, baba yake akiwa ni Afisa utumishi katika wizara ya Madini na nishati huku mama yake akiwa Katibu Muhtasi katika ofisi ya waziri mkuu wa Nchini Blaziniar.Tangu anazaliwa maisha yalikuwa mazuri kupita kiasi huku wazazi wake wakijitahidi kumpatia kila alichokihitaji.Waliishi kama wako peponi huku pesa kwao ikiwa sio tatizo.
Uzuri aliojaaliwa Geneviv ulianza kuonekana tangu akiwa mdogo hali ambayo ilizidi kuwaongezea fahari mzee Rwakatare na mkewe.Kila aliyemuona mtoto Geneviv alishindwa kujizuia kumsifia.Sura yake iliyokuwa na mchanganyiko safi wa baba na mama ulizidi kumfanya aonekane kama malaika…
“you have beared a very cute angel sir,congrats!”
(umezaa mtoto mzuri sana mzee,hongera sana)
Hiyo ilikuwa ni kauli kutoka kwa mmoja kati ya wafanyakazi wenzake mzee Rwakatare akimsifia kwa kuzaa mtoto mzuri kiasi kile.
Bi Patricia naye alikuwa akipokea sifa kila alipopita na mwanae hali iliyozidi kumpa kichwa na kumfanya ajione kama mama wa malaika.
”Atawasumbua sana vijana wa kiume akikua huyu,kama wewe ulivyonisumbua kipindi nakutafuta darling…”
Mzee Rwakatare alimtania mkewe wakati wakipata chakula cha jioni na mtoto wao Geneviv.Bi Patricia alitabasamu huku akimbusu mumewe shavuni.
Siku zikawa zinasonga kwa kasi huku Geneviv akizidi kukua na kupendeza zaidi, urembo wake ukizidi kujionyesha dhahiri hali iliyomfanya aonekane tishio mbele ya kila aliyemtazama.
Alipotimiza miaka saba wazazi wake wakaona bora wamuanzishe shule.Akatafutiwa shule nzuri yenye hadhi ya kimataifa, st Benard Blaziniar academy,shule iliyokuwa ikisifika kwa kutoa elimu bora kwa nadharia na vitendo.Baada ya taratibu zote kukamilika Geneviv akaanza shule.Aliahidi kwa wazazi wake kuwa atasoma kwa bidii mpaka afike chuo kikuu.
“I want to be a doctor daddy! I want to heal the world…”
(Nataka kuwa daktari baba,nataka kuuponya ulimwengu)
Geneviv alikuwa akimwambia baba yake asubuhi wakiwa ndani ya gari lao akimpeleka shule.
“Sure! Go for it and you can be what you you want to be”
(Hakika utakuwa kama unavyotaka kuwa ukijipangia malengo vizuri na kuyatekeleza)
Mzee Rwakatare alikuwa akimtia ujasiri bintiye kuwa anaweza kuwa daktari ikiwa atajiwekea malengo madhubuti ya kusoma kwa bidii.
“Let education be your only heritage daughter coz when everything has gone the future still remain dark”
(Ikazanie sana elimu ndio iwe urithi pekee maishani mwako, vitu vyote vitakapopita, maarifa yatabaki kuwa mwanga pekee wa maisha yako)
Baada ya kumfikisha shule,Geneviv alipokelewa na mwalimu na kuelekezwa utaratibu wa Shule.Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa Geneviv kuanza shule.Alikuwa amechoka kufungiwa ndani kila siku,akaona huo ndio muda muafaka wa kuanza kufurahi na wenzake.Alijiwekea nadhiri ya kusoma kwa kadri ya uwezo wake wote ili azidi kuwafurahisha wazazi wake na kutimiza ndoto yake.
Baada ya siku chache tu tangu Geneviv ajiunge na Shule ya st Bernard Blaziniar, wanafunzi karibu wote na walimu walishamfahamu kutokana na uzuri aliojaaliwa.Wengine wakambatiza jina na kuanza kumuita “Cute Angel”. Usingepata shida kumtafuta kwani kila kona ya shule alifahamika. Akapata marafiki wengi huku wavulana anaosoma nao Grade one (darasa la kwanza) wakijigonga kila mmoja akitaka awe mchumba wake.
