Friday, August 26, 2011

HOTUBA YA SUGU MJENGONI ILIYOZUA MTITI

HASH POWER 7113/ Acreditation: Joseph Mbilinyi 'Sugu'

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uhai, afya njema na kunipa fursa ya kipekee ya kufanya maajabu yenye manufaa kwa taifa langu; Kwa Baraka zake, niliweza kung’ara kwenye sanaa na kuwa nyota wa muziki wa Bongofleva; Kwa uwezo wake, leo nimekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini; Na kwa mapenzi yake, mimi Msanii wa Bongofleva sasa nimekuwa Waziri Kivuli wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha maoni na mapendekezo ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni, na Michezo, kwa mwaka wa fedha 2011/2012, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99(3) na (7) toleo la 2007.
Mheshimiwa Spika, natambua na kuthamini imani na heshima kubwa niliyopewa na wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini, katika uchaguzi mkuu uliopita. Kwa pamoja tuliweza kuthibitisha kuwa Mbeya Mjini ni Jimbo la Wajanja. Licha ya kuletewa mabomu ya machozi na virungu, bado hakuna yeyote kati yetu aliyeogopa. Uwongo haukuweza kufunika ukweli na hata rushwa haikuweza kurubuni akili.
Kwa pamoja tulijitoa mhanga kulinda kura zetu bila woga, na hatimaye Dunia nzima inajua na imekubali kuwa mimi ndiye SUGU na CHADEMA si chama legelege.
Mheshimiwa Spika, namshukuru na kumpongeza kwa moyo wa dhati kabisa Katibu Mkuu wangu, Dk. Willbrod Peter Slaa, na makamanda wote wa CHADEMA nchi nzima kwa kazi kubwa tuliyoifanya katika uchaguzi mkuu uliopita, na kwa harakati nzito tunazoendelea kuzifanya za kuikomboa nchi hii. Watapiga kelele sana, lakini hatutarudi nyuma, tunasonga mbele mpaka kieleweke.
Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima namshukuru Kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Freeman Aikael Mbowe (Mbunge), Naibu Kiongozi Mhe. Kabwe Zuberi Zitto (Mbunge), na Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani, Mhe. Tundu Lissu, kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri Kivuli wa wizara hii nyeti; pia kwa ushirikiano wao mkubwa wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu ya kibunge.
Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati wadau wote wa Sekta ya Habari, Utamaduni na Michezo, kwa kutuamini na kuthamini kazi kubwa ya uwakilishi inayofanywa na Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, hata kuamua kutupa ushirikiano mkubwa katika maandalizi ya hotuba hii. Naomba niwatambue baadhi ya wadau hao kwa shukrani kama ifuatavyo;
· Baraza la Habari Tanzania (MCT)
· Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika – Tanzania (MISA-TAN)
· Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)
· Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)
· Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
· Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na,
· Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
SEKTA YA MICHEZO
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali ilieleze Bunge ni kwanini kocha wa netiboli, Simone Mcknnis
rais wa Australia aliyetia saini Septemba mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitatu kufundisha netiboli nchini lakini alikatiza mkataba wake na kuondoka kurudi kwao Australia kwa kile kilichoelezwa kushindwa kutimiziwa masharti ya mkataba wake.
Mheshimiwa Spika, taarifa zinaeleza kuwa kocha huyo alikatiza mkataba kutokana na kukosa kulipwa mshahara wake na Chama cha Netiboli Tanzania, Chaneta, kama mkataba wa makubliano baina yake na CHANETA ulivyohitaji kutekelezwa.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inasema hii ni aibu kwa nchi yetu, na kwanini watendaji wachache watutie aibu watanzania wote?
Mheshimiwa Spika, ili kuboresha Sekta ya Michezo, kuipa msisimko wa kutosha na kuchochea ajira kupitia sekta hii, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa Serikali kuanzia mwaka wa fedha wa 2011/2012, ianze kufanya mambo yafuatayo;
Mamlaka ya Viwanja vya Michezo ianzishwe
Mheshimiwa Spika,
Kwa mantiki hiyo, Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuanzia mwaka wa fedha 2011/2012 iwe inatenga angalau wastani wa shilingi bilioni 70 kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa viwanja hivyo. Viwanja vijengwe kila mwaka kimoja kwa utaratibu wa kuhakikisha kila kanda inakuwa na kiwanja chake.
