ILIPOISHIA:
Muda mfupi baadaye, wote tulikuwa
‘saresare maua’, akanisukuma kwa nguvu kwenye uwanja wa fundi seremala,
nikaangukia mgongo, akaja juu yangu kwa kasi, maandalizi ya mechi ya kirafiki
isiyo na jezi wala refa yakaendelea huku akionesha kunikamia kama Simba na
Yanga zinavyokamiana zinapokutana uwanjani.
SASA ENDELEA...
Kipyenga kilipolia tu, Shamila ndiye
aliyekuwa wa kwanza kugusa mpira, akawa anabutua mashuti ya nguvu na kunifanya
nihisi kama atanielemea na kunishinda ndani ya muda mfupi tu, jambo ambalo
kwangu lingekuwa aibu kubwa.
Nikajipanga na kuanza kwenda naye sawa,
akawa akipiga mashuti kwa kubutua, mimi naukontroo mpira na kumpiga chenga za
mwili, wakati mwingine nikawa natambaa na chaki kama Christiano Ronaldo, jambo
lililofanya kibao kigeuke, badala ya yeye kuwa ananishambulia kwa kasi, ikawa
mimi ndiyo namshambulia.
Ilibidi nitumie ujuzi wa hali ya juu
kuwahi kummaliza nguvu ili nimalize mchezo kwani Junaitha naye alikuwa
akinisubiri na sikujua alikuwa na lengo gani. Kutokana na jinsi nilivyokuwa
namshambulia Shamila kwa akili, haikuchukua muda mrefu, akatangaza kusalimu
amri, akanikumbatia kwa nguvu!
“Nakupenda sana Jamal, nataka unioe,
nataka niwe mkeo wa ndoa,” alisema Shamila kwa sauti kama mtoto mchanga,
nikamnong’oneza sikioni kwamba asiwe na wasiwasi, nitamuoa, nikamuona
akitabasamu na kuangukia upande wa pili kama mzigo. Haikuchukua muda, akawa
anakoroma kuonesha kwamba tayari alishapitiwa na usingizi mzito, hakujua kama
nilikuwa nacheza na akili yake.
Kwangu mimi ilikuwa ni zaidi ya ushindi
kwani nilijua sasa hatanisumbua tena. Harakaharaka nikainuka na kuchukua gwanda
zangu na kuzitia mwilini, ikabidi nirudi kwanza kwenye chumba changu.
Harakaharaka nikaenda kujimwagia maji huku nikitafakari kilichotokea muda mfupi
uliopita.
Kiufupi nilikuwa nimebadilika sana,
sikuwa Jamal yule ambaye hata mimi mwenyewe najijua. Awali nilikuwa muoga sana
wa wanawake, hata Raya, msichana aliyetokea kunipenda kwa moyo wake wote,
ilinichukua muda mrefu sana mpaka kuja kukutana naye kimwili lakini sasa,
nilikuwa kama jogoo, kila tetea anayepita mbele yangu sikuwa naona hatari
kumpitia. Hata sielewi ujasiri huo niliupata wapi.
Wakati nikiwa naendelea kujimwagia maji,
ni kama Junaitha alichoka kunisubiri kule chumbani kwake, nikashtukia akiingia
chumbani kwangu. Nilimtambua kuwa ni yeye hata kabla sijamuona kutokana na
jinsi alivyoniita.
“Mbona huji jamani, mi nakusubiri mpaka
nachoka bwana!” alisema huku akikaa kitandani. Nikamwambia kuwa nilikuwa
nasikia sana joto kwa hiyo niliamua kujimwagia maji kabisa.
“Sasa si ungekuja kulekule kwangu uoge?”
alisema. Kwa kuwa tayari nilishamaliza, nilijifunga taulo na kutoka.
“Utasababisha hawa watoto wajue siri
yetu bure! Nataka nikiingia chumbani na wewe uwe umeshafika,” alisema kwa sauti
yenye mamlaka, nikacheka huku nikijifuta maji. Alisimama na kusogea mlangoni,
akachungulia huku na kule, alipoona hakuna mtu, alitoka na kuusindika mlango.
Harakaharaka nilivaa nguo zangu,
nikatoka na kufunga mlango, nikatembea kwa umakini mpaka kwenye mlango wa
chumba cha Junaitha, nikausukuma, ulikuwa wazi, nikaingia mpaka ndani.
Wewe ni mwanaume wa kipekee sana Jamal,
samahani usione kama nakufosi kuwa na mimi kwa sababu nimekuzidi kila kitu na
hapa upo kwangu, hapana! Ni kwa sababu sijawahi kukutana na mwanaume kama wewe
maishani mwangu. Mtu anaweza kukuona mdogo kwa nje lakini una mambo makubwa
sana,” alisema Junaitha na kunisogelea, akanikumbatia kwa nguvu, nikalihisi
joto la mwili wake kwenye mwili wangu.
Japokuwa nilikuwa nimetoka kwenye mchezo
muda mfupi uliopita, kwa jinsi Junaitha alivyokuwa akihamasisha, nilijikuta
nikiwa tayari kwa mpambano mwingine, japokuwa hata sheria za mchezo hazikuwa
zikiruhusu kilichokuwa kinataka kufanyika.
Haukupita muda mrefu, tuliingia uwanjani
tena lakini tofauti na Shamila, Junaitha alikuwa na utaalamu wa hali ya juu.