“Geneviv njoo tudimbedimbe mi niwe baba wewe uwe mama” aliongea mwanafunzi mmoja aliyeitwa Kim darasani na kusababisha darasa zima licheke.
Ukiacha uzuri na shani alivyokuwa navyo Geneviv,pia alitokea kuwa mwelewa “Bright” darasani hali ilyomfanya azidi kuwa kivutio kwa walimu wake na wanafunzi.
Kadri siku zilivyokuwa zinaenda mbele umaarufu wa Geneviv ukawa unaongezeka.
Nyumbani nako hali ilizidi kuwa shwari huku baba yake mzee Manuel Rwakatare na mkewe bi Patricia wakizidi kuonyeshana mapenzi motomoto. Amani na upendo vikazidi kutawala ndani ya familia ya mzee Rwakatare hali iliyozidi kumpa furaha Geneviv.Akawa anazidi kukua vizuri kimwili, kiakili na kiroho, kwani alifundishwa pia kumcha Mungu.
****************************************
Katika kipindi hiki chote, baba yake alikuwa bado ni mfanyakazi wa wizara ya madini na nishati huku akipokea mshahara mnono na marupurupu yaliyomfanya aweze kuyamudu maisha ya familia yake kwa kiwango cha juu kabisa.Alianzisha vitega uchumi vingi nchini Blaziniar na katika nchi jirani ya Tanzania.Pamoja na kwamba alipata mshahara mkubwa na mke wake naye alikuwa akipokea mshahara mnono, bado siri ya utajiri wao uliokuwa unazidi kukua kila ilipoitwa leo haikufahamika.Kwa makadirio ya haraka ilitosha kusema kwamba mafanikio makubwa aliyokuwa nayo mzee Manuel Rwakatare yalizidi kipato chake halisi.
Mambo yakaanza kubadilika ofisini kwake mara baada ya Raisi mpya, mhe. James Kahungo “the JK”, kuingia ikulu ya Blaziniar.Raisi huyu mpya mwana mageuzi halisi aliwataka watumishi wote wa wizara zote nyeti kuorodhesha mali walizokuwa wanazimiliki na kueleza namna walivyozipata.
Tofauti na maraisi wengine ambao nao walikuwa wakitoa mkwara kama huo bila kusimamia utekelezaji, James kahungo alionyesha kudhamiria kiuhakika kuwapunguza wahujumu nchi.Miezi mitatu tu tangu aingie madarakani,watumishi zaidi ya mia tatu walisimamishwa kazi kwa kosa la ubadhirifu na kujilimbikizia mali kinyume na sheria ya nchi ya Blaziniar.
Kivumbi kikahamia kwenye wizara ya Madini na Nishati ambako uozo mkubwa ulifichuliwa wa hujuma nzito zilizokuwa zikifanyika.Mzee manuel Rwakatare, baba yake Geneviv naye akawa miongoni mwa waliokumbwa na Ufagio wa chuma.Alisimamishwa kazi baada ya kugundulika kuwa ameingiza hasara ya mamilioni ya pesa kwenye ofisi yake.Mahakama ikaamuru mali zake zote isipokuwa nyumba aliyokuwa anaishi zitaifishwe ili kufidia deni alilokuwa anadaiwa.
Ilikuwa vigumu sana kwa mzee Manuel Rwakatare kukabiliana na hali halisi.Alishazoea kucheza na mamiloni ya pesa,leo ghafla anafukuzwa kazi na mali zake zote kufilisiwa! hakutaka kuamini haraka kuwa ni kweli yamemkuta. Akaanza kuhangaika kwa waganga kutafuta ni nani aliyemloga bila mafanikio…akaanza pia kwenda kuroga usiku na mchana ili arudishwe kazini lakini wapi! Mwisho akajikuta akiishiwa mbinu. Mkewe bi Patricia akawa anajitahidi kumfariji mumewe na kumtuliza kwa maneno matamu lakini hgakufanikiwa.
“Mume wangu yote tumwachie mungu, mshahara wangu utatosha kutufanya tuishi vizuri na mwanetu atasoma bila shida, wewe kinachokuumiza ni nini? Calm down please my Huz, everything gonna be alright”
Bi patricia alikuwa akimbembeleza mumewe usiku baada ya kuona hali ya mumewe inazidi kuwa mbaya, chakula hali wala usingizi hapati.Pamoja na kujaribu kumfariji usiku kucha kila siku, bado haikusaidia kitu.Mzee Rwakatare alikuwa amekata tamaa kabisa…kila kitu kilipoteza maana kwake.Akaona njia bora ya kutoa mawazo na mfadhaiko ni kunywa pombe! Akaanza kidogokidogo kunywa pombe,kumbe ndio alikuwa anaongeza matatizo.