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
SEKTA YA UTAMADUNI
Mheshimiwa Spika
Mheshimiwa Spika,
· Kufanya utafiti wa watu wote waliotoa mchango mkubwa wa kihistoria katika kupigania Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano ili waweze kukumbukwa na michango yao kuenziwa.
· Kutambua maeneo, majengo, na sehemu mbalimbali zenye umuhimu mkubwa wa kihistoria.
· Kupitia matukio muhimu ya historia yetu ili yaweze kuelezewa katika mwanga wa kihistoria. Hii ni pamoja na Uhuru, Mapinduzi, Muungano, Uasi wa Jeshi, Azimio la Arusha, Operesheni Vijijini na Vita ya Kagera.
· Kukusanya vielelezo mbalimbali vyenye umuhimu mkubwa wa kihistoria kutoka watu binafsi, taasisi binafsi na nje ya nchi ili hatimaye vitu hivyo, viweze kuingizwa katika historia yetu kwa ajili ya kuwa ni urithi wa vizazi vijavyo.
· Kuandika ripoti maalum juu ya historia yetu na matukio mbalimbali ili yaweze kutunzwa kama sehemu ya historia yetu maalum.
· Kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuenzi utamaduni wetu muhimu pamoja na watu mbalimbali ambao walichangia katika matukio mbalimbali kwa namna ya pekee na ambao historia yetu haijawakumbuka ipasavyo.
LUGHA YA KISWAHILI KAMA SEHEMU YA UTAMADUNI WETU
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika, elimu bora utolewa kwa lugha sahihi, na lugha sahihi kwa nchi yetu ni lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa Prof. Kahigi, mtaalam, mchambuzi na mtafiti wa lugha ya kiswahili aliyebobea ni kwamba hakuna nchi yeyote Duniani ambayo imeendelea kwa lugha ya kukopa. Hivyo basi, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutumia lugha ya Kiingereza katika kutoa elimu kwa vijana wetu.
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
SEKTA YA SANAA
Mheshimiwa Spika, nianze na sekta ya Sanaa. Na hapa natangaza maslahi, kuwa mimi ni msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) na nimekuwa kwenye fani hii kwa muda mrefu sasa. Kwa uzoefu wangu na kwa niaba ya Kambi rasmi ya Upinzani, nachukua fursa hii kuieleza serikali kwamba; “Sanaa si mapambo au burudani tu kama ilivyozoeleka, bali Sanaa ni ajira inayoweza kubadilisha maisha ya Mtanzania yeyote anayejihusisha nayo na inaweza kabisa kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya Bajeti ya Serikali, ikiwa Serikali yenyewe, itadhamiria kwa dhati kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia hii”.
Mheshimiwa Spika, Ripoti moja nchini Marekani ya mwaka 2007 ilisema, nanukuu; “Makampuni yanayotengeneza na kuuza kazi za hatimiliki yataendelea kuwa moja ya nguvu kubwa za uchumi wa Marekani, kwani mapato yatokanayo na filamu, muziki, michezo ya video, na mifumo ya kompyuta yanachangia zaidi ya asilimia kubwa ya Pato la Taifa na kuajiri takribani watu milioni 5.4…” mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa sekta ya Sanaa ikifanyiwa mapinduzi makubwa inaweza kabisa kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya bajeti ya Serikali yetu na kuchangia maendeleo ya taifa hili. Ikiwa Sanaa inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa kubwa kama Marekani; Je, Tanzania tuna maendeleo gani ya kujivunia hata tupuuze Sanaa? Bado hatujaipa sekta hii umuhimu wake unaostahili;
Matokeo yake Mheshimiwa Spika, Wasanii pamoja na Serikali bila kujua, wamekuwa wakinyonywa kimapato na Wadhamini, Wazalishaji, na Wasambazaji wa kazi za Sanaa, hususan kwenye biashara ya kuuza muziki na filamu. Kwa mujibu wa utafiti wa Dkt. Jehovaness Aikaeli ambaye ni mchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema sekta ya muziki pekee ikifanyiwa maboresho, inaweza kuiingizia Serikali mapato ya kodi ya wastani wa shilingi bilioni 50 kwa mwaka.
