Monday, August 1, 2011

BIG BROTHER 2011 WINNERS


Hatimaye ile shoo kubwa zaidi barani Afrika, Big Brother Amplified, juzi Jumapili ilifikia tamati baada ya siku 91 ambazo washiriki walipaswa kukaa mjengoni kabla ya washindi kupatikana kutimia. Kismati kilikuwa ni kwa mshiriki wa Nigeria, Karen na Wendall wa Zimbabwe ambao ndiyo waliotangazwa kuwa washindi baada ya kupata kura nyingi katika wiki ya mwisho.

Katika wiki ya mwisho ya mchakato huo, washiriki saba waliokuwa wamesalia, Vina, Hannie, Lomwe, Sharon, Luclay, Wendall na Karen walitakiwa kupigiwa kura kutoka nchi mbalimbali za kuendelea kubaki, na mwenye kura chache angetolewa. Wa kwanza kutoka alikuwa ni Lomwe ambaye hakupata kura hata moja, akafuatiwa na Hannie, Lomwe na Sharon ambao walipata kura moja moja.


Luclay alipata kura mbili na kuwa wa mwisho kutoka, wakati Wendal alipata kura nne kutoka Zambia, Zimbabwe, Namibia na Kenya huku Karen akiibuka kidedea kwa kupata kura sita kutoka Nigeria, Angola, Ghana, Msumbiji, Tanzania na moja kutoka sehemu nyingine za Bara la Afrika.

KAREN IGHO
Mwanadada aliyezaliwa kwenye mji wenye machafuko ya kidini ya muda mrefu wa Jos nchini Nigeria, Karen, 27, ambaye hana kazi maalum alipotangazwa kua mshindi, alijikuta akishindwa kujizuia kutoa machozi ya furaha, akapiga magoti na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu wake. Dola za Kimarekani laki mbili (sawa na shilingi milioni 300) zimemfanya kulala masikini na kuamka tajiri.

WENDALL
Rubani kutoka jijini Harare, Zimbabwe, Wendall, 23, alipoatangazwa kuwa mshindi sambamba na Karen, alikurupuka na kukimbiliamahali mama yake alipokuwa, wakakumbatiana na kuanza kusherehekea ushindi. Mwenyewe anaeleza kuwa alidhani Luclay na Karen ndiyo wangeibuka washindi, hivyo anajisikia kuwa na bahati ya mtende. Kama mwenzake, Wendal naye amejinyakulia Dola za Kimarekani laki mbili (sawa na shilingi milioni 300).

Hii ni mara ya kwanza kwa Big Brother kuwa na washindi wawili walioondoka na kitita sawa na kukamilisha maana ya neno ‘Amplified’.
Katika wiki ya mwisho ya mchakato huo, washiriki saba waliokuwa wamesalia, Vina, Hannie, Lomwe, Sharon, Luclay, Wendall na Karen walitakiwa kupigiwa kura kutoka nchi mbalimbali za kuendelea kubaki, na mwenye kura chache angetolewa. Wa kwanza kutoka alikuwa ni Lomwe ambaye hakupata kura hata moja, akafuatiwa na Hannie, Lomwe na Sharon ambao walipata kura moja moja.

Luclay alipata kura mbili na kuwa wa mwisho kutoka, wakati Wendall alipata kura nne kutoka Zambia, Zimbabwe, Namibia na Kenya huku Karen akiibuka kidedea kwa kupata kura sita kutoka Nigeria, Angola, Ghana, Msumbiji, Tanzania na moja kutoka sehemu nyingine za Bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...