Maisha yakaanza kubadilika kwa kasi ya ajabu, kutoka kwenye umilionea hadi kwenye ufukara. Akiba ya Pesa zilizokuwa zimesalia akawa anazitumia kunywea pombe…”From Hero to Zero”
ndivyo wambea wa mitaani walivyoanza kumuita na kumbeza baada ya habari kuzagaa karibu kila kona ya nchi juu ya kufukuzwa kwake kazi.Ni katika kipindi hiki Geneviv alikuwa akijiandaa kufanya mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya msingi. Hakufahamu mara moja ni nini kimemtokea baba yake kwani muda mwingi alikuwa yuko shule akijiandaa na mitihani.
“Mama mbona dadii siku hizi haendi kazini?”
Geneviv aliuliza swali ambalo lilikuwa kama msumari wa moto kwa Bi Patricia. Ilibidi atumie uongo kumridhisha Geneviv kuficha aibu ya mumewe.
“Dadii yuko likizo mwanangu,ameamua kupumzika nyumbani”
Geneviv hakuridhika na jibu hilo lakini kwa jinsi alivyozisoma hisia za mama yake kwa haraka akajua lazima kuna kitu ambacho mama yake anamficha.Akauliza swali lingine ambalo nalo lilikuwa gumu…
“Lakini mbona siku hizi anachelewa sana kurudi nyumbani na akija anakuwa ananuka pombe…kwani ameanza lini kunywa Pombe? Mwalimu shuleni ametufundisha kuwa kunywa pombe ni vibaya na ni tabia hatarishi,sasa mbona baba ameanza kunywa?”
Geneviv alikuwa akiendelea kumshambulia mama yake kwa maswali mfululizo ambayo yote Bi. Patricia alishindwa kuyajibu.
“Basi mngoje akirudi umuulize mwenyewe maana mimi nashindwa kuyajibu.”
Alijitetea Bi Patricia na kabla hata hajamalizia ,wote walisikia mlango ukigongwa kwa nguvu,wakajua baba mwenye nyumba karudi.Geneviv akanyanyuka na kukimbilia mlangoni kwenda kumfungulia baba yake.
Tofauti na alivyozoea kumuona,mzee Rwakatare alikuwa tofauti kabisa,hali iliyomfanya Geneviv arudi nyuma kwa hofu…
“Whats wrong with you daddy?”
Aliuliza Geneviv kwa sauti iliyokuwa ikitetemeka kwa hofu.Mzee Rwakatare alikuwa amelewa kupita kiasi ,akishindwa hata kutembea vizuri kiasi cha kujiegemeza kwenye mlango kama mgonjwa,ile Geneviv anafungua tu mlango,mzee Rwakatare alidondokea kwa ndani na kuanguka sakafuni kama gunia …Puuh!
“Daddy! Are you sick? Mama njoo umuone daddy…”
alipaza sauti kwa nguvu Geneviv na kuanza kukimbilia ndani alikomuacha mama yake.Alikuwa ameshtuka kupita kiasi akidhani baba yake amepatwa na jambo baya.Hakujua kuwa Starehe ya pombe ndiyo iliyomfanya awe vile.
Hata kabla ya kumuona,Bi Patricia alishajua kilichomsibu mumuwe.Alichokifanya ni kumtuliza mwanae Geneviv ambaye alionekana kuchanganyikiwa,akampeleka chumbani kwake na kumsihi alale mpaka asubuhi na kumhakikishia kuwa baba yake hakuwa na tatizo lolote.Kweli Geneviv alikubali kulala kwa shingo upande huku maswali mengi yasiyo na majibu yakipishana kichwani mwake.
Baada ya kuhakikisha Geneviv ametulia Bi Patricia alirudi mlangoni na kumkuta mumewe akiwa bado palepale chini akikoroma kutokana na kuzidiwa na pombe.Kwa upole alimuinua na kumpeleka chumbani kwao.Alimvua nguo na kumpeleka bafuni ili angalau azinduke baada ya kuoga maji ya baridi.Kweli alifanikiwa kwani baada ya kummwagia maji mengi ya baridi Fahamu zilimrudia na pombe zikamuisha kichwani.Baada ya kumuogesha vizuri,Bi Patricia alimshika mkono mumewe na kumpeleka chumbani ambapo alimlaza vizuri na kumuacha apumzike.