Mheshimiwa Spika, tafiti chache zilizowahi kufanyika, ukiwemo utafiti wa Taasisi ya RULU/BEST – AC, wa mwaka 2007/08, zimeonyesha kuwa Wasanii na Serikali kwa pamoja, wamekuwa wakipoteza mapato mengi yatokanayo na biashara ya kazi za sanaa, hususan muziki na filamu kama ifuatavyo;
· Maharamia wameendelea kurudufisha santuri na kanda za muziki, filamu na kazi nyingine za sanaa, na kujipatia mapato haramu kwa jasho la Wasanii, lakini hakuna hatua kali zinazochukuliwa kukomesha hali hii.
· Wasanii wengi wamekuwa wakiingia mikataba isiyo na manufaa kwao baina yao na Wadhamini, Wazalishaji, Wasambazaji wa kazi za Sanaa na hivyo kunyonywa kimapato, kwa sababu tu ya kukosa uelewa mzuri wa masuala ya mikataba na kutokuwepo udhibiti wa kutosha wa Serikali.
· Serikali kwa mwaka 2007 pekee, ilipoteza mapato ya muziki, ya jumla ya shilingi bilioni 71 sawa na asilimia 0.5 ya Pato la Taifa.
· Kodi inayokusanywa na Serikali katika Sekta ya Muziki, inapatikana katika asilimia 12 tu ya kiwango cha mapato kinachotakiwa kulipiwa kodi kwenye sekta hiyo.
· Hasara inayotokana na ulipaji mdogo wa kodi kwa taifa kwenye sekta ya muziki pekee, inakadiriwa kuwa sawa na asilimia 0.1 ya Pato la Taifa na hasara hiyo ilitegemewa kuongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2007.
· Wakati wa utafiti iligundulika kuwa ni asilimia 12.5 tu ya Wafanyabiashara wa kazi za Sanaa, ndio waliokuwa wamelipa mirabaha, asilimia 87.5 hawakuwa wamelipa.
Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na wizi na uharamia huu wa kazi za Sanaa na kuokoa mapato ya Wasanii na ya Serikali, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza yafuatayo;
COSOTA iwe Mamlaka
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na.7 ya mwaka 1999 ifanyiwe marekebisho kwa lengo la kuipa meno zaidi ya kulinda haki na kuhakikisha Wasanii wananufaika na kazi zao. Jedwali zima lenye marekebisho yanayopendekezwa katika sheria hiyo, limo katika Kiambatanisho Na. 1 cha hotuba hii. Moja ya mapendekezo yaliyomo kwenye kiambatanisho hicho, yanalenga kuifanya COSOTA kuwa chombo chenye nguvu zaidi katika kulinda kazi za Wasanii kuliko ilivyo hivi sasa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika sehemu ya marekebisho tunayopendekeza, Kambi rasmi ya Upinzani tunataka Sura Na. 218 ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, ifanyiwe marekebisho ili kuunda Mamlaka ya Hakimiliki Tanzania (COPYRIGHT REGULATORY AUTHORITY OF TANZANIA (CORATA) badala ya kuiacha COSOTA kama ilivyo hivi sasa. Mamlaka haya yakishaundwa yatakuwa na nguvu zaidi ya kushughulikia mambo mbalimbali ya kazi za wasanii,yawe ndio msimamizi na mratibu wa masuala ya Hakimiliki kwa kushirikiana na vyama vya msingi vya wasanii vilivyopo chini ya BASATA,kama vile Chama Cha Muziki Wa Dansi Tanzania(CHAMUDATA) na kile cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Tanzania Urban Music Association (T.U.M.A), tofauti na sasa ambapo COSOTA imebakiwa na kazi ya kusajili kazi za wasanii na kukosa nguvu ya kuzilinda.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa mwenye Hakimiliki ana jukumu la kulinda haki zake kwa kwenda mahakamani pale anapoona haki yake imepokwa na mtu au kikundi chochote, bado ipo haja ya kuhakikisha kuwa Polisi wetu wa upelelezi wanahusika moja kwa moja katika kulinda haki za Wasanii.
Mathalan, nchini Marekani hawana polisi wa kulinda hakimiliki moja kwa moja, lakini Shirika lao la Upelelezi (FBI), limekuwa likifanya uchunguzi wa mara kwa mara kuhusu hakimiliki za wasanii, kila kunaporipotiwa suala la wizi wa kazi za msanii, na limekuwa linahusika moja kwa moja katika kutoa ushahidi na kusaidia kupatikana kwa haki ya msanii husika.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa taasisi za Serikali: Polisi na Forodha washirikiane kwa karibu na Mamlaka ya Hakimiliki na Hakishiriki tunayotaka ianzishwe (CORATA), kukomesha uharamia wa kazi za Sanaa. Jeshi la Polisi liunde kitengo cha kukabiliana na wasiotekeleza sheria ya hakimiliki. Forodha watengeneze utaratibu wa kutoza kodi kikamilifu kwenye kazi za muziki, filamu na Sanaa nyingine zote zinazouzwa nje ya nchi. Na mashirika ya uzalishaji wa kazi za muziki –waunde ushirikiano na taratibu zao za kukabiliana na uharamia wa kazi za sanaa kwa mapana yake.
