Friday, December 9, 2011

Walking Corpse! (uncensored)

HASH POWER 7113

WALKING CORPSE: MAITI INAYOTEMBEA
corpse in morgue
ILIPOISHIA:
Tukaenda kukaa kwenye mawe makubwa yaliyokuwa pembeni ya mto, mbali na makazi ya watu, mahali palipokuwa na miti mingi iliyoshonana. Tulipofika tu, kabla hatujafanya chochote, tulisikia sauti ya mtu akituamuru kutulia kama tulivyokuwa. Tukashtukia wanaume wanne wenye miili mikubwa na silaha za jadi wakitokeza kwenye miti, Kim alikuwa mjanja kwani aliruka kwenye mawe makubwa na kufanikiwa kutimua mbio, akaniacha peke yangu nikiwa sijui cha kufanya.
Mmoja kati ya wale wanaume alianza kumkimbiza Kim, wengine wakanizunguka na kuanza kunivutavuta. Nikashtukia mmoja akinivuta sketi yangu, akakata vishikizo na kuivuta kwa nguvu. Nikabakiwa na ‘skin tight’. Akanibeba juu juu na kunilaza juu ya jiwe kubwa. Nikawa napiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyenisikia. Sikuelewa wanataka kunifanya nini, nikahisi hatari kubwa mbele yangu.
 SASA ENDELEA…


Katika hali ambayo hata Shanice hakuitegemea, nyokamkubwa alianguka kutokajuu ya miti iliyokuwa imeshonana na kuwekagiza. Na kuangukia mgongoni mwa Yule mwanaume aliyekuwa amenishika na kunilaza juu ya jiwe. Nilimshuhudia akianza kutapatapawakatiyule nyoka mkubwa mweusi alipokuwa anamviringisha shingoni na kumkaba. Ilibidi wenzake waende kumsaidia, wakaachana na mimi kwa mufda, wakawa wanapambana ana nyoka yule mkubwa aliyekuwa anatema mate yenye sumu.
Walipambana naye kwa muda, lakini wakazidiwa ujanja,nyoka akamng’ata shingoni  yule mwenzao ambaye ndiye aliyetaka kunifanyia mchezo mchafu sekunde chache zilizopita, nikawaona wakihaha kuokoa maisha yake. Niliutumia muda huo kunyata kwenye mawe, nikaruka na kutimua mbio kimya kimya kuzamia kwenye miti mikubwa. Kama kuna siku ambayo niliwahi kutimua mbio siwezi kukumbuka, lakini ninachokumbukasiku ile nilikimbia kwa kazi kubwa sana.
Dakika chache baadaye nilikuwa nimeshatokeza kwenye njia ya waenda kwa miguu, nikageuka nyuma kuangalia kama kuna mtu alikuwa akinifuata, lakini kwa kudfra za mwenyezi Mungu hakukuwa na mtu. Nilizidi kukimbia bila kukutana na mtu yeyote. Mpaka nafika njia ya panda ya kuelekea kwetu, nilikuwa bado siamini kama nimenusurika kutoka kwenye mdomo wa mamba.
Kwa bahati mbaya au nzuri, nilipofika nyumbani nilimkuta mama akiwa anamwagilia bustani za maua mbele ya nyumba yetu. Kwanza alishangaa kuniona nikoitimua mbio, nikiwa pekupeku huku machozi yakiwa bado hayajakauka machoni mwangu.
“Wewe! Una nini?” alisema mama na kuacha kila kitu alichokuwa anakifanya.
“Mama rescue me! They want to rap me!” (mama niokoe wanataka kunibaka) nilisema huku nikilia, nikapitiliza ndani na kujifungia mlango kwa nje.
***
Kim alipokimbia alishindwa kuelewa upande alikokuwa aneleke, akajikuta badala ya kujikomboa anazidi kupotea. Yule mwanaume aliyekuwa anamfukuza alizidi kumkaribia, na alipotishia kumchoma na mshale, ilibidi Kim asalimu amri na kusimama.
“Nisamehe tafadhali, nitafanya chochote unachokitaka ilimradi msinidhuru mimi wala mchumba wangu,” alisema Kim huku akilia. Yule mwanaume hakumuelewa, alimshika nyuma ya suruali na kumnyanyua juu, akawa anatembea kwa kutumia vidole vya miguu yake. Baada ya kumburuza sana, hatimaye alimfikisha pale alipokuwa amewaachsa wenzake.
Tofauti na alivyotegemea, alipofika alishangaa wenzake wakiwa wamemzunguka mwenzao mmoja aliyekuwa amelala chali juu ya mawe. Kim alipotazama kwa haraka, alidhani Yule aliyelazwa pale katikati alikuwa ni Shanice, akazidi kuingiwa na hofu kuu kwenye mtima wake.
 Alimuachia Kim na kukimbilia pale wenzake walipokuwa wamezunguka, Kima akautumia muda hio kutoroka. Kama ilivyokuwa kwa mwenzake, naye alitimua mbio kali kupita maelezo kwenye msitu ule na baada ya dakika kadhaa akawa ameshafika kwenye njia ya waendsa kwa miguu.
Hakutaka hata kugeuka nyuma, alitimua mbio kurudi shuleni, hukuakiwa hakumbuki daftari zake aliziacha wapi. Alipishana na watu wengi njiani ambao walikuwa wakimshangaa, lakini hakujali, akatimua mbio kwa kadiri ya uwezo wake mpaka alipofika shuelni kwao.  



No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...