Alipohakikisha kuwa kila kitu kimetulia Bi Patricia alienda chumbani kwa mwanae Geneviv.Alimkuta akiwa bado hajalala.Alikuwa amejikunja kitandani huku ameukumbatia mto wake.Aligundua namna mwanae alivyopatwa na mshtuko kwa kumuona baba yake katika hali ile.Akaamua kumfariji na kumfanya asahau kila kitu.Alianza kumfanyia utani kama walivyozoea kufanyiana kila siku na baada ya muda mfupi Geneviv alikuwa tayari ameshasahau yote yaliyotokea,wakawa wanacheka kwa furaha.
Kelele za vicheko zilimshtua mzee Rwakatare ambaye aliamka na kuanza upya kuvaa nguo.Japokuwa pombe ilikuwa imepungua lakini bado akili yake ilikuwa haijatulia.Alifikiri mkewe na mwanae wanamcheka yeye kwa sababu amelewa sana,kumbe haikuwa hivyo.Akajikuta hasira zikianza kumpanda na mara akainuka na kuanza kufoka kwa sauti. Bi Patricia aliposikia mumewe anafoka alitoka haraka na kumucha Geneviv akijiandaa kulala.Akawa anatembea kwa haraka kuelekea chumbani kwao, kabla hata hajafika akamuona mumewe akitoka kwa jazba chumbani.Wakakutana mlangoni…
”Mnachekacheka nini na mwanao? mnanicheka mimi sio? Sasa leo mtanijua!”
Aliongea kwa ukali mno mzee Rwakatare, akimfokea mkewe kama mtoto mdogo.Bi patricia alibaki ameduwaa akimshangaa mumewe.Tangu waoane karibu miaka kumi na tano iliyopita hakuwahi kumuona mumewe akiwa katika hali kama ile. Bila hata kusubiri mkewe ajitetee mzee Rwakatare akaanza Kurusha ngumi na mateke kama anapigana na mwanaume mwenzake.Mkewe akaamua kukimbilia chumbani bila ya kupiga kelele hata kidogo akihofia mwanae Geneviv angejifunza kitu kibaya.
Alipoingia chumbani alitaka kuwahi kujifungia kwa ndani lakini Mzee Rwakatare akamuwahi na kuusukuma mlango kwa nguvu.Akaingia na kuufunga mlango kwa ndani.Kilichoendelea humo ikawa ni kipigo mtindo mmoja.Bi Patricia alijitahidi kujitetea lakini wapi…baadae akaanguka chini na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na maumivu huku damu nyingi zikimtoka puani na mdomoni.Baada ya kuona mkewe amedondoka na kupoteza fahamu,mzee Rwakatare akatoka na kuufunga mlango kwa nje.Akahamia kwenye chumba anacholala mwanae.
Kitendo cha Geneviv kumuona baba yake akiingia chumbani mwake kilimfanya moyo umlipuke kwa hofu.Alishasikia ugomvi uliokuwa unaendelea chumbani kwa wazazi wake, akajua sasa ni zamu yake.Tangu aanze kuwa na akili hakuwahi kupigwa hata kibao na baba yake,akabaki akisubiri aone kitakachomtokea.
Mzee Rwakatare baada ya kumuona mwanae akiwa amejawa na hofu kiasi kile,anajikuta nguvu zikimuishia na kuanza kumuomba msamaha mwanae.Geneviv alishindwa kuelewa nini lengo la baba yake na akabaki akimkodolea macho huku akishindwa kuificha hofu yake.Mzee Rwakatare akawa mpole ghafla na akasogea na kukaa karibu na geneviv juu ya kitanda chake.Bado Geneviv akawa anatetemeka mwili mzima kiasi cha kufanya kijasho chembamba kimtoke na kuiloanisha Night dress ndogo aliyokuwa ameivaa.Dakika kama tatu zikapita huku wakiwa bado wanatazamana,mwishoni Geneviv alishindwa kujizuia na kumuuliza baba yake kwa sauti ya kutetemeka,
“Where is my mum,Why do you act like this to us?