Mheshimiwa Spika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari mwaka huu, wakati akizindua kampeni ya kuzuia malaria ambayo iliwashirikisha baadhi ya wasanii, aliahidi kuundwa kikosi kazi (task force) kitakachowashirikisha COSOTA, Polisi, Tume ya ushindani, TRA, BRELA, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wasanii mbalimbali wanaojihusisha na sanaa ili kutafuta ufumbuzi dhidi ya uharamia na wizi wa kazi za Sanaa.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka wizara kuliarifu Bunge hili, je kikosi kazi hicho kiko wapi mpaka leo? Na kama kiliundwa, kiliundwa kwa taratibu zipi, na kwanini suala hilo haliko wazi?
Mradi wa Stickers kwenye kazi za Sanaa
Mheshimiwa Spika, mbali na marekebisho hayo ya kisheria na kimfumo tuliyopendekeza, Kambi rasmi ya Upinzani pia tunaitaka Serikali ndani ya mwaka wa fedha wa 2011/2012, itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuanzisha utaratibu rasmi wa kuwa na Stickers kwa ajili ya kazi zote za Sanaa, hususan kwenye kanda na Santuri za muziki, filamu, na kazi zote za Sanaa zinazoshikika na kuuzika. Hapa tunashauri kuwa mamlaka tunayotaka ianzishwe, yaani COPYRIGHT REGULATORY AUTHORITY OF TANZANIA) ishirikiane kwa karibu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kuandaa utaratibu mzima wa kuwa na Stickers hizo na jinsi ya kuusimamia.Na sio kuwaachia tena watu binafsi kusimamia hili.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inaamini kuwa utaratibu rasmi wa kuwa na Stickers ukitumika sekta ya Biashara ya Kazi za Sanaa inaweza kupata mafanikio ya kuridhisha ndani ya muda mfupi. Mfano mzuri ni Sticker yenye nembo ya TRA inayowekwa kwenye bidhaa za Konyagi. Faida kubwa ambayo itapatikana kwa kuwa na Stickers za TRA kwenye kazi za Sanaa ni kuwa stickers hizi zitawezesha kubaini kazi halisi (Original) iliyofanywa na msanii mhusika dhidi ya kazi za bandia zilizorudufishwa au kughushiwa.
Sambamba na hilo ni kwamba mapato ya Wanamuziki, Watunzi wa filamu na washirika wao pamoja na Serikali yataongezeka na hivyo mchango halisi ya sekta hii kwenye uchumi wa nchi utakuwa wazi.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inatambua kuwa baadhi ya makampuni ya usambazaji na utangazaji wa kazi za Sanaa, yamekuwa yakijiwekea yenyewe Stickers kwenye kazi zao za Sanaa, lakini bado Stickers hizo hazijaweza kuwasaidia vya kutosha katika kulinda kazi hizo, kwani bado umma hauna taarifa za kutosha, na mbaya zaidi Stickers zenyewe zimekuwa zikighushiwa hivyo kutotoa msaada unaotakiwa.
Kwa kutilia maanan hilo, Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa ni muhimu sana utaratibu wa kuwa na Stickers rasmi za kiserikali kwa kazi zote za Sanaa, ukaanzishwa mara moja ndani ya mwaka wa fedha 2011/2012, ili kuokoa mapato ya Wasanii na mapato ya kodi ya Serikali yanayopotea kwenye sekta hii ya sanaa.
Mheshimiwa Spika, pia tuna taarifa kuwa Wasanii wengi kutoka nje ya nchi wanaofanya maonyesho mbalimbali hapa nchini wamekuwa hawatozwi kodi licha ya kulipwa fedha nyingi. Kwa hiyo, tunaitaka Serikali kuanzia mwaka wa fedha wa 2011/2012, ihakikishe kuwa Wasanii hao wa nje ya nchi ambao wamekuwa wakilipwa dola laki 1hadi dola laki 4 kwa onyesho moja hapa nchini, wawe wanatozwa kodi ya kutosha, ili fedha hizo ziongezee bajeti kuu ya Serikali na kuwasaidia Watanzania wengi maskini.