Naye hakuwa na papara kama mimi, maandalizi ya kupasha viungo moto yalienda
taratibu, kipyenga kilipopulizwa, kila mmoja akawa anacheza kwa staili ya
kumvizia mwenzake, ladha ya mchezo ikawa tofauti kabisa na Shamila.
Mtanange wa kukata na shoka uliendelea,
hata sijui nguvu za kuhimili mikikimikiki nilizipata wapi kwa sababu kwa jinsi
nilivyomudu kucheza na mpira, hata Junaitha mwenyewe hakugundua kwamba nimetoka
kulisakata tena kabumbu muda mfupi tu uliopita.
Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa
kuashiria kumalizika kwa mpambano huo, Junaitha alikuwa hajitambui,
nikajikokota na mpira wangu kwapani kwa sababu kama sheria zinavyosema,
mchezaji akipiga hat trick anaondoka na mpira wake, nikavaa gwanda zangu na
kurudi chumbani kwangu, nikimuacha Junaitha naye anakoroma.
Nilipofika na kujitupa kitandani,
kutokana na jinsi nilivyokuwa nimechoka, sikuelewa tena kilichoendelea mpaka
nilipokuja kuzinduka alfajiri ya siku ya pili. Junaitha ndiye aliyekuja
kuniamsha, cha ajabu eti akawa ananilaumu kwamba kwa nini sikulala kule kwake,
akawa ananiuliza niliondoka muda gani? Nikajua kwamba kwa vyovyote na yeye
ndiyo alikuwa amezinduka alfajiri hiyo.
Kwa kuwa siku hiyo tulikuwa na ratiba
ngumu sana, tulianza kujiandaa, tukawaamsha watu wengine wote ambapo Shamila
alikuwa mgumu sana kuamka kwa madai kwamba bado mwili wake ulikuwa umechoka,
ikabidi Junaitha atumie nguvu.
Saa kumi na mbili juu ya alama, wote
tayari tulikuwa tumeshajiandaa, tukakaa mezani na kunywa chai iliyoandaliwa na Junaitha
kisha baada ya hapo, tukatoka. Ilibidi tutumie gari la Junaitha ambalo kabla ya
hapo, sikuwa najua kama anamiliki gari. Lilikuwa ni Toyota Alphard la kisasa,
akasema tukitumia ile Noah ya akina Firyaal itakuwa rahisi kutambulika.
Gari tulilopanda lilikuwa na vioo
tinted, jambo lililofanya iwe vigumu kwa mtu wa nje kuona kilichokuwa
kinaendelea ndani, Junaitha mwenyewe ndiyo akakaa nyuma ya usukani na mimi
nikakaa pembeni yake. Kwa jinsi tulivyokuwa tumejikausha, isingekuwa rahisi kwa
mtu yeyote kuhisi kwamba kuna mchezo ulikuwa ukiendelea kati yetu.
Hata Shamila mwenyewe, japokuwa mara kwa
mara alikuwa akinitazama kwa macho ya kuibia, hakuweza kuhisi chochote, achilia
mbali mpenzi wangu Raya ambaye muda wote alikuwa ametulia. Tulitoka na breki ya
kwanza ilikuwa ni kwenye kituo kikuu cha polisi, Junaitha akatutaka wote tubaki
ndani ya gari, akashuka na kuingia kituoni.
Baada ya kama dakika ishirini, alitoka
akiwa ameongozana na askari mmoja aliyekuwa na nyota nyingi mabegani, ambaye
alionesha ishara tu, askari zaidi ya sita wenye silaha wakaingia ndani ya difenda,
Junaitha akarudi kwenye gari letu na yule askari akaungana na vijana wake.
“Kuna watu itabidi tuwapitie,
mwanasheria wetu pamoja na yule mwandishi wa habari, nadhani wote tayari
watakuwa wanatusubiri sehemu tuliyokubaliana,” alisema Junaitha. Nikamuuliza
swali:
“Kwa hiyo hapa tunaelekea wapi?”
“Tulia jamal, mbona una haraka, nimesema
leo ndiyo leo na watu wote watatujua sisi ni akina nani. Shenaiza na Firyaal,
naomba mkaze mioyo yenu maana kinachoenda kutokea kwa baba yenu siyo kizuri
lakini lazima tufanye hivi,” alisema Junaitha, akawasha gari, tukaondoka huku ile
difenda ikitufuata kwa nyuma.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
hadithi zako zimeishia hewani unaziendelezea wapi?
ReplyDelete
ReplyDeleteMbona hizi hadithi zako haziendelei...Tatizo nini..au unaziendeleza wapi..?
We kaka upo mzima kweli? mbona kimya sanaaa umetuacha hewani tuambie wapi tufatilie hata kama kwa kulipia Thanks
ReplyDeleteMini ni mwandishi was riwaya niwapate vipi!?
ReplyDeleteMimi ni mwandishi was riwaya niwapate vipi,? Ninayo Kama?
ReplyDeleteDoa
Mbumbumbu
Salome
Sikujua
Chozi la fukara
Mbio za sakafuni
Bendera fata upepo
Elimu ya Samia
Village doctor
Mama alisema
Tafta mchumba
Ficra potofu
Mateso ya dada
Utabiri
Nikupenini
Laana
Wema wangu
Cheo
Mdimu
Sinto oa tena
Akili kichaka
Together
N.k no 0676570495