(Mama yangu yuko wapi,kwanini unatufanyia hivi)
Kwa mara ya kwanza Mzee Rwakatare akaligundua kosa alilolifanya,akajikuta akikosa jibu la kumpa mwanae…akiwa bado anajikanyaga, Geneviv alimsukuma kwa nguvu na kukimbilia chumbani aliko mama yake,alipofika mlangoni akakuta mlango umefungwa kwa funguo, akawa anagonga kwa nguvu akimtaka mama yake amfungulie…akiwa bado anagonga,akaona kitu chini ya mlango ambacho kinamshtua mno.Aliona michirizi mikubwa ya damu ikichuruzika kupitia chini ya mlango kutoka ndani ya chumba alimo mama yake.Nguvu zikamuishia na taratibu akakaa chini na kuzigusa zile damu akiwa bado haamini.
“Dady, did you kill my mother? I hate you… “
Geneviv aliongea kwa sauti kubwa na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani.Mzee Rwakatare akiwa amechanganyikiwa akatokea mlango wa nyuma na kutokomea gizani akielekea kusikojulikana.Geneviv akazidi kupiga mayowe yaliyowaamsha majirani ambao ndani ya muda mfupi walikusanyika kutaka kujua kumetokea nini.
Geneviv akisaidiana na majirani waliuvunja mlango na kufanikiwa kuingia chumbani ambako walimkuta mama yake akiwa amelala chini huku damu nyingi zikimtoka puani na mdomoni.Uso mzima ulikuwa umevimba kiasi cha kutotambulika…Geneviv akajikuta mwili wote ukimlegea akiwa haamini alichokiona, ghafla na yeye akaanguka na kupoteza fahamu.
************************************************
Bi patricia alikuja kurudiwa na fahamu baada ya siku mbili.Alipofumbua macho tu,sauti ya kwanza kuisikia ilikuwa ni ya mwanae Geneviv aliyekuwa amekaa pembeni yake akilia huku akisali kwa sauti ya chini, ndani ya wodi ya upasuaji ya hospitali ya Planet Health Aid.Kumbukumbu za matukio yote yaliyompata zilikuwa zimepotea kutokana na majeraha makubwa aliyokuwa ameyapata sehemu za kichwani na kifuani.
“Hapa ni wapi?” Aliuliza Bi Patricia huku akizishangaa dripu za maji na dawa zilizokuwa zinatiririka kuingia mishipani mwake.Kitendo cha kufumbua macho na kuuliza hapo ni wapi kilimshtua Geneviv aliyekuwa amezama kwenye kilio na Sala ya kumuombea mama yake.
“She is awake, Nurse Please come quick, my mother is back into her counciousness”
Aliongea Geneviv kwa sauti kubwa huku akiwa na furaha na akakimbia mpaka kwenye chumba cha nesi aliyekuwa anamhudumia mama yake.Sekunde chache baadae Geneviv alirudi akiwa ameongozana na nesi. Bi Patricia alikuwa bado akijaribu kukumbuka ni nini kilichomtokea mpaka akawa hapo.
Geneviv akawa anamshukuru Mungu kwa kumrejeshea fahamu mama yake huku machozi yakizidi kumiminika kwenye mashavu yake laini.Nesi alimtumliza Geneviv kwa kumwambia kuwa mgonjwa anahitaji kupumzika zaidi kwani alipata majeraha makubwa hivyo kelele zingemuongezea maumivu.Geneviv alielewa haraka na akatulia kimya akimtazama mama yake usoni alikokuwa amefungwa bandeji kubwa.
“Pole mum, My dad is a devil,I hate him…”
Aliongea Geneviv huku akimpiga busu mama yake.Hapo Bi Patricia akaanza kukumbuka yaliyomtokea mpaka akawa hpo hospitalini.Aliumia sana moyoni mwake, na kilichomuumiza haikuwa majeraha na maumivu aliyoyapata, aliumizwa zaidi na Geneviv ambaye aliyashuhudia yote na kujifunza kitu kibaya akilini mwake.
“Don’t cry for me Geneviv, im okay and everything is fine, Pray God for your daddy, don’t hate him.”
Aliongea Bi Patricia kwa taabu akimsihi binti yake kuchukulia kawaida yote yaliyotokea na kuzidi kumwomba Mungu kwani yeye ndiye mweza wa yote.