Mheshimiwa Spika, tunaitaka Serikali kwa kushirikiana na vyombo husika, iweke utaratibu wa kuhakikisha kuwa pale Msanii wa ndani anapofanya onyesho au kazi ya pamoja na Msanii kutoka nje, basi kuwe na mgawanyo mzuri na wa haki wa mapato kati ya Msanii huyo wa Nje na Msanii Mzawa. Pendekezo hili linazingatia ukweli kuwa kwenye maonyesho ya muziki yanayofanywa kwa kuwashirikisha kwa pamoja Wasanii wa Nje na wale wa Ndani, wa Nje wamekuwa wakilipwa fedha nyingi sana kuliko wale wa ndani, licha ya kuwa kazi iliyofanywa ni moja na wote wameingiza mapato.
Mheshimiwa Spika, ili kuboresha Sekta nzima ya Sanaa nchini, na kuhakikisha inaongeza ajira zenye tija, na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji uchumi, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe;
· Serikali ndani ya mwaka wa fedha wa 2011/2012,pamoja na kufanyia kazi tafiti zilizokwishafanywa na wadau mbalimbali wa sanaa, ifanye utafiti mahsusi na wa kina kuhusu Sekta nzima ya Sanaa (Feasibility Study), ili kubaini fursa na vikwazo vyote vilivyopo, na kuainisha njia na mikakati kabambe ya kuboresha na kuisimamia sekta husika, kwa manufaa ya Wasanii na uchumi wa nchi.
· Kupitia matokeo ya utafiti huo, Wizara ndani ya mwaka wa fedha 2011/2012, iandae Mpango mahsusi wa Maboresho ya Sekta ya Sanaa, ambao pamoja na mambo mengine, ulenge kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato ya Sanaa na kuchochea ajira nyingi na zenye tija kwa vijana.
· Chuo Kikuu cha Sanaa cha Bagamoyo kipandishwe hadhi na kuwa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Kawawa cha Bagamoyo (Kawawa Memorial University – Bagamoyo). Lengo liwe ni kuhakikisha kuwa chuo hiki kinatoa mafunzo yote ya hali ya juu ya mambo ya sanaa, michezo na utamaduni kwa vijana wa Kitanzania na wale wanaotoka ng’ambo, huku tukimuenzi Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa, kwa mchango wake mkubwa katika taifa hili alioutoa kwenye uongozi na Sanaa.
· Serikali ihakikishe kuwa asilimia 90 ya bajeti zote za Wizara, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali zinazotengwa kwa ajili ya kunaksisha ofisi, iwe inatumia kazi za sanaa na samani zinazopatikana hapa Tanzania au zinazotokana na ubunifu wa Watanzania. Hii itachochea ajira katika kazi za Sanaa na kuweka ushindani wa kibiashara ambao utainua ubora wa kazi hizo.
· Masomo ya Sanaa yarudishwe katika ngazi zote za elimu katika shule za binafsi na serikali, ili kuchochea ubunifu na umahiri wa vijana katika kazi za sanaa na kuinua vipaji vyao mbalimbali.
· Serikali ihakikishe mafunzo ya Sanaa yanatolewa kwa vyuo vya elimu ili kuweza kupata walimu wa kutosha wa sekta hii.
· Mashindano ya ubunifu wa kazi za Sanaa yaanzishwe yakiwa ni sehemu ya mashindano ya michezo ya UMISHUMTA na UMISETA.
Kashfa ya Nyumba ya Sanaa
Mheshimiwa Spika, Nyumba ya Sanaa ilianzishwa mnamo 1972 kwa madhumuni ya kutoa mafunzo ya Sanaa kwa vijana, wanawake na wasiojiweza pamoja na kutafuta masoko ya Sanaa na kazi za mikono. Hata hivyo, kuanzia mwaka 1995 kumekuwepo hali ya kutoelewana baina ya wajumbe wa Bodi ya wadhamini baada ya kutiliana shaka wenyewe kwa wenyewe, pia kati ya Bodi ya Wadhamini na Wanachama waanzilishi wa Nyumba ya Sanaa.
