Saturday, August 13, 2011

...

Safari iliendelea mpaka kwenye mji mdogo wa Tunduma kisha jijini Mbeya. Kila kitu kilikuwa kigeni kwa Gamutu, alikuwa akishangaa kuanzia mazingira ya nje na ndani, watu na kila kitu alichokiona.
Baada ya kuwasili jijini Mbeya, kwa kuwa muda ulikuwa umeenda walilazimika kulala hadi kesho yake ndipo waendelee na safari.
"Kwa nini ulikuwa unasumbua watu kwenye gari?" Bi Lubunga alimuweka chini mjukuu wake. Vitendo alivyovifanya kwenye basi vilimkera sana bibi yake.
"Bibi nilikuwa naona watu wakifanya mambo ya ajabu barabarani ndiyo maana nikawa napiga kelele."
"Mambo ya ajabu kama yapi?" alizidi kuhoji Bi Lubunga.
"Mwanzo nilikuwa naona watu ambao hawajavaa nguo wakicheza barabarani, baadaye nikaona watu wengi wakiwa wanachimba kaburi katikati ya barabara," Gamutu alizidi kujitetea.
"sasa hayo machache ndiyo yaliyokufanya uwe unapiga kelele njia nzima? Kumbuka kuwe wewe ulifanyiwa tambiko la maisha ukiwa mdogo. Hakuna mtu anayeweza kukuchezea kirahisi, kuwa na roho ya kiume," alisema bi Lubunga na Gamutu akatingisha kichwa kama ishara ya kuelewa kile alichoelezwa.
Siku ile walilala Mbeya mpaka kesho yake ambapo walipanda mabasi ya kuelekea jijini Dar es salaam kisha Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...