Bi Patricia aliendelea kutibiwa kwa siku kadhaa na hali yake ilipokuwa nzuri akaruhusiwa kurudi nyumbani.
Kwa siku zote alizokuwa Hospitalini, mumewe hakuwahi kuja hata mara moja kumjulia hali yake.Msaidizi mkubwa akawa ni mwanae pekee Geneviv ambaye ilibidi aache kwenda shule kwa takribani wiki mbili akimhudumia mama yake.Kipindi ambacho Geneviv alikuwa haendi shule, wenzake ndio walikuwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kufanya mtihani wa mwisho wa kumalizia elimu ya msingi.
Aliendelea kumuomba Mungu amsimamie katika wakati mgumu aliokuwa nao.Kwa kipindi chote hicho Mzee Manuel Rwakatare alikuwa hafahamiki yuko wapi kwani hata nyumbani kwake alikuwa hakanyagi.
“Mum why cant we report dad on police station for the pain he has caused you?”
(mama kwanini usimshitaki baba polisi kwa maumivu aliyokusababishia?)
Aliuliza Geneviv wakati akimpoozea mama yake uji.Pamoja na maumivu aliyosababishiwa na mumewe,Bi Patricia bado alikuwa anampenda na alishamsamehe kwa yote yaliyotokea.
“Mwanangu Geneviv,matatizo ya kifamilia humalizwa na wanafamilia wenyewe kwa msaada wa Mungu baba wa Mbinguni,kwenda polisi ni kuongeza matatizo kwani hawatatusaidia chochote.Mungu anatufundisha kuwapenda wanaotufanyia mabaya, kusamehe
na kusahau kama yeye anavyotusamehe dhambi zetu,nakuomba usimchukie baba yako,msamehe kwani ni shetani ndio anamtumia kwa sasa,jifunze kusamehe…”
Bi Patricia alikuwa akimpa darasa zito binti yake kwani alionekana kuanza kumchukia baba yake.Wakiwa bado wanaendelea na mazungumzo yao, walisikia mlango ukigongwa kwa nguvu.Wakajua “Simba mtu amerudi”. Geneviv akainuka na kwenda kufungua mlango.Alikuwa ni baba yake,mzee Rwakatare.Japokuwa ilikuwa ni asubuhi,alionekana ameshalewa kama mtu aliyelala kwenye kilabu cha pombe.Bila hata salamu, mzee Rwakatare aliingia mpaka ndani alikomkuta mkewe akinywa uji alioandaliwa na mwanae.
“Karibu mume wangu,habari za asubuhi!” alimpokea kwa moyo mkunjufu mumewe.Mzee Rwakatare hakujibu kitu, akaanza kufoka.Safari hii alikuja na hoja mpya akimtuhumu mkewe kuwa anatembea na bosi wake na ndio maaana wakaandaa njama za kumfukuzisha kazi. Bi patricia hakujibu kitu akawa anamtazama mumewe usoni kwa huruma. Geneviv alikuwa amesimama mlangoni akishuhudia yote yaliyokuwa yakiendelea. Ghafla mzee Rwakatare alimvamia mkewe pale alipokuwa amelala akiuguza majeraha yake ya kupigwa ambayo yalikuwa bado hayajapona.
“Si naongea na wewe? Mbona hunijibu…kiburi sio?”
Kabla hata Bi Patricia hajajibu lolote, alishtukia akipigwa kibao kizito usoni, damu zikaanza kumtoka masikioni,puani na mdomoni.
Geneviv alishindwa kuvumilia kitendo kile alichokiona.kwa nguvu zake zote akaibeba stuli iliyokuwa mbele yake na kuinyanyua juu, kisha akaishusha kwa nguvu kichwani kwa baba yake.Ilitua kisawasawa utosini na kumfanya mzee Rwakatare apige yowe kubwa kisha akadondoka chini na kutulia kimya…alipoteza fahamu.
“Umefanya nini Geneviv, si nilikwambia usilipe ubaya kwa ubaya?” aliongea Bi patricia huku akijikongoja kuamka kitandani na kumuinamia mumewe pale chini huku akijifuta damu zilizokuwa zinavuja baada ya kupigwa kibao na mumewe.