Mheshimiwa Spika, matokeo ya hali hiyo ni kufunguliwa kwa kesi mahakamani. Katika kesi hiyo, iliyotolewa hukumu tarehe 24 Februari, 2005, Msajili aliamua kufuta rasmi usajili wa Bodi ya Wadhamini ya Nyumba ya Sanaa akiwataka wakabidhi mali na shughuli za NYUMBA kwa asasi mbadala. Uchunguzi uliofanywa na Kambi rasmi ya Upinzani umebaini kuwa tangu kutolewa kwa hukumu hiyo, Bodi haijawahi kukasimisha amali na majukumu ya Nyumba ya Sanaa kwa asasi mbadala, na badala yake imeendelea kuwepo na kupelekea Nyumba hiyo kuendeshwa kama kampuni binafsi kwa faida ya wajumbe wachache wa Bodi.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani ina taarifa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo iliyofutwa na baadhi ya wajumbe wake wameleta mwekezaji ambaye wameshaingia naye ubia kimkataba, kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa katika eneo lenye jengo la sasa. Izingatiwe hapa kuwa mwekezaji atapaswa kulivunja au kubadilisha mfumo wa jengo la sasa la Nyumba ya Sanaa, ndipo aweze kujengwa la ghorofa.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani, inaitaka serikali na Bunge lako tukufu lizingatie yafuatayo;
· Tujue kuwa Nyumba ya Sanaa hivi sasa inawanufaisha wachache ambao si walengwa waliokusudiwa. Tufahamu kwamba wanufaika hawa hawana rekodi ya uwekezaji katika Nyumba ya Sanaa, hivyo wanavuna matunda yaliyopandwa na wengine hasa kupitia ushirikiano mwema baina ya serikali ya Tanzania (kupitia Ikulu), Norway (kupitia shirika la NORAD) na Uholanzi (kupitia shirika la NOVIB).
· Tutambue kuwa Nyumba ya Sanaa ilikuwa ni mlango wa masoko ya Sanaa na kazi za mikono, hivyo kutokuwepo kwake kunakwamisha juhudi za wazalishaji kazi za sanaa wa Tanzania kuweza kushiriki vyema masoko na hasa soko la pamoja la Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Spika, kwa kuyazingatia yote hayo na kwa manufaa ya wadau wote wa Sanaa na taifa zima kwa ujumla, Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka serikali ichukue hatua zifuatazo kuhusiana na Nyumba ya Sanaa:-
Mheshimiwa Spika, kwanza tunataka Nyumba ya Sanaa irudishwe Serikalini kwa Mdhamini Mkuu wa Serikali ili mchakato wa uanzishwaji wa Bodi huru ya kusimamia malengo yake anuai ufanyike. Uhuishaji wa Nyumba ya Sanaa utachangia sana kuongeza ajira na pato la taifa, hivyo kupunguza tatizo la uzururaji na kilio cha masoko ya kazi za sanaa.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tangu kufutwa kwake mnamo mwaka 2005, Nyumba ya Sanaa imeendelea kufanya biashara pamoja na kuingia mikataba ya biashara mpaka sasa, Kambi rasmi ya Upinzani tunaitaka serikali ifanye tathmini na ilipwe kodi kutokana na faida ya biashara zilizoendeshwa mara baada ya kusitishwa uendeshaji wake.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani tunaitaka Serikali isitishe mara moja uvunjwaji wa jengo lililopo sasa, kwani ni utalii na ni alama ya taifa inayoonyesha jinsi serikali za Norway na Tanzania zilivyothamini juhudi za wasanii na wazalishaji kujikwamua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa.
Tunataka Nyumba ya Sanaa ifufuliwe upya bila kubadili malengo yaliyopelekea kujengwa kwake, na badala yake kila kitu kiboreshwe kwa kuheshimu malengo yale yale. Tunaamini Serikali hii inayojiita Serikali sikivu, itaheshimu matakwa ya Watanzania hususan Wasanii ambao pasipo shaka yoyote ile wanataka Nyumba yao irudi kwenye mikono salama kama tulivyopendekeza.
Ahadi ya Studio ya Wasanii
Mheshimiwa Spika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii Studio ya kufanyia kazi zao. Hata hivyo, baadaye wananchi na wadau wengi wa sanaa, nikiwemo mimi binafsi, tulishangaa kusikia Studio hiyo wamepewa NGO binafsi ya Tanzania House of Talent (THT)! Pia Rais aliahidi na kutoa nyumba ya Serikali kwa Wasanii ambayo ingetumika kuendeshea Studio husika, lakini nyumba hiyo ya Serikali iliyotolewa na Rais sasa iko chini ya THT na ndio makao ya THT!