Geneviv alibaki akimshangaa mama yake, Pamoja na maumivu yote aliyokuwa anapewa na mumewe bado alikuwa akimtetea!
“No mum,no mum, it pain my heart, cant tolerate to see this…im walking away”
Aliongea Geneviv na kuanza kukimbia kuelekea nje akiwa haelewi anakokwenda. Hakukusudia kumuumiza baba yake,lakini pia hakuweza kuvumilia kuona mateso aliyokuwa anayapata mama yake.
Hakukumbuka hata kuvaa viatu,akatoka hivyohivyo huku akikimbia kama aliyerukwa na akili.Alikimbia umbali mrefu sana mpaka akaanza kuhisi mwili wote ukiishiwa nguvu.Akatafuta mti wenye kivuli na kujitupa chini huku machozi yakimtoka kama chemchemi.Taratibu usingizi ukaanza kumpitia…
****************************************
Mzee Rwakatare alikuja kushtuka baada ya masaa manne tangu alipopoteza fahamu kwa kupigwa na kitu kizito kichwani. Alijikuta amelala chumbani kwake huku mkewe Bi Patricia akimpepelea kwa kanga yake na kiyoyozi alichokisogeza karibu kabisa na kitanda.
“Pole mume wangu, nisamehe kwani mimi ndio chanzo cha yote”
Alikuwa akiongea Bi Patricia kwa sauti ya chini huku machozi yakimtoka. Mzee Rwakatare alifumbua macho akiwa hakumbuki kilichomtokea, alichokihisi ni maumivu makali sehemu ya utosini.
“What happened to me!” Alihoji mzee Rwakatare kwa sauti ya chini,mkewe hakumjibu kitu, akabaki akimtazama usoni kwa huruma.Baada ya muda kumbukumbu zikaanza kumrudia upya.Alikumbuka kila kitu kuanzia siku ya kwanza alipompiga na kumjeruhi vibaya mkewe na kisha kumtelekeza chumbani akiwa amepoteza fahamu.Alikumbuka alivyoshinda kwenye baa za pombe kwa wiki mbili mfululizo huku akiwa hajui mkewe anaendeleaje ingawa alisikia kuwa alikuwa amelazwa.Alikumbuka pia jinsi alivyoingia kwa vurugu asubuhi hiyo na kuanza kumpiga upya mkewe japokuwa alijua kabisa kuwa bado hajapona.Kumbukumbu zake ziliishia hapo…
“What happened to me?....” alirudia swali lake lilelile lakini Bi Patricia hakumjibu kitu zaidi ya kuendelea kububujikwa na machozi.Kilichomshangaza Mzee Rwakatare ni kule kuzinduka na kujikuta yuko mikononi mwa mkewe.kwa matukio aliyokuwa anamfanyia aliamini isingekuwa rahisi kwa mkewe kuendelea kumpenda na kumjali kiasi kile.Alipomtazama tena usoni,aligundua mkewe alikuwa na makovu makubwa ambayo ni yeye ndiye aliyemsababishia.Alijikuta dhamira yake ikimshtaki kwa uovu aliomfanyia mkewe waliyetoka naye mbali kimaisha.
“Patricia…”
Bi Patricia alishtuka kumsikia mumewe akilitaja jina lake kwani tangu wampate mtoto wao Geneviv, mumewe aliacha kabisa kumuita jina lake…akitumia zaidi mama Geneviv au My Darling!
“Abee mume wangu!” aliitikia Bi Patricia kwa adabu huku akijifuta machozi.
“Naomba nisamehe mke wangu.Najua nimeuumiza sana moyo wako Darling, Najua nimekufanya ulie sana mke wangu…I know…I know! But please 4give me…I will never hurt you again.”
Mzee Rwakatare alishindwa kuyazuia machozi yasimtoke.Alimvuta mkewe na kumkumbatia kwa nguvu.Bi Patricia hakujibu kitu zaidi ya kumwambia kuwa yote alimwachia Mungu na alishamsamehe kwa sababu anampenda.
“Mwanangu Geneviv yuko wapi? Hebu mwite nimuombe msamaha sababu najua yeye ndiye aliyeumia zaidi”.
“Ngoja nimuangalie chumbani kwake…Aliinuka Bi Patricia kwa kujikongoja na kuelekea chumbani kwa Geneviv.Alishajua kuwa hayupo ila alitaka tu kwenda kuhakikisha.”
*********************************************
“Oyaa washkaji eeeh…huyu si ndo yule Cute Angel Geneviv wa sculi kwetu?”
“Ndo mwenyewe mwana! Halafu mi nilikuwa namtamani siku kibao useme ndio alikuwa ananimwaga kila nikimuaproch!”
“Hata mimi nilikuwa namlia taiming siku kibao ila nilikuwa namgwaya si unajua mtoto mwenyewe alivyo juu!”
“Leo kajilengesha kwenye 18 zetu…ful kujisevia”
Hayo yalikuwa ni mazungumzo ya vijana wanne waliokuwa wametoka porini kuvuta bangi baada ya kutoroka shule.Walimkuta Geneviv akiwa amelala chini ya mti kutokana na uchovu wa kukimbia juani akitoroka kwao baada ya kumjeruhi baba yake kwa kumpiga na stuli mpaka akapoteza fahamu wakati akimpiga mama yake.
Akiwa usingizini alisikia sauti za watu wakichekelea kwa furaha.Aliposhtuka alikuta vijana wapatao wanne wamemzunguka na kabla hata hajakaa sawa alijikuta akivamiwa mwilini na kubanwa pale chini kiasi cha kushindwa hata kufurukuta.Mmoja alimziba mdomo huku wengine wakimvua nguo.Kufumba na kufumbua nguo alizokuwa amezivaa zilichanwachanwa na kumuacha akiwa mtupu.Akajua kilichokuwa kinataka kutokea.
Hakuna kitu alichokuwa anakiogopa maishani mwake kama kubakwa.Tangu awe mkubwa hakuwahi kumjua mwanaume hata siku moja na aliapa kujitunza mpaka atakapokuja kuolewa.Hakuwa tayari kuamini kuwa usichana aliokuwa akiutunza kama yai ndio ulikuwa unatolewa kwa aibu na maumivu makubwa namna ile.Alijitahidi kufurukuta lakini wapi,akataka kupiga mayowe ya kuomba msaada lakini hakuweza…akashuhudia kijana wa kwanza akifungua zipu yake na kumuinamia pale chini.Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kufumba macho huku akiuma meno.Kilichofuatia ikawa ni maumivu makali kupita kiasi ambayo hakuwahi kuyapata maishani mwake.
Baada ya yule wa kwanza kumaliza, alishuhudia wa pili akijiandaa…akajua huo ndio ulikuwa mwisho wake.Alijikaza mpaka naye akamaliza, akashuhudia watatu naye akijiandaa…akajikuta fahamu zikimtoka polepole kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayapata.
Wale vijana waliendelea kumfanyia ushetani ule Geneviv kwa zamu zamu mpaka wote wanne walipotosheka baada ya kurudia karibu mara tatu tatu.Wakamuacha akiwa amepoteza fahamu wakitokomea kusikojulikana.
Geneviv alikuja kushtuka baada ya kuhisi baridi kali ikimpiga.Aliposhtuka akajikuta yuko palepale chini ya mti, huku nguo zake zikiwa zimechanwachanwa.Alitaka kuinuka,maumivu makali yakamrudisha chini.Akawa anajaribu kukumbuka kilichomtokea,akapeleka mkono wake kwenye ikulu yake changa,kulikuwa kumeharibiwa vibaya mno…ndipo hapo kumbukumbu zilipomrudia,alikuwa amebakwa.Alibaki amepigwa na bumbuwazi akitamani hiyo iwe ndoto lakini haikuwa hivyo,ukweli ukabaki kuwa palepale,alibakwa.
Alijaribu tena kuinuka,lakini safari hii alisikia maumivu makali kupita kiasi.Akajilaza chali huku akilia kilio cha kuomboleza.Alijikuta akimchukia mno baba yake mzee Rwakatare kwani bila yeye asingepatwa na tukio baya namna ile.
“I hate my daddy! I hate men, they are Devils”
Sunday, October 11, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1
Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...
-
Ni wiki nyingine ambapo mwenyezi Mungu ametujaalia kukutana katika busati letu la mahaba ambapo tunajadiliana mambo mbalimbali yanayohusu ...
-
HASH POWER 7113 NI matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko poa. Ni wiki nyngine tunapokutana kwenye busati letu ambapo tunajuzana na kuja...
No comments:
Post a Comment