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
SEKTA YA HABARI
Weledi na Maadili ya Uandishi wa Habari
Mheshimiwa Spika, vyombo vya habari ni taasisi muhimu sana katika ujenzi wa taifa lenye kufuata misingi ya demokrasia na utawala bora. Vyombo vya habari vina dhima kubwa ya kutoa habari na taarifa kwa umma wa Watanzania kuhusu mambo yanayohusu maisha yao na vilevile kutoa elimu na burudani. Vyombo vya habari ni kiungo muhimu cha kuunganisha jumuiya mbalimbali, kujenga utaifa na umoja na kuhimiza maendeleo.
Vyombo vya habari kwa ujumla wake ni taasisi yenye nguvu sana. Ina uwezo mkubwa sana wa kujenga na vilevile kubomoa ikiwa vitatumiwa na kujiendesha vibaya au kuingiliwa uhuru wake. Hivyo basi, wakati vyombo vya habari vina wajibu wa kufanya kazi kwa kuzingatia umakini, weledi na maadili ya uandishi wa habari, Serikali nayo ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha uhuru na haki za kutafuta na kupata habari vinalindwa.
Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiotiliwa shaka kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikikiuka kabisa maadili ya uandishi wa habari, wakiingilia faragha za watu binafsi, wakiandika habari ambazo hazikufanyiwa utafiti wa kutosha na kuwanyima hao wanaowaandika haki yao ya kuelezea upande wao wa habari husika.
Mheshimiwa Spika, kinachosikitisha zaidi ni pale ambapo baadhi ya waandishi wa habari na baadhi ya vyombo vya habari na ambavyo vimepewa dhamana kubwa na jamii wanapokubali kununuliwa na kutumiwa na baadhi ya watu wenye nguvu ama za kisiasa au za kifedha ili kuendeleza ajenda zao binafsi. Hili ni jambo lisilopendeza hata kidogo na halina mustakabali mzuri kwa amani na maendeleo ya nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, hili ni jambo ambalo wote tunatakiwa tulikemee kwa nguvu zetu zote na kila inapowezekana tuwaumbue na tuwataje wale wote wanaoshiriki katika matendo haya ambayo hayana nia njema sio tu kwa tasnia yenyewe ya habari kwa kuipa jina baya na kuipaka matope, bali kwa nchi yetu kwani tuna mifano dhahiri hapa Afrika na kwingineko duniani juu ya athari ambazo zimewahi kutokea vyombo vya habari vilipotumika vibaya.
Mheshimiwa Spika, taasisi yenye nguvu kama hii ni lazima iwe na wataalamu waliobobea kwenye fani kielimu, wenye kuzingatia weledi na wenye kuwajibika. Tunalihimiza Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambalo limeundwa na tasnia ya habari yenyewe kuweka na kusimamia weledi na maadili ya uandishi wa habari kuwa likaze kamba na lisilee vyombo vya habari ambavyo havina sifa wala uwezo wa kufanyakazi kwa weledi na uadilifu.
Sheria ya Haki ya Kupata Habari na Sheria
Mheshimiwa Spika, haki ya kupata habari ni haki ya msingi ya binadamu na inalindwa na Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni haki ambayo inamhusu kila Mtanzania bila ya kujali wadhifa au daraja lake kwenye jamii, umri au jinsia. Mwaka 2006, na nataka niamini kwa nia njema kabisa, Serikali ilianzisha mchakato wa kutunga sheria ya Uhuru wa Habari kwa kutoa rasimu ya muswada wa sheria hiyo.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo rasimu ya muswada huo ilikataliwa na wadau kwa sababu haikukidhi haja wala viwango vya sheria kama hiyo vinavyotakikana. Mwaka 2007, Serikali iliitikia wito wa wadau wa habari na haki za binadamu wa kutaka kuwepo na sheria mbili tofauti na kutenganisha rasimu yake ya Muswada wa Sheria ya Uhuru wa Habari na kutengeneza rasimu mbili, moja ya sheria ya Haki ya Kupata Habari na nyingine ya sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari.
Mheshimiwa Spika, hoja ya kutenganisha muswada huo ilikuwa na bado ni ya muhimu sana, kwa sababu sheria ya haki ya kupata habari ni mtambuka na inahusu haki ya kikatiba ya Watanzania wote. Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ni ya kisekta na inahusiana zaidi na kutoa mwelekeo wa jinsi vyombo vya habari vitakavyofanya kazi nchini.
Mheshimiwa Spika, mchakato huo ulipata muitiko mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu ambao kwa umoja wao walitembea nchi nzima kukusanya mawazo na mapendekezo ya wananchi kuhusu Sheria ya Haki ya Kupata Habari. Walipeleka mapendekezo yao kwa Serikali ili yaweze kujumuishwa katika mchakato wa utungaji wa sheria.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa Sheria hii ni muhimu sana, kwani itaimarisha utawala wa wazi na uwajibikaji. Utawala ulioshamiri katika mila za usiri ndio ulioifikisha Tanzania yetu mahali pabaya. Ndio chanzo cha mikataba mibovu na kushindwa kwa uwajibikaji kwa sababu tu watendaji wabovu wanaweza kujificha katika kinga ya usiri.
Mheshimiwa Spika, Sheria ya Haki ya Kupata Habari ni mtambuka kwani inagusa haki ya kila Mtanzania. Si sheria ya kuifanyia mzaha na kuifutika kwenye sheria nyingine ambayo inahusu kundi la watu wachache kama tunavyotaarifiwa kuwa Serikali inataka kuweka sheria hii chini ya ile ya Huduma za Vyombo vya Habari. Tunaitaka serikali izingatie kuwa Sheria ya Haki ya Kupata Habari itatunufaisha sote na si waandishi wa habari tu. Na ni lazima ifuate misingi ya kimataifa ya “usiri mdogo na uwazi mpana”yaani “minimum secrecy, maximum disclosure.”
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikitoa ahadi mwaka hadi mwaka kuhusu mchakato wa utungaji wa sheria hii muhimu. Lakini hadi leo hatujaona muswada wa sheria hiyo ukiacha ule ambao wadau wamependekeza. Kambi rasmi ya Upinzani tunaitaka Serikali ifanye hima kuuleta bungeni muswada wa sheria hiyo ndani ya mwaka huu huu, ili tuujadili na kupitisha sheria hiyo bila ya kukawia zaidi.
Mheshimiwa Spika, sisi tumepitia mapendekezo ya wadau wa sekta ya habari na tumejiridhisha kuwa yanakidhi haja ya kuboresha tasnia nzima ya habari na tayari yana ithibati ya wananchi. Kwa hiyo, mbali na kutaka muswada huo uletwe hapa bungeni ndani ya mwaka huu huu, Kambi rasmi ya Upinzani pia tunaitaka serikali kuhakikisha kuwa muswada itakaouleta uwe umezingatia maoni yote hayo ya wadau.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani tunaitahadharisha serikali kuwa isijaribu kuchakachua hata kidogo maoni hayo ya wadau, kwa sababu tumejiridhisha kuwa yana msingi na dhamira ya dhati ya kuboresha tasnia nzima ya habari na uhuru wake. Pendekezo la wadau limo katika Kiambatanisho Na. 5 cha hotuba hii. Tunachukua fursa hii kuwataarifa mapema wadau wote wa habari kwamba tutakuwa pamoja nao wakati wote wa harakati za kushinikiza muswada huo uletwe bungeni ndani ya mwaka huu. Tunataka sheria hiyo ipatikane mapema iwezekavyo ikiwa imebeba maoni yote ya wadau.
Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari
Mheshimiwa Spika, katika sera ya Habari na Utangazaji iliyotolewa na Serikali na kupitishwa na Bunge lako tukufu mwaka 2003, kipengele cha 2.2.2 ukurasa 15, kinaelekeza kwamba; “Sheria mbovu za habari ambazo zimekuwa zikikosolewa na kulalamikiwa kwa kuwa haziendani na misingi ya kidemokrasia zitadurusiwa, kurekebishwa au kufutwa.” Hivyo basi, Serikali iliahidi kuwa itatunga sheria mpya zinazoendana na wakati na kukidhi mahitaji ya kidemokrasia ya wananchi.
Mheshimiwa Spika, tunasisitiza kuwa mapendekezo ya wadau yanakidhi kwa kiwango kikubwa ahadi hiyo ya Serikali na wadau walizipitia sheria 27 zinazogusa habari na kupendekeza sheria 17 miongoni mwa hizo ama zidurusiwe, zirekebishwe au kufutwa. Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka serikali isiendelee kusuasua kwenye jambo hili na ilete muswada bungeni wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha.

1 comment:

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...